KIONGOZI wa muda mr e f u s e r i k a l i n i n a m t a
a l a m u a n a y e t a m b u l i k a kitaifa na kimataifa katika masuala ya
uwekezaji, Bw. Emmanuel Ole Naiko, ameteuliwa kuwa balozi wa heshima wa
Botswana nchini Tanzania, ambapo makao yake yatakuwa jijini Dar es Salaam.
Akitangazwa na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, jijini Dar es Salaam, juzi Bw.
Naiko, aliishukuru serikali ya Botswana chini ya uongozi wa Rais Ian Khama na
Waziri wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa, Bw. Phandu T.C Skelemani, kwa
kumteua kuwa
mwakilishi wao hapa Tanzania.
"Naamini ni Mwenyezi Mungu
aliyewaongoza na
mimi napenda
kuwahakikishia kwamba sitawaangusha. Nitawawakilisha kwa ukamilifu wote ulio
ndani ya uwezo wangu," alisema Bw. Naiko.
Bw. Naiko alimshukuru Waziri Membe kwa
kukubali kumkabidhi dhamana hiyo kubwa. "Wewe ni ndugu na rafiki yangu wa
muda mrefu naamini uliona ni vyema ukanipa heshima hii wewe mwenyewe,"
alisema.
Alisema Botswana ina vivutio vingi vya
uwekezaji kama Tanzania na kuwa Watanzania na jumuiya y a Af r i k a Ma s h a r
i k i wanakaribishwa kuwekeza katika nchi hiyo.
"Nadhani wakati umefika Botswana nayo
kupata wawekezaji kutoka Tanzania kama wao walivyowekeza Mlimani City,"
alisema.
Nc h i y a B o t swa n a imepakana na nchi
za Afrika ya Kusini, Zimbabwe, Namibia na Zambia. Ina ukubwa wa sq km 58,2000,
wakazi milioni 2.
Ni nchi iliyo na amani na utulivu toka
uhuru na ina kiwango kidogo sana cha rushwa barani Afrika.
Nchi hiyo imedhamiria kuongoza katika
sekta za fedha, madini hasa uranium, shaba na usafirishaji wa almasi na copper
na pia kuendeleza uwekezaji katika sekta ya utalii kwani Botswana ina mbuga
nyingi za wanyama na hasa Vistoria Falls ambayo iko mpakani na Zimbabwe na
Zambia katika mji wa Kasane.
"Watanzania walioko huko wameanzisha
chama chao na mimi nilikutana nao nilipokuwa TIC," alisema.
Kodi ya mapato katika nchi hiyo ni
asilimia 22; VAT ni asilimia 12 na pia kuna msamaha wa kodi kwa wawekezaji ni
kati ya miaka mitano mpaka 10.
No comments:
Post a Comment