Na Elizabeth Joseph, Dodoma
MTU mmoja
anayefahamika kwa jina la Nyerere Bakari mkazi wa Makirinya, Wilaya ya Kondoa
anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua mwenzake kwa kumpiga risasi.Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Dodoma, David Misime alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake na kuongeza kuwa Bakari alifanya mauaji hayo mnamo Julai
23, mwaka huu, saa nane usiku.
"Marehemu huyo
alitambulika kwa jina la Abdallah Mgunda (25) ambaye ni mkazi wa Kwadelo
wilayani Kondoa ambapo mtuhumiwa alitumia silaha inayodhaniwa kuwa ni gobore
kwa kumpiga risasi zilizompata sehemu ya kifuani na kwenye mapaja na
kusababisha kifo chake."
"Chanzo cha
mauaji hayo kinadhaniwa kuwa ni ugomvi uliozushwa na mtuhumiwa huyo kuwa
marehemu alikuwa amelisha mifugo katika shamba lake," alisema Misime.Aidha alisema kuwa
mnamo tarehe hiyo majira ya saa 12 katika eneo la Nkuhungu Manispaa ya Dodoma
mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Imani Francis (28) ambaye pia ni mkazi wa
eneo hilo alikutwa ameuawa katika eneo la Itega kwa kupigwa na watu
wasiojulikana.
M i s i m e a l i e l
e z a k u w a uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu huyo alishakuwa na tuhuma
za kubaka na wizi wa unyang'anyi ingawa matukio hayo hayakuwahi kuripotiwa
polisi.
Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi
kwani ni kosa la jinai kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment