11 February 2013

Ni kweli tutenganishe siasa na biashara



Aziz Msuya

RAIS Jakaya Kikwete aliwahi kueleza nia yake ya kuhakikisha Wanasiasa ambao ni Wafanyabiashara wana chagua kimojawapo kati ya Biashara na Siasa ili kuondoa mgongano wa kimaslahi unaoweza kujitokeza wakati wa kutekeleza majukumu yao.


Rais Kikwete alieleza nia yake hiyo baada ya kubaini jinsi Viongozi wa Siasa ambao ni wafanyabiashara wanavyoweza kutumia nafasi zao za
uongozi kutekeleza maslahi yao ya kibiashara hata ikiwa ni kwa kuvunja sheria au kutumia nafasi zao za kisiasa kupata upendeleo utakaozinufaisha biashara zao hata ikiwa ni kwa kukwepa au kusamehewa
kodi.

Dhana hii imejitokeza kwa Watumishi na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ambapo  Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. Stephen Mhapa amekiririwa hii karibuni kweye kikao cha Baraza la Madiwani
baada ya Maamu Mwenyekiti Bi Ritha Mlagala kuasilishaarifa ya Kamati ya fedha,Utawa na Mipango ambayo ilionyesha upungufu wa Mapato.

Alisema madiwani na watumishi wa Serikali kwenye maeneo yao wamekuwa wakifanya biashara jambo ambalo linaleta usumbufu katika ukusanyaji wa ushuru vijijini na kuwasihi kutotumia nafasi zao za uongozi vibaya na kuwataka wafuate utaratibu ili wasikwamishe mfumo mzima wa ukusanyaji ushuru na hivyo kupunguza mapato ya Halmashauri.

Kimsingi alichokisema Mh Rais Kikwete na kinachotokea Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ndio hasa kinachotafsiri alichokisema Mh Rais na
kwamba kuna haja sasa Mh Rais akatekeleza kwa vitendo azma yake hiyo ingawa inaonekana utekelezaji huo ni mgumu sana katika mazingira ya
sasa ya kisiasa lakini ukweli unabakia pale pale kwamba mtu mmoja kua mwanasiasa na mfanyabiashara ni tatizo.

Mfanyabiashara yeyote nia yake ni kuhakikisha anatengeneza faida kubwa kwa kutumia mtaji mdogo bila kujali kama njia anazotumia kufanyabiashara ni sahihi au la hata ikiwa ni kwa kutumia cheo chake
cha siasa kukwepa kodi, kupunguziwa kodi au kusamehewa kodi ili mradi tu apate faida kubwa kwenye biashara yake na hapa ndipo tatizo lilipo
kutumia nafasi ya kisiasa kufanya biashara kwa njia haramu.

Kama alivyosema Rais Kikwete ni vema viongozi hawa wakachagua moja Siasa au biashara ili kuondoa mgongano wa kimaslahi na pia kupoteza uadilifu wao wakati wa kuwatumikia wananchi kwa sababu ni ukweli
usiofichika kwamba hakutakua na uwanja sawa wa kufanyia biashara miongoni mwa wafanyabiashara wa kawaida na wafanyabiashara wenye nyadhifa za kisiasa na hapo ndipo matumizi mabaya ya madaraka
yanapoanzia.

Itakua vipi mfanyabiashara wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA atakapokuwa anakadiriwa kodi ya mapato? Hali itakuwaje? Au itakuwa vipi Diwani atakapokuja kudaiwa ushuru wa Nyumba yake ya kulala
wageni na Kampuni ya kukusanya ushuru ambayo imepewa kazi hiyo na Halmashauri na diwani huyo ni mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Biashara,Uchumi na Fedha. Unategemea nini?

Bila Shaka inaonyesha wazi kwamba kunakuwa na mgongano mkubwa wa kimaslahi ambao kumalizwa kwake ni kwa wahusika kuchagua moja ama kufanya Siasa au kufanya biashara ili kuepuka kujipendelea na
shinikizo kwa wakusanyaji wa mapato kama ilivyotokea kwa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Hali inakua mbaya zaidi kwa Wanasiasa wanaofanya biashara za Kimataifa kwa sababu athari ya kukwepa kodi huwa ni kubwa sana kwani biashara hii hua inahusisha mitaji mikubwa na hivyo athari zake kadhalika hua kubwa.

Nionavyo mimi wakati umefika sasa kuhakikisha yanatengenezwa mazingira au Katiba Mpya ijayo ikatamka wazi kwamba ni marufuku mtumishi wa Umma
au Kiongozi wa Siasa kuwa mfanyabiashara kwa sababu wanasababisha mgongano wa kimaslahi lakini pia wanakwamisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali.


No comments:

Post a Comment