13 March 2013

Wabunge Chadema kuhojiwa kwa pingu *Polisi wapewa kazi hiyo kuhakikisha wanahojiwa *Ndugai asema kamati wasiyoitambua ipo kisheria *Dkt. Slaa, Lissu wajibu mapigo, wamtega Makinda



Grace Ndossa na Gladness Theonest

OFISI ya Bunge imesema, wabunge ambao watagoma kwenda kuhojiwa katika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Jeshi la Polisi litawapeleka kwa pingu katika kamati hiyo.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana kwa njia ya simu, Naibu Spika wa Bunge, Bw. Job Ndugai, alisema kamati hiyo ipo kisheria na imepewa mamlaka hayo kwa mujibu wa kanuni, sheria ya Bunge.
   
Alisema kamati hiyo ina mamlaka ya kumuita mtu yoyote kupitia polisi au ofisi ya spika kwa kumuandikia barua na kumuhoji.

“Kamati ina mamlaka ya kumuita mtu yoyote na kuhoji, kama akikataa atapelekwa kwa pingu kuhojiwa...hata mimi mwenyewe nikiitwa nisipokwenda nitapelekwa kwa pingu,” alisema.

Aliongeza kuwa, wote wanaoitwa huwezi kujua wanaitiwa nini
hivyo ni muhimu kuzingatia wito wa kamati husika.

Bw. Ndugai alisema, hawezi kubishana na Mbunge wa Hai ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Bw. Freeman Mbowe katika vyombo vya habari kutokana na madai yake kuwa wabunge wa chama chake, wapo tayari kufukuzwa ubunge lakini hawapo tayari kuhojiwa
na kamati hiyo.

Alisema hizo ni siasa tu ambapo kamati hiyo imetoa taarifa kwa
kila mbunge aliyetakiwa kufika za Bunge atekeleze agizo husika
kwa kujitokeza na kusikiliza alichoitiwa.

Wakati Bw. Ndugai akitoa msimamo huo, uongozi wa CHADEMA jana walikutana na waandishi wa habari na kutoa msimamo wao kuwa hakuna mbunge ambaye atakwenda kuhojiwa na kamati hiyo.

Msimamo huo umeungwa mkono na wabunge 32 kutoka CHADEMA na NCCR-Mageuzi wanaopaswa kuhojiwa na kamati hiyo ambayo wameiita batili wakiamini tayari imekwisha muda wake tangu kwenye Kikao cha Bunge la kumi na wapo tayari kufukuzwa ubunge kwa kukataa wito huo.

Akitoa msimamo huo mbele ya waandishi wa habari, Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa, alisema chama hicho kilipokea ujumbe wa Jeshi la Polisi ukiwataka wabunge hao waende kuhojiwa na kamati hiyo.

“Awali wabunge wanne ndio waliotuhumiwa na kuitwa vinara wa vurugu bungeni lakini kupitia taarifa hii ya polisi ambayo ni ya vitisho, imetushangaza kuona wabunge wengine 28 wa CHADEMA na NCCR-Mageuzi, nao wameingizwa katika listi wakati mwanzo hawakuwepo.

“Haifahamiki hawa wabunge waliotajwa majina yao katika taarifa hiyo wanashtakiwa kwa kosa gani...haya ni matumizi mabaya ya sheria, kanuni, katiba na taratibu za Bunge, sisi tunajua kamati zote zilishamaliza muda wake tangu Bunge la 10.

“Tunachojua Kamati Mpya inatarajiwa kupata viongozi wapya machi 14 mwaka huu, hivyo hatupo tayari kuhojiwa na kamati
hii ambayo ni batili na haipo,” alisema Dkt. Slaa.

Aliongeza kuwa, hivi sasa uendeshaji wa Bunge unaofanywa na Spika, Bi. Anne Makinda, unafanyika kibabe kwa kukipendelea Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo chombo hicho kimekuwa cha ukandamizaji badala ya kutetea haki.

“Spika kama hujui kanuni ni bora akajifunze ili ujue kutafsiri, kutumia kanuni, sheria na katiba badala ya kusema mimi ndio niwafundishe watu wangu, wakati nikiwa bungeni sheria zilikuwa zinafuatwa na Spika aliyepita,” alisema Dkt. Slaa.

Mbunge wa Singida Mashariki, Bw. Tundu Lissu, alisema kwa
sasa hakuna kamati yoyote ya Bunge bali zote zilishafungwa hivyo anashangaa kusikia kuna kamati inayopaswa kuwahoji wabunge ambayo wao hawaju imeundwa na nani.

Alisema inashangaza leo hii wabunge wa CHADEMA na NCCR-Mageuzi wanapoitwa vinara wa vurugu bungeni jambo ambalo linaonesha wazi kuwa tayari wamehukumiwa wakati sheria
inakataza kufunguliwa mashtaka kwa kosa lilelile.

“Sikutaka kusema kwa sababu waliniambia nisizungumze lakini naona nisenme, nilipoitwa kwenye kamati hii niliwaambia kuwa siitambui lakini walinijibu wameambia na Spika waendelee...
kumbe hawaongozwi na kanuni bali Spika,” alisema Bw. Lissu.

