31 July 2013

KANUNI ZA BUNGE:PINDA HAKUKOSEA

  • WABUNGE WAMKINGIA KIFUA
 Na Eckland Mwaffisi


SIKU moja baada ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kueleza kusudio lao la kumshtaki Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kwa madai ya kuvunja katiba ya nchi Ibara ya 13 (1), wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni mjini Dodoma, Juni 19 mwaka huu, sakata hilo sasa limezidi kuchukua sura mpya.

Hali hiyo inatokana na Mbunge wa Tabora Mjini, Bw. Ismail Aden Rage (CCM) kudai kuwa, hakubaliani na hauoni uhalali wowote wa LHRC kumfikisha mahakamani Bw. Pinda ambaye analindwa na Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge namba tatu ya mwaka 1988 pamoja na Katiba ya nchi Ibara ya 100.
 Akizungumza na Majira Dar es Salaam jana, Bw. Rage alisema Mbunge yeyote hawezi kushtakiwa mahakamani anapotekeleza wajibu wake ndani ya Bunge hivyo kituo hicho kinapaswa kuwaacha wabunge na viongozi wa Serikali wafanye kazi zao bila vitisho.
Alisema, kabla kituo hicho hakijafikia uamuzi huo, kinapaswa kupitia Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge namba tatu pamoja na Katiba ya nchi Ibara ya 100 ili kujiridhisha kama kuna uhalali wa kumfungulia mashtaka Bw. Pinda.
“Kama LHRC wamekerwa na matamshi ya Waziri Mkuu aliyoyatoa bungeni mjini Dodoma kwa niaba ya Serikali, waende kulalamika kwa Spika wa Bunge si kumfungilia mashtaka kwa kigezo cha kuangalia haki.
“Tusiangalie haki peke yake bila wajibu, suala hili linakuzwa kwa shinikizo la kisiasa jambo ambalo halipaswi kushabikiwa hata kidogo, mtu yeyote ambaye atakataa kutii amri halali, polisi anaruhusiwa kutumia nguvu ya ziada,” alisema.
Bw. Rage alikwenda mbali zaidi na kuongeza kuwa, yupo tayari kumsaidia Bw. Pinda akishirikiana na wabunge wenzake wa CCM ambao wanamuunga mkono kwa kuhakikisha kama Waziri Mkuu atafikishwa mahakamani, watasimamisha wanasheria makini wa kumtetea na kushinda.
“Kama leo hii tutaruhusu LHRC imfungulie mashtaka Waziri Mkuu bila sababu za msingi mbali ya kulinda sheria za nchi, upo uwezekano mkubwa wa wabunge wengine kufanyiwa kitendo kama hicho...mbunge anapozungumza ndani ya Bunge haruhusiwi kushtakiwa kwa kauli yake,” alisema Bw. Rage.
Aliongeza kuwa, Jeshi la Polisi nchini lina kaulimbiu inayosema ‘Utii wa Sheria bila Shuruti’, hivyo watu wote wanaokataa kutii amri halali wanatambua madhara yanayoweza kutokana na ukiukwaji huo hivyo alichosema Bw. Pinda ni sahihi.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Mkurugenzi wa Uboreshaji na Utetezi kutoka LHRC, Bw. Harold Sungusia, alisema wanakamilisha taratibu za kufungua mashtaka dhidi ya Bw. Pinda katika Makahama Kuu.
Alisema Bw. Pinda amevunja katiba ya nchi kwa kusema kuwa, “Ukifanya fujo na umeambiwa usifanye hiki na wewe ukaamua kukahidi utapigwa tu, maana hakuna namna nyingine...ehee wote tukubaliane kuwa nchi inaongozwa kwa misingi ya kisheria sasa kama weweukijifa nyajeur iutapigwatu.
“Na miminase mam uwapige tukwasab abu hakunana mnanyin ginemaa natumechoka ”,alise maBw. PindaambapoB w.Sungus iaaliong eza kuwa ,kau li hiyoni kin yumech aK atiba , S heriazanchi namising iya HakizaBinad am u.
Bw. Sungusia aliongeza kuwa, kituo hicho kilitegemea Bw. Pinda angefuta kauli yake ambayo aliitoa katika Bunge la Bajeti lililoisha hivi karibuni lakini hadi sasa hajafanya hivyo.
 

1 comment:

  1. Kauli ya Pinda imekua na tija kubwa na ilitolewa kwa wakati wake. Wahuni walifyata! Tulipata nafasi ya kupumua! Iacheni serikali ifanye kazi yake ya kulinda raia kutokana na wahuni. Hao wenzetu waache waseme na kutishia kwa vile ndio ajira yao. Wasipofanya hivyo hawana kazi! Lakini wajue nao wanalindwa na kufaidika kutokana na kauli ya waziri mkuu.

    ReplyDelete