18 February 2013

Ndugai ajibu madai ya chadema

Na Benedict Kaguo

NAIBU Spika wa Bunge, Bw. Job Ndugai, amesema kitendo cha viongozi na wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kushirikisha wananchi ili kumshikiniza yeye na
Spika Bi. Anne Makinda, waondoke katika nafasi walizonazo,
kinaonesha wazi jinsi chama hicho kilivyokosa viongozi
makini wenye utashi wa kuongoza nchi.


Kauli ya Bw. Ndudai inatokana na chama hicho, kutoa namba zao
kwa wananchi waliohudhuria mkutano wa CHADEMA uliofanyika
hivi karibuni Temeke Mwisho, wazitumie kuwapigia simu, kutuma
kutuma ujumbe mfupi wa maneno (sms), katika simu zao ili 
kushinikiza wajiuzulu katika nafazi walizonazo bungeni.

Akizungumza na Majira jana, Bw. Ndugai alisema, wabunge wa chama hicho kama walibaini udhaifu wao katika uendeshaji vikao vya Bunge, walitakiwa kuwasilisha hoja ya kutaka wapigiwe kura
ya kuondolewa katika nafasi walizonazo bungeni si vinginevyo.

Alisema kuwa, kitendo cha wabunge wa chama hicho kuanika namba zao hadharani na kuwashawishi wananchi wawapigie
simu usiku ili wasilale ni cha kihuni ambacho hakiwezi
kutimiza azma ya kuwaondoa tatika nafasi walizonazo.

“Kanuni za Bunge zinaeleza wazi kuwa...kama wabunge wanataka viongozi waondoke katika nafasi zao, wapeleke malalamiko yao kwa Katibu wa Bunge ili yaweze kufikishwa kwenye Kamati ya Maadili na baadae Bunge zima kuhojiwa.

“Theluthi mbili ya wabunge ikiridhia kuondoka kwa kupiga kura za siri, viongozi hao watalazimika kuondoka...kama watataka mimi niondoke, waandike mashtaka yangu kwa Spika ili yapelekwe kwenye Kamati ya Maadili na kupelekwa bungeni,” alisema.

Bw. Ndugai aliongoza kuwa, baada ya suala hilo kufikishwa
katika kamati husika, kura za siri zitapigwa na zikitimia theluthi mbili atalazimika basi naondoka.

Alisema kinachofanywa na wabunge wa CHADEMA ni tofauti badala yake wanakwenda kwa wananchi na kutoa namba zao za
simu ili wapigiwe na kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno (sms), kushinikiza waondoke kitu ambacho haiwezekani.

Aliongeza kuwa, hata Waziri Mkuu kama wabunge wanataka aondoke katika nafasi yake, upo utaratibu kama huo ambapo
nusu ya wabunge kama watapiga kura ya siri kuridhia jambo
hilo atalazimika kuondoka.

“Nawahadharisha Watanzania wajihadhali na viongozi pamoja na wabunge wa CHADEMA ambao hawataki kufuata sheria zilizopo, huu ni mfano mdogo unaodhihirisha hawafai kuongoza nchi yetu
kwa sababu hawawezi kusimamia sheria zilizopo.

“Hili ni jambo dogo lakini pamoja na chama hiki kudai kina wanasheria waliobobea, wado wameshindwa kuonesha uwezo
wao badala yake wanakimbilia kwa wananchi kulalamika sasa wakipewa nchi itakuwa hatari zaidi...wataiendesha kibabe
hivyo hawastahili kupewa uongozi hata kidogo,” alisema.


Akizungumzia ujumbe wa simu alizopokea, Bw. Ndugai alisema
si watu wote walikuwa wakimtumia (sms) za matusi, bali wengine walikuwa wakiomba ada za watoto wao, mitaji ya biashara na wale
wa Mtwara kuzungumzia suala la gesi.

“Nilichogundua, wengi wao kati ya wale niliopokea simu, lafudhi
zao ni kutoka mikoa ya Kanda ya Kaskazini, nilishangazwa kidogo
na jambo hili...kwanini wengine wasipige iwe wao tu,” alihoji.

Bw. Ndugai alisema hoja binafsi ya mbunge wa Ubunge, Bw. John Mnyika, ilikuwa dhaifu kwa sababu tayari Serikali imetenga nusu
ya bajeti ya Wizara ya Maji kwa ajili ya Jiji la Dar es Salaam.

“Alichokuwa akikifanya Bw. Mnyika ni kutafuta sifa kwa wananchi ionekane yeye ndiye aliyepigania kupatikana kwa huduma hiyo jijini Dar es Salaam, kama angekuwa makini angewasilisha hoja ya tatizo la maji nchi nzima kwani Bunge ni la Taifa.

“Nusu ya bajeti ya maji imekwenda Dar es Salaam kwenye wakazi milioni tano, nusu nyingine imekwenda katika mikoani mingine nchini yenye watu milioni 44 sasa usawa uko wapi, kwanini azungumzie Dar es Salaam pekee,” alihoji Bw. Ndugai.

2 comments:

 1. Wewe Ndungai ni mwongo, watanzania karibu wote wana lafudhi zinazofanana, unaposema waliokupigia wana lafudhi za kaskazini inaonekana unataka kuonyesha ukabila. Kwa hiyo na hao walioongea suala la gesi ni watu wa kaskazini? na hao waliokuomba ada ni wa kaskazini pia? mbona hujasema kama ni wagogo? Kuwahusisha wananchi kwa kuwapa namba zenu siyo udhaifu ila ni ujasiri mkubwa, au kwa vile walitaka uachie ngazi? Unasema kama hawakutaki wapige kura bungeni kupata 67%? wangeweza vipi wakati mnatumia U-CCM mkiwa bungeni na kukandamiza wapinzani? unajua kabisa kuwa wewe na Anna makinda mnapendelea CCM na hamuwezi kuondolewa kwa njia ya kura ndiyo maana mnafanya hivyo. WEWE NA MAKINDA MSILIFANYE BUNGE KAMA LENU BINAFSI, MMEWEKWA NA WATANZANIA HIVYO HESHIMUNI WANANCHI WOTE.

  ReplyDelete
 2. Ukasikazini kwa Vipi Ndugai..........lafudhi zao wewe unasema NINI.....Waliowaajiri ninyi mkawa bungeni ni nani......Ni sis wananchi.
  Hebu msione kuwa watu wengine hatujui msemacho.
  Ndugai jaribu kuon aya kuwa uu mtu wa kuwa na Staha ya kujibu yaliyo na UKWEILI na unachokisema ni kuwa hata iweje kinachokusukuma mseme hayo ni WINGINE wenu BUNGENI.
  BUT.........time will tell........then WE ARE SUPPOSE TO MEET THE WRONG PEOPLE BEFORE MEETING THE RIGHT ONE SO THAT,WHEN THE FINALLYMEET THE RIGHT PERSON, WE WILL KNOW HOW GREATFUL FOR THAT GIFT

  ReplyDelete