JUKWAA la
Katiba nchini, linakusudia kufungua kesi ili kuiomba mahakama isitishe mchakato
wa Katiba Mpya hadi Tume ya Mabadiliko ya Katiba na wadau wakubaliane mambo ya
msingi ndipo mchakato huo uendelee.
Lengo la jukwaa hilo ni kutafuta haki za Watanzania
ili waweze kupata Katiba Mpya waitakayo si vinginevyo.
Mwenyekiti wa jukwaa hilo, Bw. Deus
Kibamba aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na
waandishi wa
habari akidai mchakato huo una kasoro nyingi.
Alisema
hoja walizoamua kuziweka bayana ni mchakato huo ambao unaendelea kushindwa
kurekebisha makosa ya miaka iliyopita katika kuandika Katiba ambayo ni uelewa,
hamasa na ushiriki duni wa wananchi katika mchakato wa Katiba yao.
Aliongeza kuwa, jukwaa hilo limeunda
timu ya mawakili 10 wakiongozwa na Mwanasheria maarufu wa masuala ya Haki za
Binadamu, Dkt. Rugemeleza Nshala.
“Hivi sasa tunaandaa hoja mu h imu z
a k u z iwa k i l i s h a mahakamani ndani ya siku saba zijazo, tunawaomba
Watanzania watuelewe kuwa tunakwenda mahakamani si kuvuruga mchakato huu bali
kuurekebisha.
“Mchakato huu umeshindwa kurekebisha
makosa ya miaka ya nyuma hivyo Katiba itakayopatikana inaweza kuwa mbaya zaidi
kuliko hii tuliyonayo kwa kuligawa Taifa,” alisema.
Alisema sababu nyingine ya kwenda
mahakamani ni juhudi walizozifanya kutaka kuonana na Waziri wa Katiba na Sheria
zaidi ya mara moja ili wazungumze naye kuhusu suala hilo pamoja na kumuona Rais
Jakaya Kikwete kushindikana.
Bw. Kibamba alisema ahadi alizotoa
Rais Kikwete kuhusu mchakato huo hazioneshi dalili ya kutekelezwa kutokana na
tume kusuasua katika utekelezwaji wake.
“Awali tume ilipoteuliwa, wananchi
walikuwa na imani nayo kutokana na watu waliopewa dhamana hiyo...mwanzo
walipewa sh. bilioni nane na mwaka 2012 walitengewa sh. bilioni 34, pesa hizi
wanapewa wao lakini bado wanachelewa kutoa rasimu yake.
“Tunaitaka Serikali ifungue ma s i k
i o kwa k u t e k e l e z a makubaliano waliyoafikiana na vyama vya
siasa...Uchaguzi wa Mabaraza ya Katiba umevurugwa na tume kwa makusudi kwa
kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM),” alisema.
Aliongeza kuwa, chama hicho kilitoa
fomu za kugombea nafasi hiyo wakati kazi hiyo ni ya tume hivyo ni wazi kuwa
mchakato huo ukiendelea, katiba ijayo itakuwa ya CCM si ya Watanzania.
Alisema kwa sasa mchakato huo hauna
uongozi na mwelekeo madhubuti kutokana na wananchi wengi walitoa malalamiko ya
kuvurugwa kwa uchaguzi wa Wajumbe wa Mabaraza ngazi ya Kata na Wilaya,
kutosikilizwa.
Bw. Kibamba alisema baada ya kufungua kesi
hiyo, jukwaa hilo halitazungumzia mchakato huo wakisubiri uamuzi wa mahakama
HIVI KWA NINI KATIBA IWE YA VYAMA VYA SIASA TU TATIZO NI MTU MMOJA AWE MAHAKAMA, NDIYE SPIKA NA NDIO RAIS. HAWA WACHUMIA TUMBO WATATUFIKISHA PABAYA. HONGERA JUKWAA LA KATIBA, TUNATAKA NA SISI VIGANJA NA MASHATI TUSHIRIKISHWE KWANI TUNA MIMILI YA DOLA IWAJIBIKE KWA WATU NA HATUTAKI WANAOJIITA WAISLAMU NA WAKIRISTO KUSHIRIKI KATIKA UUNDAJI WA KATIBA YETU WAUNDE KATIBA ZAO ZA KUCHANGISHA SADAKA NA SIO KATIBA YA WATANZANIA
ReplyDelete