N a Yu s u p h Mu s s a ,
Lushoto
BAADHI ya walimu
wilayani Lushoto wamefananisha elimu nchini na maghorofa mabovu yanayojengwa
jijini Dar es Salaam, kwani inazidi kushuka kutokana na mfumo mbovu wa mitaala
na uingizaji holela wa vitabu vya kufundishia na kujifunzia shuleni.
Wakizungumza juzi kwenye mkutano wa wakuu wa shule za msingi na sekondari
katika Halmashauri ya Bumbuli, uliondaliwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa Bumbuli,Bw. January Makamba, walisema
Serikali ishirikishe wadau kwenye
utungaji wa mitaala. "Kama mchakato wa
Katiba Mpya unavyoshirikisha wadau, vivyo hivyo utungaji au uanzishwaji wa mitaala
m i p y a i w a s h i r i k i s h e wadau ili kupata mitaala itakayokubalika
vinginevyo elimu itaendelea kushuka. "Itazidi kuporomoka kwa vile haina
misingi mizuri. Hivi inakuwaje mtoto wa darasa la kwanza anakwenda shuleni na
madaftari tisa, turudishe utaratibu wa 'K' tatu yaani masomo ya Kusoma,
Kuandika na Kuhesabu" alisema Mratibu wa Elimu Kata ya Soni, Bi. Luth
Msagati. Mratibu wa Elimu Kata ya Milingano alisema mitaala iliyopo kwa sasa
hata walimu hawaijui, hivyo ni vigumu mwalimu kumfundisha mwanafunzi akaelewa,
huku akisema changamoto nyingine ni kuwaingiza sekondari wanafunzi waliopata
alama 70.Mkuu wa Shule ya Sekondari Kwa Mongo,Bw. Anthony Kihiyo, alisema kwa
Serikali kuruhusu wanafunzi wa shule za kata
na zile za Mtakatifu kufanya mtihani mmoja ni sawa na kumpambanisha Francis
Cheka na mgonjwa aliyelazwa Hospitali ya Muhimbili. "Wanafunzi wa shule za
kata kufanya mtihani mmoja na wale wa shule binafsi ni kuwaonea. Hata mabondia
uzito wao unapimwa na unatakiwa ulingane ndipo wapigane," alisema,Bw.
Kihiyo. Kwa upande wake Bw. Makamba alisema pamoja na Waziri Mkuu Mizengo Pinda
kuunda tume ya kuchunguza kiini cha matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka
jana, bado walengwa ambao ni walimu hawajapewa nafasi ya kutoa maoni yao juu ya
suala hilo .
No comments:
Post a Comment