*Wasema Hoja zake zimezingatia sheria si porojo za siasa
*Wakerwa na wasomi wanafunzi kubeza maoni yake
Na Mwandishi Wetu
SIKU moja baada ya waliojiita wanafunzi wa kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, Profesa Mwesiga Baregu kupinga
maoni ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Mark Bomani kuhusu malipo ya Kampuni ya Dowans, wanasheria kadhaa jijini Dar es Salaam wamemuunga mkono na kusisitiza kuwa maoni hayo ni sahihi kwani yamezingatia mtazamo wa kisheria.
Wakizungumza na gazeti hili kwa sharti la majina yao kutoandikwa, wanasheria hao kwa nyakati tofauti jana walisema kwa mujibu wa sheria, kauli ya Jaji Bomani katika mahojiano maalum na gazeti hili juzi ni sahihi na kwamba alitumia uzoefu wake kisheria na huo ndio ukweli kuhusu malipo hayo.“Ukiangalia ukweli wa kisheria hoja zote alizozungumza
Jaji Bomani kuhusu uhalali wa malipo ya Dowans na madhara yanayoweza kuikumba nchi endapo itakataa kulipa ni sahihi. Mimi kama mwanasheria mzoefu namuunga mkono, hawa wanaojaribu kupinga hoja zake
naamini bado wachanga kisheria.
Malipo ya Dowans kwa vigezo alivyotoa Jaji Bomani hayakwepeki japo waliohusika katika mkataba lazima wachukuliwe hatua,”alisisitiza mwanasheria mmoja wa kujitegemea jijini Dar es Salaam. Alisisitiza kuwa iwapo hukumu ya kesi dhidi ya Shirika
la Umeme Tanzania (TANESCO) katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi ya Migogoro ya Kibiashara (ICC) ilitolewa na watu wenye sifa, Tanzania haiwezi kukwepa kuilipa Dowans kwa kutumia mabavu.
Alishauri Watanzania kuacha ushabiki na kupoteza muda katika suala hilo badala yake watafute ufumbuzi wa tatizo la umeme kwani umeme si suala la
kisiasa bali linagusa uchumi na
maendeleo ya nchi.
“Kumshambulia Jaji Bomani si sahihi, hoja alizotoa ni za kitaalamu zenye mtazamo wa kisheria. Maoni ya Jaji Bomani yanapaswa kuheshimiwa kwani kama mtaalamu na mkongwe wa fani ya sheria ana haki kutoa maoni yake kwa kuzingatia uzoefu wake, huyu ni mwanasheria anazungumza kwa kuitazama sheria si porojo za kisiasa,” alisema wakili mwingine jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa sheria ni utaalamu si ushabiki.Aliwashambulia waliojiita wanafunzi wa sheria mwaka wa tatu kwa kauli zao dhidi ya Jaji Bomani na kueleza kuwa wamekosa hoja kwani walipaswa kujibu kwa misingi ya hoja alizotoa Jaji Bomani badala ya kutoa majibu yasiyo na mantiki
hatua inayoshusha hadhi na usomi
wao.
Naye Jaji Bomani akizungumza na gazeti hili jana, alieleza kusikitishwa na watu wanaomshambulia katika maoni yake kwa kutanguliza ushabiki bila kuzingatia ukweli na mantiki
ya kisheria.
“Mimi nilitoa maoni yangu kama mwanasheria mzoefu, Jaji na Mwanasheria Mkuu mstaafu wa Serikali kwa kuzingatia sheria za nchi na za kimataifa na kwa maslahi ya heshima ya nchi katika jumuiya ya kimataifa. Sikutoa maoni hayo kisiasa kama wengi wanavyofanya. Inasikitisha kuwa tumefikia mahali hata mtu hawezi kutoa maoni yake bila kupachikwa maneno ya ovyo ovyo. Mimi ni mwanasheria ninayeheshimika haijawahi na haitatokea kurubuniwa na mtu yeyote. Inasikitisha sana,” alisema Jaji Bomani.Hivi karibuni katika mahojiano yake na gazeti hili, Jaji Bomani alisema kisheria malipo ya Dowans hayakwepeki kinyume na hapo taifa litaingia kwenye matatizo makubwa zaidi.Akaeleza kuwa ni vigumu Mahakama Kuu kutengua hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC Court) kama hakukuwa na kasoro zozote katika utoaji hukumu hiyo.
“Kwa kesi za usuluhishi kama hii hukumu hii inaweza kutenguliwa tu kama hao wapatanishi hawakuwa na sifa za kuwa wapatanishi kitu ambacho hapa hakiwezi kutumiwa kwa kuwa katika suala hili, hawa walikubaliwa na pande zote,” alikaririwa akisema Jaji Bomani na kuongeza;“Hukumu hii inaweza kutenguliwa tu kama ikidhihirika kwamba wamepewa rushwa kwa kutoa hukumu ya namna hiyo. Vinginevyo Mahakama Kuu haijihusishi na kuingilia kesi yenyewe.” “Mimi kwa upande wangu kama nilivyokwisha kusema siku za nyuma jambo hili liishe ili mitambo hiyo itumike hapa nchini kuzalisha umeme tuondokane na hali ya mgawo na upungufu wa umeme na hilo ndilo jambo muhimu kwa uchumi wa nchi.Jaji Bomani aliyetumikia nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kati ya mwaka 1965- 1976 akirithi wadhifa huo kutoka kwa mwingereza Bw. Roland Brown,alisisitiza kuwa kwa mujibu wa sheria, haoni sababu za kukwepa kulipa fidia hiyo na kushauri kuwa kilichopo sasa ni kuzungumza na hao wanaodai ili kufikia muafaka wa namna ya malipo hayo.Alishauri kuwa kukataa kulipa kimabavu si sahihi hivyo serikali inapaswa kutafakari kwa makini jambo hilo kabla ya kufikia maamuzi.
