20 February 2013

Rais Kibaki kuanza ziara ya siku 2 leo
Na Mwandishi Wetu

RIAS Mwai Kibaki wa Kenya, leo anawasili nchini kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili kutokana na mwaliko wa Rais Jakaya Kikwete, ambaye Septemba 2012, alifanya ziara ya kitaifa nchini humo.

Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Wizara ya Mambo
ya Ndani na Ushirikiano wa Kimataifa, imesema Rais Kibaki anatarajiwa kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere, saa tisa alasiri.

Baada ya kuwasili uwanjani hapo, atapokelewa na mwenyeji wake Rais Kikwete ambapo akiwa nchini, atafanya mazungumzo rasmi Rais kabla ya kushiriki dhifa ya kitaifa ambayo ataandaliwa.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, kesho Rais Kibaki anatarajiwa kukutana na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, kuzindua Barabara iliyopewa jina lake na kutembelea Gereza Kuu la Ukonga kujionea shughuli zinazolenga kuwarekebisha wafungwa kuwa raia wema.

Shughuli hizo ni pamoja na mafunzo ya ufundi yatawawezesha kujitegemea wanapomaliza vifungo vyao ambazo ni ushonaji, useremala na kilimo cha kisasa. Rais Kibaki na ujumbe wake,
ataondoka nchinikesho na kurejea nchini kwake

No comments:

Post a Comment