19 March 2013

Lwakatare apanda kortini kwa ugaidi *Akabiliwa na mashtaka manne, anyimwa dhamana *Mawakili wake wakwama, Machi 20 kurudi tena



Na Grace Ndossa

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, jana limewafikisha kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Wilfred Lwakatare pamoja
na Bw. Ludovick Joseph.


Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo saa 2 asubuni, mbele ya Hakimu Emilius Mchauru ambapo wakili wa Serikali,
Bw. Prudence Rweyongeza, alidai washtakiwa hao wanakabiliwa
na mashtaka manne.

Akisoma mashtaka hayo, Bw. Rweyongeza alidai kuwa, washtakiwa hao walifanya makosa hayo Desemba 28,2012, eneo la King'ong'o, Kimara Stop Over ambao wote walikula njama na kutenda kosa la jinai wakitumia sumu kumdhuru Bw. Dennis Msacky.

Shtaka la pili ni ugaidi ambapo washtakiwa hao wanadaiwa kushirikiana na kuumteka nyara Bw. Msacky kinyume cha
sheria ya ugaidi namba 21 ya mwaka 2002.

Alidai shtaka la tatu ni washtakiwa hao kudaiwa kufanya mkutano wa kupanga ugaidi dhidi ya Bw. Msacky ambao shtaka la nne linamkabili Bw. Lwakatere peke yake ambalo ni kuruhusu
mkutano ufanyike nyumbani kwake ambapo yeye na
Bw. Joseph, walihamasisha kufanya ugaidi.

Washtakiwa hao walikana mashtaka yote ambapo Bw. Rweyongeza alidai kuwa, mashtaka yote manne yako chini ya sheria ya ugaidi sheria namba 21 ya mwaka 2002 hivyo hayana dhamana.

Alidai washtakiwa hao hawatakiwi kujibu chochote, kunyimwa dhamana na Mahakama Kuu ndiyo yenye uwezo wa kuisikiliza
kesi hiyo hivyo aliiomba mahakama hiyo, itoe ruhusu kwa Bw.
Joseph, aendelee kuwa chini ya Jeshi la Polisi kwa mahojiano.

Jopo la mawakili upande wa utetezi likiongozwa na Bw. Tundu Lissu, Bw. Nyaronyo Kicheere, Profesa Abdallah Safari na Bw. Peter Kibatala, walidai mahakama lazima ijiridhishe na mashtaka yaliyotolewa ili iweze kutoa maamuzi.

Bw. Kibatala aliitaka mahakama hiyo isichukulie hoja za upande wakili wa Serikali juu juu bali iende mbali zaidi kabla haijaamua  kumnyima dhamana mshtakiwa wa kwanza Bw. Lwakatare.

Alidai mahakama lazima iangalie kama kweli mashtaka
hayo yanaonesha matendo yanayoendana na ugaidi.

Kwa upande wake, Prof. Safari alidai mahakama lazima iangalia kwa undani suala hilo kwani kesi nyingine ni za kubambikizwa kwani sheria ya ugaidi ni nzito sana.

Aliongeza kuwa, upo uwezekano wa Bw. Lwakatare kubambikiwa mashtaka asiyoyafanya ili aendelee kukaa ndani.

Wakili wa Serikali, Bw. Rweyongeza, aieleza Mahakama kuwa, hakuna mtu aliyebambikiwa kesi na mashtaka hayo yasichukuliwe
kichama kwani mshtakiwa katika kesi hiyo hajatajwa anatoka
chama gani na wao hawajui itikadi yake kisiasa.

Hakimu Mchauru aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 20 mwaka
huu, ambapo watuhumiwa wamerudishwa rumande.

3 comments:

  1. KAMA ALIYETUHUMIWA KUMTEKA ULIMBOKA NA KUMTESA HAJAACHIWA HUYU NAYE HANA TOFAUTI NA SHEHE PONDA ATAISHIA MAHABUSU HUWEZI KUPANGA MIKAKATI YA KUUA WATU UWEKWE RUMANDE NA KISHA UACHIWE UENDELEE KUUA WATU UKIACHIWA UKITOROKA JE KAMA WALIOMUUA KAMANDA WA POLISI LIBERATUS BARLOW MPAKA LEO NI KIZUNGUMKUTI LEO ASHIKWE MUUAJI HALAFU AACHIWE UTAKUWA UZEMBE WA HALI YA JUU AMANI YA TANZANIA NI BORA ASILIMIA MIA MOJA KULIKO WILFRED RWAKATARE ANGEFAHAMU ANA KISUKARI ASINGEFANYA UGAIDI

    ReplyDelete
  2. wachaga na wahaya wanataka nchi hivyo watanzania mtaona mengi, niliwahi kuandika mapema katika maoni yangu usimuamini mwanasiasa yeyote awe wa upinzani au wa chama tawala,wanaweza fanya jambo lolote kwa maslahi ya chama chake au binafsi. sishangai Lwakatare kuwa gaidi,kwa nini leo mnataka gaidi aachiwe laiti angekuwa muislam ndio kapanga hayo msingesema chochote. nchi hii haki ni ya kila mtu,haiwezekani mwanasiasa aachiwe kwa shinikizo kutoka nje ya mfumo ambao upo na wako wanaoutumikia magerezani lakini huyu aachiwe,mkikamata dola mtatenda haki?

    ReplyDelete
  3. Wakili wa serikali yuko sawa kabisa. Kuwa upinzani isiwe ngao ya kutendea maovu na kudai kuwa serikali inawaonea,.,..kila mtu anatakiwa atii sheria za nchi!

    ReplyDelete