Alionya kwamba endapo serikali itatumia mabavu kugoma kulipa na Dowans ikasajili hukumu ya kesi hiyo nje ya Tanzania, kisheria kampuni hiyo inaweza kupewa uwezo kukamata mali za serikali huko ziliko.Novemba 15 mwaka jana,Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara ilipitisha hukumu dhidi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuilipa Dowans fidia ya sh. bilioni 94 kutokana na kuvunja mkataba.
Hao ndio wasomi wetu. Wote wamegeuka kuwa wanasiasa sijui Tanzania tunaelekea wapi. Cha kusikitisha hata viongozi wa dini wanaonekana kuegemea upande mmoja ama mwingine. Hii ni hatari. Wasomi mnaojifanya kuongea kama wasomi fanyeni kama Mwesiga Baregu, yeye tunamjua sasa kuwa ni mwanasiasa amshachagua. Tunaomba nanyi wengine mchague. Tuliambiwa Richmond ilikuwa kampuni hewa haikuwa na uwezo wala mitambo ya kuzalisha umeme, sasa hii mitambo iliyorithishwa Dowans ilitoka wapi, na ilifikaje nchini? Na kama Richmond ilikuwa kampuni hewa mbona tanesco wameambiwa wailipe fidia? Ina maana ICC imeona hii kampuni ni halali? Pia nimesikia hii kampuni imekuwa sued huko Marekani na Dowans, ina maana hii kampuni ipo? Halafu kama hiyo haitoshi, wasomi na wanasiasa wanatwambia kuwa Dowans ni ya Rostam, Lowassa na JK. I am confused. Kama Dowans ingekuwaya ya JK tanesco walitoa wapi ubavu wa kukatisha mkataba? Jamani uchaguzi umeisha JK ni rais, naomba mtu mwenye ukweli wa maswali haya atuelezee vizuri bila kutoa majibu ya kisiasa.
ReplyDeletewatanzania wengine ni wajinga nadiriki kuwaita wajinga samahani! huwezi ukajiita umebobea halafu ukaundermine politics au siasa hawa inawezekana ndio wanaoamini siasa maana yake sihasa ni wapumbavu kila discipline ina maana yake bila siasa hakuna sheria uchumi, elimu, utamaduni.maisha nisiasa kwa hiyo usilaumu wanasiasa jilaumu wewe usiyepevuka kiakili panukeni enyi wanasheria uchwara an eye can not see itself Bomani wenu kakosea hata mimi sijui sheria kama mtaalamu lakini kuna mambo hayaishui kuwa na utashi akina bomani na wanasheria wengine ndio mumeharibu nhi hii mafisadi wakubwa ndio maana yesu hakuitaji wansheria waongo watetezi wa wahalifu sheria gani hiyo yakubesha mizigo nchi lengo sio utaalaamu au ubobezi kila mtu amebobea ktk nyanja fulani tufike mahali kila mtu aheshimu mawazo ya taaluma nyingine sio kumlaumu mtu kwa uanasiasa,uprofesa,udini,ujinga, uelewa wake suluhu ni kwa nini tulipe deni kesi ambayo haijasikilizwa ! nani shahidi wetu kwanini hukumu ndio ijulikane kwa wote ! pesa ya kulipa inatoka wapi? nani anayo?hivi tumelogwa!kunawatu wanalala njaa vijijni haya ni matatizo ya viongozi wasiojua hali halisi ya maisha ya wtz wamezaliwa hawana shida ambao hawajawahi kubebwa kwenye baiskeli hata waje shinyanga wajionee kila kitu baiskeli kuna vijiji vingine hata tarehe ya leo hawajui
ReplyDeleteELINEEMA JONATHAN MOSI,
ReplyDeleteDUU HII KALI SASA MBONA TUNACHANGANYA HIVI JAMANI. OK NI KWEL KISHERIA HAYAKWEPEKI HAYO MALIPO SASA KAMA RICHMOND ILIKUWA KAMPUNI HEWA KWA MTU ANAYETAFAKARI VIZURI MWENYE AKILI ZENYE UTASHI KWANINI SERIKALI IKAAMUA KURISISHA MKATABA KWA HUYU FATAKI DOWANS BILA YA KUVUNJA MKATABA NA RICHMOND ILI HATA WAKITUDANGANYA WATUDANGANYE VIZURI. MMMH UTAFIKIRI TANZANIA HAKUNA WASOMI NACHELEA KUSEMA HIVI, TUNARUDISHWA KARNE YA 9,SASA HUU NI UFATAKI WA AINA YAKE, BWANAEE JAJI BOMAN BADO SIJAKUELEWA KABISAAA,BADO WAZEEKA VIBAYA
Ebana kweli mkubwa uliyeeleza hapo juu ushahidi upo tosha kwamba wamiliki wa hiyo dowans na richmond ni watanzania hebu jiulize kwnini upande wa utetezi wa serikali ya tz hawakwenda kwenye kesi na ningependa kumkumbusha mwenzangu hapo juu kwamba suala la kuvunja mkataba na dowans lilifanywa makusudi ili wapate hizo fedha kawani gharama za fidia ni kubwa kuliko mapato wanayopata kila siku na waliona washaanza kuandamwa kwa hiyo walifanya makusudi sula ni kuendelea kupinga suala hilo na kuishinikiza serikali kukata rufaa mbona kesi ya kupinga mgombea binafsi walikata rufaa kwanini hili wasikate rufaa ina maana wanafaidka na haya malipo tena wanataka kulipa hata kabla ya kampuni kusajiliwa na vip kampun ifanye kazi bila kusajiliwa mnae shinikiza kulipa fedha hizi hawatahusika na mateso ya ulipaji kwani unaweza kukuta wanalipiwa na serikali bili zao tuamke jamani sio porojo zisizi za msingi kwenye mambo ya msingi.
