15 May 2013

'Viroba vikipigwa marufuku tutahamia kunywa gongo'

Na Reuben Kagaruki


 BAADHI ya wakazi wa jijini Dar es Salaam, wamepinga vikali hoja iliyoanzia bungeni wiki iliyopita kwamba kinywaji cha Konyagi aina ya Kiroba kipigwe marufuku nchini na wameonya kuwa uamuzi huo ukifikiwa watahamia kunywa gongo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao, walisema endapo serikali itachukua uamuzi wa kupiga marufuku kinywaji hicho, itakuwa haijawatendea haki walalahoi, kwani ndiyo wanywaji wakubwa.
Mkazi wa Ukonga Mombasa, wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam, alisema
Serikali isipige marufuku kinywaji hicho kwani ndiyo mkombozi wao.
"Tukikubali hilo tutakuwa kama Zambia ambayo ilizuia viroba, lakini nchi nzima imejaa viroba vya Malawi, Zaire na Burundi, lazima tuiadhibu serikali ikose kodi kote kote, bia hatunywi, viroba vya nje tutakunywa, pamoja na gongo,"alisema.
Alisema haiingii akilini kukihusisha kinywaji hicho na ajali za magari. Alifafanua kwamba hata kabla ya viroba kuingia sokoni ajali zilikuwepo nyingi.
"Sisi tuna imani na viroba kwa vile vina ubora wa uhakika tofauti na pombe ya gongo ambayo inapikwa bila kupimwa ubora hivyo ni hatari kwa usalama wa afya zetu," alisema Mwiruka.
Kwa upande wake, Bw. John Kamugisha, mkazi wa Chanika, alisema, wanaotaka viroba vipigwe marufuku hawawatendei haki wananchi wa kawaida ambao kwa asilimia kubwa hawana uwezo wa kununua bia ambazo bei yake ni kubwa.
"Siku hizi wananchi wengi wamehamia kwenye makambi ya jeshi ambapo bia zinauzwa bei nafuu na wengine wanakunywa viroba kwa sababu vinauzwa bei nzuri, wananchi hao wakibugudhiwa watahamia kwenye gongo," alisema.
Wakazi wengi waliohojiwa walisema kuwa jambo hilo inawezekana ikawa njama za wafanyabiashara kutoka nchi jirani ambao hawaitakii mema Tanzania kwa kuwa pombe hiyo kuwepo kwake pia kunakuza pato la Taifa.
Naye, Bw. Mwesigwa Joas alisema hapendi viroba ni pombe ya wanyonge hivyo aliwataka wabunge kuthamini kinywaji hicho na bidhaa inayozalishwa na wazawa.
"Huwezi ukahusisha viroba na pikipiki, kwani nchi hii ina pikipiki nyingi na watu milioni 43, uhusiano wake uko wapi, kwanza hata leseni hamuwapi?" alisema.
Watu walitoa maoni hayo baada ya kuona kinywaji chao cha kiroba kinapigwa vita kupitia vyombo vya habari.
Inadaiwa kuwa kampeni inayoendeshwa na kampuni zenye uhusiano na kampuni kubwa ya pombe duniani yasiyopenda, nchi za Afrika zizalishe pombe zake, bali ziendelee kununua kutoka Ireland, Kenya na Uingereza.
Akizungumza na waandishi wa habari mwanzoni mwa wiki hii, Mkurungenzi Mkuu wa Konyagi, Bw. David Mgwassa, alisema kuwa kwa kipindi kirefu kumekuwa na mchezo mchafu wa kuharibiana jina kampuni yake sokoni kwa kutumia baadhi ya vyombo vya habari vya hapa nc

1 comment:

  1. Wabunge acheni mizengwe kukurupukia ajenda zisizo mashiko. Wacha watu wanywe waburudike. pato la taifa likue. Kama suala ni ajali au kutokuwajibika kwa wanywaji basi vyombo vyetu vya usalama vinahusika katika kutoa elimu na kukazia sheria zilizopo. Kumbuka si kila mtamzania ni dereva na kikundi kidogo cha watu kisipelekee kutoa maamuzi yatakayokandamiza wengi. Mmenunuliwa au? KIROBA HOYEEEEEEE!

    ReplyDelete