18 February 2013

Mbowe 'afunguka' mauaji ya Z'bar, Geita



Na Queen Lema, Arusha

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowem amesema mauji ambayo yametokea nchini dhidi ya viongozi wa dini mkoani Geita na Zanzibar ni matokeo ya Serikali kutofuata ushauri wao.

Alisema chama hicho ya kiliitaka Serikali isipuuze lililoanza kujitokeza kwa Watanzania wenyewe kwa wenyewe kubaguana
kwa kivuli cha imani ya dini zao lakini ushauri huo haukuweza kufanyiwa kazi hivyo kuwanyiwa wananchi uhuru wa kuadudu.

Bw. Mbowe aliyasema hayo jana mjini Arusha wakati chama
hicho kikizindua Kanda ya Kaskazini ambayo itakuwa ikitoa
huduma za kichama katika mikoa iliyopo katika kanda hiyo.

“Leo kila mahali unasikia mauji ya viongozi wa dini, tatizo hili limechangiwa na Serikali ambayo imeshindwa kufanyia kazi
ushauri tuliowapa ili mambo haya yasiendelee kutokea.

“CHADEMA tunalaani mauaji yaliyotokea kwa Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste Assemblies of God, Mathayo Kachila huko
Chato, mkoani Geita na yale yaliyotolea leo (jana), Zanzibar kwa
Padri wa Kanisa Katoliki la Minara Miwili, lililopo Mji Mkongwe, Zanzibar, Evaristus Mushi,” alisema.

Akizungumzia uzinduzi wa kanda hiyo, Bw. Mbowe alisema ni
moja ya mikakati waliyoiweka ambapo viongozi wa kanda husika wataweka misingi imara ya chama hicho kuchukua nchi 2015 ili
iwe huru zaidi kuliko ilivyo sasa.

“Kanda hii itaweza kutatua kero mbalimbali za wananchi ambazo zinawakabili, hivi sasa kazi za maendeleo zitafanywa na mikoa minne tofauti na awali,” alisema.

No comments:

Post a Comment