ReplyDeleteHuu ni wizi wakalamu tume ya bunge ilidhihirisha hakuna kampuni kama hio na watanzania tulishuhudia Watanzania wenzangu hapa tumeibiwa tunaendelea kuibiwa kutokana na mioyo ya viongozi waselikari yetu walivo na roho ya kuijilimbikizia mali ni ufisadi tu huu wasomi na wanasiasa wote hawamhurumii mtanzania anaehangaika kijijini wote tamaa kwenye pesa.
ReplyDeleteHivi hawa wanasheria wanaotetea Dowans walipwe mbona wanachelea kutajwa majina yao, kila mara utasikia " Hakupenda jina lake litajwe" kuna kitu gani hapo1 Mbona Prof. Baregu amaetoa mawazo yake na jina lake; Hao wanasheria wanaogopa nini ? Hii taluma ya sheria siyo hesabu ambapo 3+2=5 hakuna jibi jingine, lakini kwenye sheria hukumu au uamuzi wa mwanasheria moja unaweza kutenguliwa na mwanasheria mwingine!! kwanini leo hii wao ndiyo wanaona kuwa wanajibu la mwarobaini wa Dowans. Hii ndiyo sababu Yesu wakuwapenda kabisa Mafarisayo(wanapindisha sheria na kuwaibia wajane)
ReplyDeleteMimi naitwa Mlay, niko Marekani kwa sasa nawasikitikia sana Ndugu zangu wa TZ kwa kuwa inaonekana kumba ninafuu wakulima walio vijijini kuliko wasomi tuliyonayo hasa wale wa zamani. Hawa kina Bomabi walikuwepo wakati hao mafisadi wanaingia mkataba na Richmond na hatimaye Dowans hawakuzungumza kitu, lakini imefika wakati wa tingo nono la ugali na asali linaingia midomoni mwao ndo wanakuwa wa kwanza kujifanya ETI wanazijua hata sheria za kimataifa. MBONA HAWAKUISHAURI SERIKALI ISIIINGIE MIKATABA MIBOVU LAKINI SASA WANATAKA TULIPE FEDHA ZA MIKATABA HIYO MIBOVU????. Je, hawa wanaojiita wanasheria wazoefu mbona kuna sheria nyingi zimepitwa na wakati lakni hawataki kuishauri serikali kuzifanyia mabadiliko lakini wako tayari kuzunguzia sheria kwenye mambo yenye maslahi binafsi tu??
ReplyDeleteDU KAZI IPO NAO HAO WANASHERIA MBONA WANAJICHANGANYA. kAMA WANACHOSEMA NI SAHIHI NA HAWAJARUBUNIWA KWA NINI WAFICHE MAJINA YAO.AU WAMESHAKULA KITU KIDOGO DOWANS?
ReplyDeleteWatanzania tuache kupiga kelele za bure maana tumeshazoea kudanganywa danganywa baadae kushau hivi hatukumbuki tulivyofanywa na kufanywa wajinga kukubali Ndugu Balaji wa Benki ya Tanzania aliekimbilia America amefariki wakati hakuna aliyethibitisha kifo hicho kwa kuona maiti yake na hakuna mtu aliyeruhusiwa kwenda kwenye maziko yake hata wale waliopo umarekani. Wapi uliwahi kushuhudia kifo kama hicho kutokea tumeganganyanywa Balali yupo umarekani anakula pesa za watanzania, hili nalo pia Dowans watalipwa tutalalamika tutasahau.
ReplyDeleteTatizo kubwa katika nchi yetu ni woga wa kusema ukweli.Tunazunguka zunguka kulinda maslahi binafsi. Wanaotetea uovu pengine wanandugu zao katika sakata la ufisadi na si vinginevyo.
ReplyDeleteNingekuwa serikali, bora kukataa kulipa halafu mali zetu zikamatwe huko kwingine kuliko kukubali kirahisi rahisi tu kama mnyama wa machinjioni, bora hizo mali zikamatwe huko ziliko and tuanze upya, jamani tumezidi ukondoo, tuandame kama Tunisia kieleweke ili tuitoe hii CCM ya tangu Uhuru, tuandamane, CCM itoke, CCM mnaboa, sana tena sana.
