31 July 2013

SAKATA DAWA ZA KULEVYA NCHINI

  • MAWAZIRI WAMO
  • WACHUNGAJI WANAITUMIA IKULU KUVUSHA


Na Rashid Mkwinda, Mbeya
 SIKU chache baada ya kijana mmoja wa Kitanzania aliyeko gerezani mjini Hong kong nchini China kuandika waraka akielezea sababu za yeye kujihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya na kuwataja baadhi ya vigogo wa dawa hizo nchini, hali imeendelea kuwa tete baada ya mawaziri wawili kuhusishwa katika biashara hiyo.

Mbali na mawaziri hao wawili (majina tunayo) pia wabunge watatu wa viti maalumu wakiwemo wachungaji wakubwa hapa nchini (majina yanahifadhiwa) nao wamedaiwa kuhusika na biashara hiyo huku wakitumia vitambulisho vya Ikulu ili kufanikisha kazi zao.
Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki katika mhadhara wa kongamano la kidini kwenye Ukumbi wa Kanisa la TAG Uyole jijini Mbeya na wanafunzi wawili ambao walikuwa wanafanya biashara hiyo (majina tunayo) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na St. Gasper cha Morogoro wakati wakisalimisha kilo tano za heroine.
Dawa ambazo walikuwa wakizisambaza jijini Mbeya ambapo baada ya kuguswa na neno la Mungu waliamua kuzisalimisha mbele ya kanisa hilo.
Wa k i z u n g u m z a k a t i k a kongamano hilo vijana hao walisema kuwa, kwa muda mrefu wamekuwa wakitumiwa kusafirisha dawa za kulevya katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi hali ambayo imekuwa ikiwanufaisha vigogo wa dawa za kulevya ilhali wao wakiishia magerezani.
Sababu za kusalimisha
“Tumeamua kujisalimisha mbele ya Mungu, tumeamua kuzisalimisha dawa hizi mbele ya Mungu, tunatubu kwa dhambi tulizozifanya, tumeiangamiza jamii isiyo na hatia...tunatubu mbele ya Mungu,” alisema mmoja wa vijana hao (jina tunalo) huku akibubujikwa na machozi mbele ya umati wa waumini waliohudhuria kongamano hilo.
Akitoa ushuhuda mbele ya ya waumini waliokuwa katika kongamano hilo ambalo liliongozwa na wachungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kipentekoste, William Mwamalanga na Mchungaji Daud Mwalonde wa Kanisa la TAG Calvary Tempo, mmoja wa vijana hao alisema kuwa amekuwa katika biashara hiyo kwa zaidi ya miaka sita ambapo amesafiri katika nchi mbalimbali za Asia kama vile Afghanistan, India na nchi kadhaa za Bara la Afrika.
Alisema kuwa, huko walichukua na kuzisafirisha dawa hizo na kupata ujira mdogo ambao haukuweza kukidhi mahitaji yao ya kila siku hivyo wameamua kujisalimisha kwa kuwa wanaamini kuwa maisha ya hapa duniani wameshindwa kufanikiwa na mbele ya Mungu wataingia motoni.
Alisema kuwa, yeye pamoja na mwenzake walikuwa wamesimama Uyole wakitokea jijini Dar es Salaam kwa mtu mmoja waliyemtambulisha (jina linahifadhiwa) ambako ndiko hufanya kituo kabla ya kusambaza mzigo huo katika vituo vya mipaka ya Tunduma hasa Wilaya ya Momba na Kasumulu Kyela ambako mzigo husafirisha nje ya nchi.
Mawaziri wamo  
   Alibainisha kuwa, katika biashara hiyo wamo mawaziri wawili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano nchini akiwemo mmoja anayehusishwa na ugombea urais mwaka 2015 na Naibu Waziri katika moja ya Wizara za serikali ya Jamhuri ya Muungano (majina tunayo). Aidha, kijana huyo alisema kuwa mtandao huu wa dawa za kulevya pia unawahusisha baadhi ya wachungaji maarufu nchini (majina tunayo) ambao alidai wanapokuwa katika biashara hiyo hutumia vitambulisho vya Ikulu na kufanikiwa kupenya maeneo mbalimbali nyeti ili kufanikiwa kupitisha dawa za kulevya.Akiendelea kutoa, ushuhuda katika kongamano hilo ambalo lililenga kuombea amani na utulivu wa nchi, alisema kuwa baadhi ya klabu za kusaidia watoto wagonjwa wanaosafirishwa kwa ajili ya matibabu nje ya nchi pia zinahusishwa katika usafirishaji wa dawa za kulevya.
