SERIKALI mkoani Tabora,
kupitia kwa Ofisa madini mkazi wa mkoa huo, BW. Elias Mutelani, imeagiza
kufungwa kwa machimbo ya dhahabu yaliyopo katika kijiji cha Kapumpa, kata ya
Kitunda, wilayani Sikonge, mkoani humo na wachimbaji wote wameamriwa kuondoka
mara moja katika eneo hilo ili kuweka utaratibu na usimamizi mpya wa uchimbaji
madini hayo. Ak i t o a t a a r i f a y a kufungwa kwa machimbo hayo, Bw.
Mutelani alisema kuwa Serikali ya mkoa imeagiza kufungwa mara moja kwa shughuli
zote za
uchimbaji katika eneo hilo ili kuweka utaratibu mpya utakaowezesha
shughuli za uchimbaji zifanyike kwa utaratibu unaoeleweka vizuri zaidi.
Akizungumzia agizo la kufungwa machimbo hayo afisa mtendaji wa kata ya Kitunda,
Bw. Julius Ndege, alisema ni kweli machimbo yamefungwa rasmi, lengo likiwa ni
kuweka utaratibu mzuri wa namna gani uchimbaji wa madini hayo uweze kufanyika
na kubainisha kuwa agizo hilo limetolewa na uongozi wa Serikali ya mkoa.
Kufungwa kwa machimbo hayo kumeleta kizaazaa na hali ya sintofahamu kwa
wachimbaji zaidi ya 4,000 waliokuwepo katika eneo hilo, baada ya Mei 3, mwaka
huu kukuta mabango la kuwataka waondoke. Wa k i z u n g u m z a n a waandishi
wa habari mkoani hapa, Mwenyekiti wa wachimbaji hao, George Mtasha, alisema
baada ya kupewa amri ya kuondoka, baadhi yao walipotea njia na wengine zaidi ya
2,000 walilazimika kutembea kwa miguu hadi Sikonge mjini umbali wa zaidi ya
kilomita kutokana na kukosa nauli. Bw. Mtasha alibainisha kuwa askari
walipofika katika machimbo hayo, walianza kuwafukuza huku wakichoma mahema
ambayo walikuwa wakitumia kulala. Katibu wa kamati ya wachimbaji hao, Bw.
Ibrahim Tundu, alisema kuwa katika eneo hilo dhahabu ipo ya kutosha sana na
hadi sasa kuna askari polisi ambao wamebakisha wachimbaji wachache.
No comments:
Post a Comment