ReplyDeleteKiama kwa wale wote waliodhania waTZ wataendelea kulala kimefika! - ni kweli kama wadau wengine walivyosema hapo juu kwamba waTZ ni waoga, lakini vuguvugu lililopo kipindi hiki sio sawa na vipindi vingine...mahali waTZ tumefikishwa ni mahali pabaya na hatutakubali KUENDELEA KUONEWA!
ReplyDeleteUanasheria wa Bomani umeshazeeka, kwahiyo wanaomuunga na wenyewe akili zao zimezekea pia.
ReplyDeleteJamani kumekuwa na mazoea ya wanasiasa na wenyenacho wanapotajwa juu ya kashifa zozote wanakibilia kwenye magazeti kutangaza nia ya kuwapeleka mahakamani watu wanao dai wanawasingizia na kuwachafulia jina.Kwa safari hii inafurahisha kwamba hao watu wanaotajwa kwenye mambo yote ya ufisadi wanaogopa kutoa kauli zao kwenye magazeti kuonyesha nia zao za kuwashitaki wanaowasingizia. Mimi nadhani ingekuwa vyema wakatoa kauli zao ili wajisafishe ikibidi waende mahakamani ili sisi tusiojua kitu tupate kuelewa mbichi na mbivu. Kukaa kwao kimya wakati sio mazoea yao ni kuona sasa karibu wanakamtwa ugoni. Ombwe lililopo ni kuwa inaonekana wanadhurumu hata washirika wao,kitendo ambacho ni cha kawaida kwa wezi wengi. Ndiyo maana wanaogopa kwenda mahakamani kwa sababu waliowadhurumu wanavyo vyanzo vingi vya habarizao. Kwa hiyo inabidi wakae kimya.
ReplyDeleteNa nyie wasomi wa maswala ya kisiasa,kiuchumi,kiutawala na kisheria hasa mlio madarakani,hivi hamuoni kama mnafanya makosa kwa watanzania. Haiwezekani kuwepo kelele nyingi hasa kwa miaka ya 1995 hadi sasa,na nyie msijirekebishe. Acheni kuwaibia watanzania kwa kutumia mbinu zenu. Kumbukeni wakati mnasoma mlikuwa na wenzenu walio soma masomo kama ya kwenu na wanaona madudu mnayoyafanya. Hawakupata nafasi kama mlizonazo kwa kutojuana na waliowaajiri ama walifauru vizuri kuliko ninyi. Wekeni masilahi ya wananchi na mheshimu maadiri ya kazi zenu. Matokeo yake mmeleta karaha na marumbano nchi nzima mmekuga gumuzo.
Nawaombeni Watanzania, tuliangalie hili suala kitaaluma zaidi. Mwacheni Jaji Bomani atowe maoni yale kitaalam anavyotazama yeye. Mimi kama awali namuunga mkono, kwa kila hoja aliyoitoa. Na ningependa tumheshimu kwa sababu kwetu wengine Jaji Bomani ni kama Babu yetu. Amemzaa baba au mama zetu. (Ni mtu mzima) anastahili heshima yake, kukaa Marekani, au kupata digrii hii yangu moja hainifanyi nijione kuwa nina ufahamu mpana katika taaluma hii zaidi yake! Kama tuna hoja tumpinge kwa hoja na si kumvunjia heshima yake kama tulivyofanya kwa Kadinali Pengo!
ReplyDeleteMimi nilivyoshauri hapo awali, kama yupo mwanasheria aliyebobea nje ya Jaji Bomani basi na awe mstari wa mbele kwenda kupinga mahakamani madai hayo!
Mtuoneshe kifungu hicho, mkisimamie na zaidi mtuwezesha kupinga malipo haya ili tupate unafuu! Watanzania tupo nyuma yenu hata kwa kupitisha harambee ya kufungua kesi hiyo Mahakama Kuu tukutane pale Mlimani City au Uwanja wa Jangwani tupo tayari! Isipokuwa sharti ni moja tu ukishindwa nguvu ya Wanzania wote tuliokuamini itakuangukia na ukubali hivyo!!! Chonde mtanzania wewe jitokeze tukuwezeshe utusaidie tunaamini utaweza tuachane na taaluma waliyoiita baaadhi yetu kuwa iliyopitwa na wakati ya kina Jaji Bomani!
Ninyi mnaoona mbali hebu jitokezeni tuisaidie nchi yetu! Soote tutakuwa nyuma yenu ilitujuwe kama ni kulipa tulipe kabla interest rate haijatuathiri sana!
Maana mpaka sasa ndoa hii na DOWANS gharama zake hazikwepeki!
Cha msigni hapa tujadili kulipa kabla hatujaathika na riba yake ila katika mchakato wa kulipa, wale waliotufikisha hapa tunawafanya nini?!
Ni lazima tuibane serikali itutajie watanzania walipo nyuma ya DOWANS na RICHMOND ambao kimsingi ndiyo waliotufikisha hapa, tutafute wanasheria wetu tuwalipe na kuwawezesha kuwashtaki wote ili wachukuliwe hatua stahili kwa mujibu washeria!