   Aliwataja  baadhi ya wabunge watatu wa viti maalumu na wabunge wastaafu kutoka chama tawala (majina yanahifadhiwa) ambao humiliki maduka makubwa katika majiji ya Dar es Salaam, Mbeya, Tanga, Arusha, Dodoma, Mwanza na baadhi ya nchi za Kiarabu ambapo walidaiwa huwa wanawatumia baadhi ya wasanii na waimbaji wa nyimbo za Bongo fleva zikiwemo za Injili katika usambazaji wa dawa hizo kwa mashabiki.Mara baada ya kusalimisha dawa hizo aina ya heroine, Mchungaji Mwamalanga aliamuru dawa hizo zichomwe moto na kutumbukizwa katika shimo la choo ambapo vijana hao baadaye viongozi wa dini waliwahifadhi.
   Akizungumza sababu za kuzichoma moto na kuzitunbukiza katika shimo la choo badala ya kuzisalimisha kwa Tume Inayohusika na Uratibu wa Dawa za Kulevya nchini ili kuzihakiki, Mchungaji Mwamalanga alisema kuwa waliamua kufanya hivyo baada ya kuona kuwa dawa hizo zimekuwa zikirejea mikononi mwa watumiaji baada ya kukamatwa.Alisema kuwa, kulingana na taarifa walizonazo ni kwamba mara kadhaa watuhumiwa wa dawa za kulevya hukamatwa lakini dawa hizo zimekuwa zikirudi kwa watumiaji na kufanya jitihada za mapambano dhidi ya dawa za kulevya kugonga mwamba.
Akizungumza na Majira Dar es Salaam jana, Bw. Rage alisema Mbunge yeyote hawezi kushtakiwa mahakamani anapotekeleza wajibu wake ndani ya Bunge hivyo kituo hicho kinapaswa kuwaacha wabunge na viongozi wa Serikali wafanye kazi zao bila vitisho.
Alisema, kabla kituo hicho hakijafikia uamuzi huo, kinapaswa kupitia Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge namba tatu pamoja na Katiba ya nchi Ibara ya 100 ili kujiridhisha kama kuna uhalali wa kumfungulia mashtaka Bw. Pinda.
“Kama LHRC wamekerwa na matamshi ya Waziri Mkuu aliyoyatoa bungeni mjini Dodoma kwa niaba ya Serikali, waende kulalamika kwa Spika wa Bunge si kumfungilia mashtaka kwa kigezo cha kuangalia haki.
“Tusiangalie haki peke yake bila wajibu, suala hili linakuzwa kwa shinikizo la kisiasa jambo ambalo halipaswi kushabikiwa hata kidogo, mtu yeyote ambaye atakataa kutii amri halali, polisi anaruhusiwa kutumia nguvu ya ziada,” alisema.
Bw. Rage alikwenda mbali zaidi na kuongeza kuwa, yupo tayari kumsaidia Bw. Pinda akishirikiana na wabunge wenzake wa CCM ambao wanamuunga mkono kwa kuhakikisha kama Waziri Mkuu atafikishwa mahakamani, watasimamisha wanasheria makini wa kumtetea na kushinda.
“Kama leo hii tutaruhusu LHRC imfungulie mashtaka Waziri Mkuu bila sababu za msingi mbali ya kulinda sheria za nchi, upo uwezekano mkubwa wa wabunge wengine kufanyiwa kitendo kama hicho...mbunge anapozungumza ndani ya Bunge haruhusiwi kushtakiwa kwa kauli yake,” alisema Bw. Rage.
Aliongeza kuwa, Jeshi la Polisi nchini lina kaulimbiu inayosema ‘Utii wa Sheria bila Shuruti’, hivyo watu wote wanaokataa kutii amri halali wanatambua madhara yanayoweza kutokana na ukiukwaji huo hivyo alichosema Bw. Pinda ni sahihi.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Mkurugenzi wa Uboreshaji na Utetezi kutoka LHRC, Bw. Harold Sungusia, alisema wanakamilisha taratibu za kufungua mashtaka dhidi ya Bw. Pinda katika Makahama Kuu.
Alisema Bw. Pinda amevunja katiba ya nchi kwa kusema kuwa, “Ukifanya fujo na umeambiwa usifanye hiki na wewe ukaamua kukahidi utapigwa tu, maana hakuna namna nyingine...ehee wote tukubaliane kuwa nchi inaongozwa kwa misingi ya kisheria sasa kama weweukijifa nyajeur iutapigwatu.
“Na miminase mam uwapige tukwasab abu hakunana mnanyin ginemaa natumechoka ”,alise maBw. PindaambapoB w.Sungus iaaliong eza kuwa ,kau li hiyoni kin yumech aK atiba , S heriazanchi namising iya HakizaBinad am u.
Bw. Sungusia aliongeza kuwa, kituo hicho kilitegemea Bw. Pinda angefuta kauli yake ambayo aliitoa katika Bunge la Bajeti lililoisha hivi karibuni lakini hadi sasa hajafanya hivyo.
 

10 comments:

  1. Hawa wachungaji walitakiwa waweke ushahidi alau robo gramu ya heroin ili ithibitike.Pili hili swala sio la kanisa yani kutubu peke yake.ingetakiwa kushirikisha vyombo vya dola kwa sababu kutajwa kwa vigogo tene wa serikali na bunge vinaidhalilisha Serikali na CCM na wote waliotajwa.Pia vijana hao wanaweza kuuawa na watuhumiwa na sidhani kuwa hao wachungaji wanaweza kufanya kazi za ulinzui.MUNGU yeye anasamehe hana tatizo lakini watu na heshma zao je?

