25 July 2013

MULUGO AWAGEUZIA KIBAO WAMILIKI WA SHULE



Na Anneth Kagenda, Bagamoyo
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi imegeuka mbogo baada ya kuhoji ni kwanini kuna shule zisizosajiliwa mitaani na zinaendelea kufumbiwa macho na kutoa elimu kwa wanafunzi jambo alilosema ni hatari kwa taifa.Pia imewaagiza Waratibu Elimu Kata kuhakikisha wa n a s amb a a kwe n y e shule zote za sekondari na kuangalia kama wanafunzi walioingia kidato cha tatu ni wale waliofaulu ama la kwa madai kuwa kuna shule nyingine wanafunzi walifeli lakini wanaendelea na masomo ya kidato hicho kama kawaida jambo ambalo ni hatari kielimu.

Hayo aliyasema wilayani Bagamoyo na Naibu Waziri wa Elimu, Philipo Mulugo mara baada ya kufungua Mafunzo ya Waratibu Elimu Kata Taifa yanayoendeshwa na Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM). Alisema ni jambo la kushangaza kuona kuna shule zimetapakaa mitaani wakati waratibu hao wapo na kusema kuwa ni kwanini wasitoe taarifa ili zishughulikiwe na ikiwa taarifa hazifiki mahali husika ni bora wakapiga simu yake ya mkononi moja kwa moja kuliko kuzifumbia macho jambo linalosababisha kuongezeka kwa watoto wengi wanaofeli.
"Kwa mfano hili la shule zisizo rasmi ninaomba sasa waratibu mnaopata mafunzo haya mara baada ya kutoka hapa hakikisheni mnatoa taarifa juu ya uwepo wa shule hizo na mkiona taarifa hazifanyiwi kazi piga simu yangu ambayo nimewapa leo na mkishindwa basi tumeni ujumbe mfupi wa maneno (sms) nitaukuta na nitajibu," alisema Mulugo.
Ku h u s u wa n a f u n z i kupandishwa madaraja bila kufaulu alisema: "Niliwahi kwenda katika shule moja sitaitaja lakini cha kushangaza nilikuta watoto ambao walifeli kidato cha pili wapo kidato cha tatu nikauliza na hawa vipi..., sikupata majibu hivyo basi baada ya hapa naomba mkafuatilie na mnipe majibu ili suala hili lifanyiwe kazi."
A l i s e m a h a k u n a anayependa kuadhibiwa juu ya matokeo mabaya ya wanafunzi, kulaumiwa na kuambiwa waziri ajiuzulu hivyo wizara yake itahakikisha kero zote zinazojitokeza inazifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuwatengenezea mazingira mazuri waratibu hao ili waweze kuisaidia wizara yake.
Wa z i r i Mu l u g o p i a aliwataka waratibu hao kuwa wavumilivu wakati Serikali ikishughulikia changamoto walizonazo ikiwamo zile za kutokuwa na ofisi huku akiwataka kuhakikisha wanaonesha mshikamano mara baada ya kufika katika shule hizo na kukuta madudu kwa kutoa taarifa kwake.
Naye Mtendaji Mkuu wa ADEM Dkt. Sisten Ma s s a n j a , a l iwa t a k a washiriki wa mafunzo hayo mara baada ya kumaliza ni vyema wakayafanyia kazi ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao.
"Ni matumaini yetu kuwa mafunzo haya mtayafanyia kazi ili yaweze kuleta matunda na mambo yaliyokuwapo awali yakiwamo ya wanafunzi kufeli yasiendelee lakini tunaandaa kozi mbalimbali ambazo mtazipata ili kujiongezea ufanisi katika kazi," alisema.
Mwenyekiti wa Mafunzo hayo, Richard Chambo alisema zipo changamoto mbalimbali zinazowakabili waratibu hao ikiwamo kuongezeka kwa majukumu hivyo ni vyema Serikali ikawatupia jicho la pili.
"Pia tunazo changamoto nyingine ambazo ni kutokuwa na ofisi, vitendea kazi, shule nyingi za kata kutokuwa na usafiri na mambo mengine mengi," alisema.



No comments:

Post a Comment