Lazima tufike hapo, kama Jk alivyosema tusiwaache majambazi wakitamba, nasi tuseme tusiwaache Mafisadi waliotufikisha hapa wakitamba! Lazima nao tuwatendee haki yao!
Carwin
HAHAHAHAHAHAAAAAAAAAAAAA
ReplyDeleteKWERI HUYU JAMAA BOMANI SI NDIO YULE SIR?
HANA JIPYA HUYO HIVI HAJUI MABILIONI YOTE HAYO TUAWEZA HATA KUWEKA MAJI KWA WANANCHI WETU WAKAACHA KUFA KWA KIPINDUPINDU? NDIO MAANA YEYE ANAONA RAHA KUITWA SIR AU ANJIONA NA YEYEY MZUNGU? AKUMBUKE FIKRA SAHIHI HUJA KWA LUGHA SAHIHI U SIR WAKO HUKO HUKO KWENU ULAYA NDIO MAANA MKIUGUA MNAKIMBILIA ULAYA KWA VILE PESA MWAPELEKA HUKO BADALA KUJENGA HAPA KWENU
Unajua kinachoendelea sasa hivi nchini ni kuhalalisha madai ya Dowans kwenye macho ya watanzania. Juhudi nyingi zinazofanyika sasa hivi ni kuwafanya watanzania wakubali kuwa deni wanalo, ni halali na hawawezi kulikimbia. Mimi ninachoshangaa ni kwa nini miaka michache iliyopita nchi nyingi zilikataa kuhalalisha na kulipa madeni yao ya nje yaliyosababishwa kimabavu na World Bank, IMF na nchi nyingine za Magharibi? Nyerere alikuwa mmoja wa viongozi waliosema deni hilo la taifa halilipiki kwa sababu ni la kiukandamizi. Na alilishikia njuga mpaka wazungu wakakubali kubadilisha mwelekeo wao. Tokea hapo tukaona nchi yetu inachukuliwa kama nchi inayotakiwa kusamehewa madeni yake. Sasa leo tunaona tofauti ya mdai na mdaiwa. Mdai si tena nchi za magharibi au world bank au IMF. Mdai ni kampuni binafsi aliyesajiliwa kwenye kainchi kengine masikini. Kampuni hiyo pia inashangaza kwani ina management na shareholders kutoka nchi nyingine na wanaidai nchi nyingine. Sasa kama Tanzania ilikuwa tayari kutokuhalalisha na kulipa madeni yake kutoka IMF, WORLD BANK na nchi nyingine za magharibi kwenye miaka ya 90, inakuwaje leo Tanzania ishindwe kukataa kulipa deni la kampuni binafsi isiyeeleweka inakotoka, inapokwenda, ilipokuwa na hata inavyofanya kazi na imewekezaje kwenye nchi inakotoka? Kwani Dowans ni organisation yenye nguvi kama IMF, World Bank na Mataifa mengine ya Magharibi?
ReplyDeleteUsiri huu wa kutoelewa uhusiano wa mdai na mdaiwa ndiyo tatizo kubwa na Jaji Bomani anatakiwa kuelezea swala hili si tu kisheria bali hata kisiasa. Vijana wakimpinga ni kwa sababu wanachanganyikiwa kutokana na kutoelewa haki za mdai na mdaiwa.
Boniface Mhella (PHD).
THE PUMBAVUZ,NYIE WASOMI FEKI MNAONUNULIWA MITIHANI NA BABA ZENU NA KUNUNUA VYETI,NA HATA HAO WANAOJITIA WAKO MAREKANI PENGINE WANAOSHA VYOO NA KUSAFISHA MAVI YA WAZUNGU HUKO. TATIZO LIKO WAPI? MAHAKAMA KUU IKO WAZI NENDENI MKAOKOE PESA ZA NCHI KWA KUZUIA SI MNASEMA INAWEZEKANA? MAANA KILA MTU AKITOA MAONI YAKE MNASEMA KAGAIWA---HOVYOOOO AKILI ZENU ZIKO MATAKONI HAMZIONI MPAKA MUENDE KWENYE KIOO,MNAPIGA KELELE ZA NINI ? NENDENI MAHAKAMANI MKAZUIE? WENGINE WANAWEKA PICHA WAKIWA WAMEVAA TAI SIJUI WANAFIKIRI HOJA ZAO NDIO ZITAONEKANA ZA MAANA. WISDOM IS BETTER THAN YOUR EDUCATION WHICH YOU CANT UTILIZE IT
ReplyDeleteMzee Bomani, anauelewa mzuri tu, ila katekwa na Mafisadi ili kuiangamiza Tanzania. Nilikuwa Nategemea kwa uanasheria wa Bomani angeanza kuelezea ni namna gani Richmond Hewa iligeuka kuwa ya maana ikanunuliwa na DOWANS. Pili Mzee Boman angekuwa na uelewa wa kutosha basi angeshauri Nchi iendeshwe kisheria siyo kisiasa kama inavyokwenda sasa. Wezi wa EPA sheria Haikufanya Kazi, Richmond sheria Haikufanya kazi, Haki za watanzania sheria haifanyi kazi, Hivyo Bwana Bomani unaona sheria kwenye kulipa Dowans TU? Bwana Boman lazima awe na uelewa kuwa kwa sasa Tanzania SIASA in Nguvu Kuliko shiria, Hivyo mawazo yako yanaweza kuwa mazuri ila siyo kwa Tanzania Ya sasa. Kama MZEE BOMANI ANASOMA COMENTS ZA WATU BASI ANGESIMAMA TENA NA KUTUELEZA KISHERIA NI NAMNA GANI RICHMOND ILIBADIKA KUTOKA KUWA FAKE MPAKA KUWA SAFI NA KUUNGANA NA DOWANS. ZAIDI YA HAPO NAKOSA AMANI KABISA KUWA HATA BOMANI AMBAYE NI UZAO WA NYERERE NA ANAINGIA KWENYE KASHIFA HIZI ZA UFISIDI? INAKATISHA TAMAA.