    ReplyDelete
  2. Kuhusu Waziri mkuu kuburutwa mahakamani mimi naona si sawa.Huyu ni kiongozi wetu wa serikali-na lazima serikali itishe waovu ili wasiendelee kutenda maovu.Kumbukeni mchozi aliotoa hapo nyuma aliposema kuwa wanaoua albino nao wasakwe.Kazi ya vyombo vya dola ni kutisha waovu.Kuna mazoea kuwa hata mtoto mhuni shuleni asichapwe,aachwe tu amgharimu mzazi pesa na achelewe,wapeane mimba,wavute bangi-huo sio utaratibu.Nasema lazima tutii maelekezo halali ya viongozi.Na MUNGU IBARIKI TANZANIA.SHALOM SHALOM.

    ReplyDelete
  3. Sioni umuhimu wa kuiweka hii habari wtk unajua kabisa hutawweza kutaja hayo majina ya waliotajwa wala kuiweka wazi hiyo barua!! Umesomea wapi, andika habari ambayo umeifanyia uchunguzi wa kina na vithibitisho vya kutosha then iweke,Naona Mwandishi umekuwa muooooga!!

    ReplyDelete
  4. watu wengine waongo tu kama unawajua siuwataje unaogopaa nini?

    ReplyDelete
    Replies
    1. haya yote yanajulikana si mageni nashanga yanatoka leo. wewe mwandishi huisaidii jamii yetu. unachotakiwa ni kutaja hao wahusika ukombozi hauji kwa kuogopa

      Delete
    2. maoni yangu, hili swala la madawa ya kulevya ni uzushi, niambie uthibitisho ukihitajika utapatikanaje wakati wameshaichoma moto? naona hata huyo mchungaji kachemsha jazba akaharibu kithibiti.

      Delete
  5. MUANDISHI HAKUITENDEA NCHI HAKI - KUFICHA MAJINA YA WAUZA UNGA. NI VYEMA WAKATAJWA KWA UWAZI.

    ReplyDelete
  6. Umairi wa mwandishi ni wa kichinvi na uduvi kwa maana kama majina ya wahusika yametajwa hadharani katika mkutano wa kidini na majina ya wachungaji yanajulikana hivyo hakuna umuhimu wa kuficha majina. Inawezekana mwandishi ni mzushi au hajui ni anafanya hata lugha iliyotumika ni nyepesi ikionyesha fasaha hana na vile vile ni mlinzi wa viongozi wa ccm, mafisadi na wauza ungo. Hongera kwa kupata kazi ktk hili gazeti vingenevyo usingepata ajira

    ReplyDelete
  7. jamani wauza unga wanajulikana mmeng'ang'ania viongozi wa ccm mawaziri eeeeeeeeeee jamani kuchafua huko kuchafua gani tenaaaaaaaa.jmani huyo slaa anae jitia mchungaji na kiongozi wa siasa ana yake .zito ana yake.jamani afanyase kosa ni lake mwenyewe asihusishwe na chama chake hayo ni makosaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  8. Tatizo la kuwa na waandishi wanaopewa ruzuku na vyama vya siasa ndio mwanzo wa ugomvi ruanda. Moja ya vilivyosababisha mauaji ya halaiki Rwanda 1994 ni gazeti moja lililoitwa kangura na lingine la kanguka. waandishi kama Rahidi wanaweza kutuletea matatizo makubwa hapa nchini tusipokwa makini nao. Hapa chama kinahusika vipi kwenye dawa za kulevya. Na hawa wachungaji nao ni wana ccm. Lkn LHRC nao wasitumike kama chama cha siasa. Kama wangeweza wangeishitaki wizara ya elimu kwa kusababisha vifo vya wanafunzi wa Form four waliojinyonga baada ya kufeli mtihani. lakini kwa kuwa viongozi wahusika ni wachaga na mkurugenzi wa LHRC ni mchaga wa chama flani hawezi kuwaaibisha ndugu zake ila anataka pinda wa katavi ndiye aaibishwe kitu ambacho kwanza LHRC hawawezi hata kidogo.
    Kuna mambo mengi yanafanyika lkn LHRC hawafuatilii ila ya viongozi wa kutoka kanda tofauti na ya Mkurugenzi wanafuatilia. Ni ushenzi kutetea haki za binadamu kwa maana ya ukanda na ukabila kwa ajili ya kutetea chama flani. kwani chadema hawana makosa. Mbona Freeman Mbowe alimpa mimba mbunge wa viti maalum chadema baada ya nkumhonga ubunge na LHRC hawajafuatilia. hii ni rushwa ya ngono, na sisi tuliopo ndani ya chadema tunalijua hili.

    ReplyDelete