30 July 2013

MHASIBU HALMASHAURI AFARIKI AJALINI



. Na John Gagarini, Kibaha
ALIYEKUWA mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani, Pius Guda (53) mkazi wa Kwa Mathiasi amefariki dunia baada ya gari alilokuwa akiendesha kugongana uso kwa uso na gari lingine. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kibaha, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei, alisema kuwa marehemu alifariki papo hapo
. Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Julai 27, mwaka huu saa 9:56 usiku eneo la Njuweni Maili Moja wilayani Kibaha. Alisema marehemu alikuwa akiendesha gari aina ya Suzuki namba T 163 AMD liligongana na gari aina ya Scania namba T 819 na tela namba 279 AFP lililokuwa likiendeshwa na Abdu Athuman.
"Gari la marehemu liligongana na gari hilo la mizigo baada ya yeye kutaka kulipita gari lingine lori la mizigo aina ya Scania lenye namba T 461 JKT na tela namba T 341 DHA likiendeshwa na Jonathan Mungi, kisha kupoteza mwelekeo na kukutana na uso kwa uso," alisema Matei. Alisema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Tumbi, huku majeruhi mmoja Mungi akipatiwa matibabu kwenye hospitali hapo

No comments:

Post a Comment