ReplyDeletewatanzania sasa tufanye kama tunisia tuiondoa ccm kwa maandamano kupinga udhalimu wao.. ufisadi, umeme,shida za walimu,ajira hakuna,madini yananufaisha waliomadrakani, watanzania tusidanganywe na kuwa hii ni nchi ya amani! amani wapi hali wengine wanafaidi nchi, matajiri wachache, wengi wetu ni hohe hahe, tunadanganywa na hii ni nchi ya amani!!!YALIFANYIKA TUNISIA HATA SISI TUNAWEZA!!!
ReplyDeleteWATANZANIA TUBADILIKE, ILIKUWA ZAMANI ENZI ZA UJINGA KWAMBA SIASA NI MCHEZO MCHAFU WA KUDANGANYA WATU NA KUWANYANYASA, SIASA NDO DIRA YA MWELEKEO WA NCHI KIMAENDELEO, UTAKAPO SIMAMA JUKWAANI NA UTAKAYO YASEMA UNAPASWA KUYATEKELEZA KAMA HUTAWEZA HUFAI KUWA MWANASIASA KIONGOZI WA KARNE HII, NDO UTAWALA WETU WA SASA UNALAZIMISHA MAMBO, SUALA LA RICHMOND KAMA LINGESHUGULIKIWA KIKAMILIFU BUNGENI LEO KUSINGEKUWA NA MALIPO HAYO YA DOWANS, LAKINI KWASABABU LILIZIMWA KWA MASILAHI NDO MATOKEO HAYO, WATZ AMKENI MFANYE MABADILIKO YA CHAMA NA VIONGOZI,
ReplyDeleteNYIE WAPUMBAVU MNAAMBIWA MAHAKAMA YA USULUHISHI YA KIMATAIFA IMEONA KUNA KOSA LIMEFANYIKA NI LAZIMA TANESCO WAILIPE DOWANS NA WASIPOLIPWA NCHI ITAKUWA KWENYE MATATIZO MAKUBWA ZAIDI SASA WEWE MJINGA UNAWEKA USHAB IKI WA KISIASA UCHAGUZI UMEKWISHA NA CCM NDIO WATAWALA NENDENI ARUSHA NA MOSHI MKAANDAMANE MUONE FAIDA YAKE KULIKO KUENDELEA KUWADANYANYA WATANZANIA NA WANANCHI WAPENDA AMANI NA MAENDELEO ALA"
ReplyDeleteAnayestahili kuheshimika atahehimika tu hata asipodai kuheshimika.Hata mtoto aliyezaliwa leo ni lazima aheshimike,ni kazi ya mikono ya Mungu Muumbaji.Pia huwezi mlazimisha mtu kumheshimu mwingine,acha alama nzuri ktk maisha yako utaheshimiwa tu ukiboronga basi huna chako.
ReplyDeleteOk nashukuru kwa waliochangia sina jipya na siwezi kufupisha michango yote mizuri iliyochangiwa hapo juu ila nimekunwa na yafuatayo.
1.Kwa nini wananchi tuletewe HUKUMU ya kesi bila kujua kesi ilikuwa inaendeleaje? 2.Kama Richmond ilikuwa kampuni HEWA ilikuwaje ikarithisha biashara zake HEWA kwa DOWANS na serikali ikakubali kufanya hivyo? 3.Kabla ya kurithisha mikataba yake Je,hao DOWANS walikuwa wanafanya nini hapa nchini maana huo URITHI ulifanyika mara moja tu? 4.Mnaoitwa mmebobea na mambo ya SHERIA mbona hamkujitokeza magazetini mkipinga URITHI HEWA? twambieni kama hamkusikilizwa na wahusika.5.Kila kampuni inakuwa na mmiliki, Richmond tunamjua aliyetolewa kama KAFARA japo wapo wengine,Je DOWANS mwenye kampuni hii ni NANI?Mwisho naombeni WTZ kuheshimu watu wa kada zote hata mtoto wa chekechea hata hao wanafunzi wa mwaka wa tatu ikumbukwe kuwa huyu anakuwa msomi zaidi ya mwalimu anayemfundisha chuoni.Tukumbuke mwalimu wako kule Primary yeye na cheti chake yumkini kile cha UPE lakini amezalisha wasomi hata hao Ma-Profs.
Namuomba kwa hiari yake kiongozi wa nchi atamke moja tu ili kama ni kulipa tujue kila MTZ atagawiwa kiasi gani cha DENI kwani MADENI FEKI mangapi tumelipishwa tumezoea na hali hiyo kwani tunasubiri kilio chetu cha umasikini wa kusingiziwa (tumatajiri) umfikie OUR Almight FATHER aliyetupa rasilimali zote hizi BUT wachache ndio wamezikumbatia.