Alisema yeye anaweza kuhojiwa kama kamati hiyo itavunjwa,
kuwekwa viongozi wengine na kudai wana mpango wa kumuandikia barua Spika kumwambia hawatakwenda kuhojiwa na kamati hiyo.

Akiwa mjini Musoma, mkoani Mara katika mkutano wa hadhara mwishoni mwa wiki, Bw. Mbowe alisema chama hicho kipo tayari wabunge wake kufukuzwa ubunge lakini si wabunge kwenda kuhojiwa na kamati hiyo.

9 comments:

  1. MBONA INASHANGAZA KUONA SPIKA NA WATENDAJI WAKE WANASHINDWA KUTENDA HAKI? HIVI KAMA NI KUFANYA VURUGU BUNGENI JE WABUNGE WA CCM HAWAFANYAGI VURUGU? HIVI WANAPOZOMEA SIYO VURUGU?

    HIVI MAKINDA KUWATAJA WABUNGE WA 4 WA CHADEMA KWAMBA NDIO VINARA WA VURUGU NDIVYO SHERIA INAVYOMRUHUSU? HAJUI KAMA ALIWADHALILISHA NA KUTAKA KUWAAMBIA WANANCHI WALIOWACHAGUA KWAMBA HAWAFAI? CHANZO CHA VURUGU ZOTE NI KITI CHA SPIKA. PIA YEYE NA NAIBU WAKE WANATAKIWA WAHOJIWE KWA KUFANYIA MDHAHA MSWAADA WA JAMES MBATIA KUHUSU ELIMU YA TZ MAANA HAWALITAKII MEMA TAIFA.

    ReplyDelete
  2. NI VEMA ULE MHIMILI WA DOLA BUNGE UHESHIMIWE KIUTARATIBU [DIRECT DEMOCRACY] TULIPASWA WOTE KUWA KWENYE UKUMBI WA BUNGE TUPELEKE KERO ZETU KWA KUWA UKUMBI HAUTOSHI IKABIDI TUTUME WAWAKILISHI[IN DIRECT DEMOCRACY] TUNAWAGHARAMIA KUWASILISHA KERO ZETU WAKATI FULANI TUNAFANYA MAKOSA KUCHAGUA WAHUNI KWENDA KUTUWAKILISHA KWANI TABIA YA UHUNI HAIONEKANI KWA MACHO ILIKUWA HIVI HIVI MBOWE ALIGOMA KURIPOTI POLISI AKIFIKIRI JESHI LA POLISI LITAMWOGOPA AKABEBWA KWENYE HELKOPTA HADI KILIMANJARO UWANJAWA NDEGE NA KUPELEKWA ARUSHA SIJUI ALIFIKIRI ISINGEWEZEKANA HEBU SIASA ZA KITOTO TUZIACHE NI LINI MAVI YA SHINGO YATATUONDOKA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hela ya kurusha helikopta mnayo , wananchi wanakufa vijijini kwa kukosa maji safi na kujifungulia vichakani kwa kukosa dawa na zahanati zisizo na waganga

      Delete
  3. Yangu masikio na macho

    ReplyDelete
  4. Yule Mbunge aliyesimama sikumoja na kumpa maelezo spika eti ufungwe mlango ili wapigane ili waweze kuheshimiana kule ndani, kle ndo kilikuwa kilio au shida ya wananchi wa jimbo lake waliyomtuma akiwakilishe bungeni?. Haikuwa vurugu? au kwa sababu alikuwa wa kutokea chama tawala?

    ReplyDelete

  5. Tatizo uwezo wa kufikiri wa wabunge wa ccm umefikia kikomo maana kazi yao ni kuunga mkono hoja hata kama haina manufaa kwa wananchi. Walianza na zomeazomea wameona haitoshi sasa wameamua kutumia baadhi ya kamati za bunge kuwazorotesha wabunge wa cdm. Hawataweza kwasababu Mungu hawapendi wanafiki(ccm) na watu wanaoshindwa kutumia akili zao hata kama ni ndogo vizuri.

    ReplyDelete
  6. TATIZO LIKO WAPI KAMA IKO SHERIA KWA MUJIBU WA KATIBA YA NCHI YETU KUITWA NA KUHOJIWA POLISI HALAFU UKARUHUSIWA HUKU UKIJUA HUNA KOSA TATIZO LA KUOGOPA KWENDA KUHOJIWA NI NINI KAMA SIO ULIMBUKENI WA KUJUA KWINGI KATIKA UONGOZI NA SIASA NANYI MSIOJUA SHERIA, KANUNI ZA BUNGE MNACHANGIA MADA KAMA VIPOFU KWA KUWA NA ULIMBUKENI WA MAWAZO FINYU SI MNYAMAZE TU, KWANI LAZIMA MSEME CHOCHOTE HUU NI ULIMBUKENE NA UFINYU WA MAWAZO NDIO MAANA MNACHANGIA BILA AKILI YA MNACHOSEMA NI VIZURI MKAELEWA NA SI ULIMBUKENI WA SIASA YA VYAMA VYENU TU.

    ReplyDelete
  7. wewe kwma sio mbuzi basi ng'ombeeee tenana wa maziwa

    ReplyDelete
  8. Uzee wa CCM usitufanye wote wazee. Mzee anapaswa apumzike na heshima zake. That is the law of nature

    ReplyDelete