- WABUNGE WAMKINGIA KIFUA
SIKU moja baada ya Kituo
cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kueleza kusudio lao la kumshtaki Waziri
Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kwa madai ya kuvunja katiba ya nchi Ibara ya 13 (1),
wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni mjini Dodoma, Juni 19 mwaka
huu, sakata hilo sasa limezidi kuchukua sura mpya.
Hali hiyo inatokana na Mbunge wa Tabora Mjini, Bw. Ismail Aden Rage
(CCM) kudai kuwa, hakubaliani na hauoni uhalali wowote wa LHRC kumfikisha
mahakamani Bw. Pinda ambaye analindwa na Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya
Bunge namba tatu ya mwaka 1988 pamoja na Katiba ya nchi Ibara ya 100.
Akizungumza na Majira
Dar es Salaam jana, Bw. Rage alisema Mbunge yeyote hawezi kushtakiwa
mahakamani anapotekeleza wajibu wake ndani ya Bunge hivyo kituo hicho kinapaswa
kuwaacha wabunge na viongozi wa Serikali wafanye kazi zao bila vitisho.
Alisema, kabla
kituo hicho hakijafikia uamuzi huo, kinapaswa kupitia Sheria ya Haki, Kinga na
Madaraka ya Bunge namba tatu pamoja na Katiba ya nchi Ibara ya 100 ili
kujiridhisha kama kuna uhalali wa kumfungulia mashtaka Bw. Pinda.
“Kama LHRC
wamekerwa na matamshi ya Waziri Mkuu aliyoyatoa bungeni mjini Dodoma kwa niaba
ya Serikali, waende kulalamika kwa Spika wa Bunge si kumfungilia mashtaka kwa
kigezo cha kuangalia haki.
“Tusiangalie haki peke yake bila
wajibu, suala hili linakuzwa kwa shinikizo la kisiasa jambo ambalo halipaswi
kushabikiwa hata kidogo, mtu yeyote ambaye atakataa kutii amri halali, polisi
anaruhusiwa kutumia nguvu ya ziada,” alisema.
Bw. Rage alikwenda mbali zaidi na
kuongeza kuwa, yupo tayari kumsaidia Bw. Pinda akishirikiana na wabunge wenzake
wa CCM ambao wanamuunga mkono kwa kuhakikisha kama Waziri Mkuu atafikishwa
mahakamani, watasimamisha wanasheria makini wa kumtetea na kushinda.
“Kama leo hii tutaruhusu LHRC
imfungulie mashtaka Waziri Mkuu bila sababu za msingi mbali ya kulinda sheria
za nchi, upo uwezekano mkubwa wa wabunge wengine kufanyiwa kitendo kama
hicho...mbunge anapozungumza ndani ya Bunge haruhusiwi kushtakiwa kwa kauli
yake,” alisema Bw. Rage.
Aliongeza kuwa, Jeshi la Polisi nchini
lina kaulimbiu inayosema ‘Utii wa Sheria bila Shuruti’, hivyo watu wote
wanaokataa kutii amri halali wanatambua madhara yanayoweza kutokana na
ukiukwaji huo hivyo alichosema Bw. Pinda ni sahihi.
Akizungumza na waandishi wa habari
juzi, Mkurugenzi wa Uboreshaji na Utetezi kutoka LHRC, Bw. Harold Sungusia,
alisema wanakamilisha taratibu za kufungua mashtaka dhidi ya Bw. Pinda katika
Makahama Kuu.
Alisema Bw. Pinda amevunja katiba ya
nchi kwa kusema kuwa, “Ukifanya fujo na umeambiwa usifanye hiki na wewe ukaamua
kukahidi utapigwa tu, maana hakuna namna nyingine...ehee wote tukubaliane kuwa
nchi inaongozwa kwa misingi ya kisheria sasa kama weweukijifa nyajeur
iutapigwatu.
“Na miminase mam uwapige tukwasab abu
hakunana mnanyin ginemaa natumechoka ”,alise maBw. PindaambapoB w.Sungus
iaaliong eza kuwa ,kau li hiyoni kin yumech aK atiba , S heriazanchi namising
iya HakizaBinad am u.
Bw. Sungusia aliongeza kuwa, kituo hicho kilitegemea Bw.
Pinda angefuta kauli yake ambayo aliitoa katika Bunge la Bajeti lililoisha hivi
karibuni lakini hadi sasa hajafanya hivyo.
Kauli ya Pinda imekua na tija kubwa na ilitolewa kwa wakati wake. Wahuni walifyata! Tulipata nafasi ya kupumua! Iacheni serikali ifanye kazi yake ya kulinda raia kutokana na wahuni. Hao wenzetu waache waseme na kutishia kwa vile ndio ajira yao. Wasipofanya hivyo hawana kazi! Lakini wajue nao wanalindwa na kufaidika kutokana na kauli ya waziri mkuu.
ReplyDelete