UKIONA KILA SAA NCHI INASOMA VIFUNGU VYA SHERIA UJUE INAKABILIWA NA TATIZO LA UTAPELI NA MAOVU YA KILA JUMLA. NCHI HII SASA HAWAFANYI KAZI KUTWA WANATAFISIRI SHERIA. NA WENGINE WANAKIMBILIA TAALUMA HIYIHIYO. NCHI HII ITAFIKA MAHALA WASOMI NI WENGI HATA KWA ASILI MIA 80 NA MA PHD HUMOHUMO LAKINI SHUHUDIA USOMI WAO DEGREE IN NGO IN HIV COUNSELLING IN HOSPITALITY PH D IN CAUSING CONFLICTS ETC. KENYA INASEMA TZ KILA MTU IKO KWA PHD.JAMANI TUZALISHENI MALI LETS EMBRACE ON TECHNOLOGY AND BUILD THIS COUNTRY. WE ARGUE OUR GOVT TO PLEASE SHOW THE WAY ACHANENI NA HILA ZA KUSOMA VIFUNGU KUTWA ETI HUYU KATOKA COSTA RICA WHAT A DESTINATION KAAMBIWA KUNA TATIZO LA RICHMOND NA UMEME TZ AND IS THE BEST PERSON TO GIVE SOLUTION. OJEMENI.
ReplyDeleteSiamini kama huyu mzee (Bomani) anapalilia Dowans walipwe. Kumbe alikuwa mwanasheria mkuu wa serikali (1965- 1976) wakati Nyerere anataifisha njia kuu za uchumi wakati wa azimio la Arusha!
ReplyDeleteHuyu inaonekana alikuwa bendera fuata upepo akimtii Nyerere tu bila kuamini yale aliyokuwa anayafanya Nyerere. Ndio maana kwa sasa kwa vile Nyerere ameshakufa, amekunjua makucha yake. Uwekezaji usio na tija kwa taifa anaufagilia.
Mbona Nyerere aliamua tu wakati wa azimio la Arusha akataifisha kila kitu. Mbona hakumshauri asitaifishe mali za watu? na mbona waliotaifishiwa mali zao hawakupora mali za Tanzania nje ya nchi?
Sisi ni taifa linalojitegemea, hatubabaishwi na "Corrupt individuals".
Ingekuwa nchi nyingine, tungewanyongelea mbali na kuitaifisha hiyo mitambo yao wanayoitumia kutuibia.
Angekuwepo Sokoine wangeshaingia lupango!
Mungu ibariki Tanzania, tupate viongozi kama Sokoine.
NI HOVYO KWELI WATANZANIA,TATIZO NI VISOMO FEKI WENGI WANATEGEMEA VYETI VYA KUGUSHI NA KUNUNUA MITIHANI,WENYEWE NI LAYMAN KWENYE LAW WANATAFSIRI SHERIA.SHIDA IKO WAPI MAHAKAMA ZIKO WAZI KABISA KWA KUSIKILIZA HOJA ACHENI KUWA MABUSH LAWYER,WAMESEMA MABWANA ZENU WA CHADEMA INAWEZEKANA MAHAKAMANI KUZUIA SASA MNANGOJA NINI? MNAKAA KUTAFSIRI VIFUNGU VYA SHERIA KWA LAYMAN (ASIYEJUA SHERIA) NI SAWA NA KUMPIGIA GITA MBUZI ACHEZE. NENDENI MAHAKAMANI WACHENI KUMJADILI HUYU MZEE KATOA MAONI YAKE KAMA WENGINE WANAVYOTOA.
ReplyDeleteangalia UWOZO sti siasa ina nguvu kuliko sheria,hivi kweli huyu ana akili timamu?
ReplyDeleteHivi kuna nchi ilikataa kulipa madeni ya IMF au zilisema hazina uwezo kwa wakati ule na kuomba tarehe za malipo zisogezwe mbele? nani kakuambia tuliitambia WORLD BANK? tulikula unga wa manjano hata mbwa uliwashinda,babu haambiliki ilibidi aambilike,acheni kudanganya watu,hamna nchi yenye uwezo wa kukataa madeni ya IMF au WORLD BANK,maneno hayo waambieni mbwa wa Slaa ambao wakiambiwa tumbukieni kwenye shimo hayo yanakwenda
ReplyDelete@ Anonymous January 19, 2011 8:51 AM
ReplyDeleteNchi nyingi zilianzisha propaganda ya kufutiwa madeni ya World Bank na IMF kwenye miaka ya 90. Tanzania ni moja wapo. Ni wazi hujui historia ya nchi yako na international finance. Kuna kitu kinaitwa Heavily Indebted Poor Countries (HIPC) kilichoanzishwa kutokana na political pressure na si wanasheria. Tanzania ilikuwa ni moja ya hizo nchi na ilinufaika kusamehewa madeni. Unakataa? Kasome! sinamuda wa kukupa lecture sasa hivi!
Kwa kifupi siasa ndizo zinazopelekea sheria mpya kutungwa. Wanasheria wanafuata tu kilichoandikwa baada ya sheria kutungwa. Hii haimaanishi wanasheria ndo watu wenye akili sana kuliko wanasiasa.
