BAADHI ya wakazi wa jijini Dar es Salaam, wamepinga
vikali hoja iliyoanzia bungeni wiki iliyopita kwamba kinywaji cha Konyagi aina
ya Kiroba kipigwe marufuku nchini na wameonya kuwa uamuzi huo ukifikiwa watahamia
kunywa gongo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
wananchi hao, walisema endapo serikali itachukua uamuzi wa kupiga marufuku
kinywaji hicho, itakuwa haijawatendea haki walalahoi, kwani ndiyo wanywaji
wakubwa.
Mkazi wa Ukonga Mombasa, wilayani
Ilala, jijini Dar es Salaam, alisema
Serikali isipige marufuku kinywaji hicho
kwani ndiyo mkombozi wao.
"Tukikubali hilo tutakuwa kama Zambia
ambayo ilizuia viroba, lakini nchi nzima imejaa viroba vya Malawi, Zaire na
Burundi, lazima tuiadhibu serikali ikose kodi kote kote, bia hatunywi, viroba
vya nje tutakunywa, pamoja na gongo,"alisema.
Alisema haiingii akilini kukihusisha
kinywaji hicho na ajali za magari. Alifafanua kwamba hata kabla ya viroba
kuingia sokoni ajali zilikuwepo nyingi.
"Sisi tuna imani na viroba kwa vile
vina ubora wa uhakika tofauti na pombe ya gongo ambayo inapikwa bila kupimwa
ubora hivyo ni hatari kwa usalama wa afya zetu," alisema Mwiruka.
Kwa upande wake, Bw. John Kamugisha, mkazi
wa Chanika, alisema, wanaotaka viroba vipigwe marufuku hawawatendei haki
wananchi wa kawaida ambao kwa asilimia kubwa hawana uwezo wa kununua bia ambazo
bei yake ni kubwa.
"Siku hizi wananchi wengi wamehamia
kwenye makambi ya jeshi ambapo bia zinauzwa bei nafuu na wengine wanakunywa
viroba kwa sababu vinauzwa bei nzuri, wananchi hao wakibugudhiwa watahamia
kwenye gongo," alisema.
Wakazi wengi waliohojiwa walisema kuwa
jambo hilo inawezekana ikawa njama za wafanyabiashara kutoka nchi jirani ambao
hawaitakii mema Tanzania kwa kuwa pombe hiyo kuwepo kwake pia kunakuza pato la
Taifa.
Naye, Bw. Mwesigwa Joas alisema hapendi
viroba ni pombe ya wanyonge hivyo aliwataka wabunge kuthamini kinywaji hicho na
bidhaa inayozalishwa na wazawa.
"Huwezi ukahusisha viroba na
pikipiki, kwani nchi hii ina pikipiki nyingi na watu milioni 43, uhusiano wake
uko wapi, kwanza hata leseni hamuwapi?" alisema.
Watu walitoa maoni hayo baada ya kuona
kinywaji chao cha kiroba kinapigwa vita kupitia vyombo vya habari.
Inadaiwa kuwa kampeni inayoendeshwa na
kampuni zenye uhusiano na kampuni kubwa ya pombe duniani yasiyopenda, nchi za
Afrika zizalishe pombe zake, bali ziendelee kununua kutoka Ireland, Kenya na
Uingereza.
Akizungumza na waandishi wa habari mwanzoni mwa wiki hii, Mkurungenzi
Mkuu wa Konyagi, Bw. David Mgwassa, alisema kuwa kwa kipindi kirefu kumekuwa na
mchezo mchafu wa kuharibiana jina kampuni yake sokoni kwa kutumia baadhi ya
vyombo vya habari vya hapa nc
Wabunge acheni mizengwe kukurupukia ajenda zisizo mashiko. Wacha watu wanywe waburudike. pato la taifa likue. Kama suala ni ajali au kutokuwajibika kwa wanywaji basi vyombo vyetu vya usalama vinahusika katika kutoa elimu na kukazia sheria zilizopo. Kumbuka si kila mtamzania ni dereva na kikundi kidogo cha watu kisipelekee kutoa maamuzi yatakayokandamiza wengi. Mmenunuliwa au? KIROBA HOYEEEEEEE!
ReplyDelete