30 July 2013

MBARONI KWA KUMILIKI MENO YA TEMBO,BUNDUKI



Na Cresensia Kapinga, Songea
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma limemtia mbaroni, John Kasimila (56), mkazi wa Kijiji cha Ligera kilichopo wilayani Namtumbo baada ya kukutwa akiwa na silaha mbili za moto, risasi mbili na kilo 50 za nyama inayosadikiwa ni ya tembo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mchana ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Deusdedit Nsimeki, alisema kuwa tukio hilo limetokea Julai 26, mwaka huu saa 9 usiku katika kijiji cha Ligela kwenye eneo la mbuga ya wanyama ya Hifadhi ya Taifa ya Selous.
Inadaiwa siku hiyo ya tukio askari wa idara ya wanyama pori ambao walikuwa kwenye doria kwenye mbunga ya Selous walifanikiwa kumkamata, Kasimila akiwa na nyama inayosadikiwa kuwa ni ya tembo yenye uzito wa kilo 50 ambayo ilikuwa imebebwa tayari kupelekwa Songea mjini.
Alisema kuwa Kasmila pia alikamatwa akiwa na silaha mbili za moto ya kwanza ni aina ya Shotgun Grina yenye namba za usajili 461570 na silaha ya pili ni aina ya liffle yenye namba 0019 ambayo ilikuwa na risasi mbili.
Silaha hiyo inasadikiwa ndiyo alikuwa ikitumika kuua tembo, ambapo kwa hivi sasa kumekuwepo na matukio mengi ya kuuawa wanyama hao.
Alisema askari wa jeshi la polisi kwa kushirikiana na kikosi cha kuzuia ujangili Kanda ya Kusini wanaendesha msako mkali wenye lengo la kutaka kuwabaini wawindaji haramu waliokithiri kwenye mbuga ya wanyama ya Selous.
H a t a h i v y o K a m a d a Nsimeki, alisema kuwa Kasimil ameshakamatwa na anaendela kuhojiwa na kwamba upelelezi wa tukio hilo ukikamilika atafikishwa mahakamani

No comments:

Post a Comment