Nenda shule!
bora kuwa mbwa kuliko mbuzi au kenge kama huyo anaye sema mbwa wa slaa acha kutaja mambo ambayo hatujadili hapa. kwani unahitaji kuambiwa na mtu kama huu ni wizi, yaelekea hata mtu akiiba mkeo utamsifu tu, kenge wewe ngoja nimtafute mkeo halafu utukane vizuri
ReplyDeleteJIBU LA YOTE HAYO NI AZIMIO LA ARUSHA. HAKUNA KULIPA.
ReplyDeletekuanzisha propaganda ya kufutiwa madeni sio kukataa kulipa deni,wewe ni muongo,mimi ni msomi ni si wa kununua vyeti au mitihani,acha kudanganya watu,ukatae kulipa pesa ya IMF au World Bank wakati ulikopa? danganya hao takataka zako. bado nasema kulipa au kutolipa hilo si suala la kisiasa ni la kisheria utoe hoja za kisheria usiropoke tu silipi
ReplyDeleteBOOOOOOOOOOO MAAAAAAAAAAAAAAAAN, inakuwaje tena mheshimiwa? Hivi umewahi kusoma andiko la mzee mzima Shaabani Robert "KUSADIKIKA"? Je wamjua mhusika aitwaye "Majivuno"? Je watambua kwamba Majivuno aliamini kuwa kidole chake kimoja tena kile kidogo kina akili kuliko wasadikika wote?
ReplyDeletesasa wewe mzee, ujasiri wa kujiita "jaji mstaafu unayeheshimika", OOh sijui "Mwanasheria uliyebobea" na mengineyo, nauliza ujasiri huo umeupata wapi? Au ni chuo kipi pekee duniani ulichosoma ambacho hakijawahi kusomwa na wa TZ wengine? Au ni daraja gani ambalo ni very unique ambalo wewe ulifaulu na hakuna mtz mwengine aliye/anaye au atakayeweza kulifaulu? NASEMA HIVI AAAAAAAAAAAAAACHA HIZO ZA KUJIKWEZA. Ulichokitoa kinywani mwako nafikiri hukukitafakari na kama ulikitafakari basi una lako jambo. Mheshimiwa, mimi naomba yafuatayo. Jalada la kesi yetu ya dowans huko ICC, case no, chamber ilimosikilizwa, jina la mwanasheria aliyeiwakilisha TZ, tarehe ya hukumu na jina la Jaji mwenzio wa ICC aliyehukumu hayo. Mzee acha kujichafua katika hizo siku za mwisho wa CCM.
NA NYIO WANASHERIA MNAOMUUNGA MKONO MZEE HUYU JITAJENI TUWAJUE, MBONA WENZENU WANAOJIAMINI NA HOJA ZAO MFANO KINA SHIVJI, MVUNGI, BAREGU, SLAA, MTIKILA NA WENGINEO HAWATOI MASHARTI YA KUTOTAJWA MAJINA! NYINYI VIPI? AU NI WANASHERIA MSIOJUA SHERIA NINI? ACHEENI KUUZUBAISHA UMMA, TUMESHAWASTUKIA NYINYI N A HUYO MZEE WENU BOMANI. KWANZA KWA HOJA ZAKE ANAICHAFUA SAFU YA MWALIMU NYERERE.
HIVI WEWE UNAOITA WENZIO MBWA WA SLAA, UNAFIKIRI UNAWEZA KUNISAIDIA KWA KUNIAMBIA WEWE NI KAJIBWA KA NANI?
ReplyDelete@Anonymous January 24, 2011 12:47 AM
ReplyDeleteSidhani kama unaendelea kusoma ila nakukumbusha tu kuwa mtunga sheria wa Tanzania ambaye ni bunge alishaona mkataba wa Tanesco na Richmond ni batili. Sasa DOWANS ameibukaje na kurithi mkataba batili na kuistaki TANESCO na kushinda mabilioni? Inamaanisha basi bunge la Tanzania lilikosea? Je mtunga sheria wa nchi yako anakosea?
kama budget ya Tanzania inapitishwa na bunge, basi hata kama Mahakama Kuu iliruhusu Dowans kulipwa, serikali itabidi tu irudi kwa hao wanasiasa ili ipige danadana za kuwaeleza wabunge itawalipaje Dowans. Na hili ni kama sheria unazozipenda zitaheshimika. Otherwise hata serikali itafanya kazi kisiasa tu.
Kwa kifupi kwenye suala hili huwezi kutoa SIASA hata siku moja. Ila kama Serikali inabariki kulipa, basi wanaweza kuwaburuta tu wananchi na kuwadidimizia umasikini wao kisiasa vile vile.
Kumbuka Tunisia na Misri wanazo pia sheria za kuwatoa viongozi wao, sema wananchi wakichoka wanaweza kutumia njia nyingine nyingi kufanya hivyo. Sheria zinafanya kazi pale watu wanapoona zinamaana ila pale zinapokuwa hazina maana basi elewa kuwa wananchi wanaamua kivyao vyao...
siombei hili litokee TZ
Huo ndo wosia wangu.. Mungu Ibariki Tanzania na watu wake.