11 September 2012

CHADEMA watoa tamko zito kwa JK *Watangaza kumtenga msajili vyama vya siasa *Wataka tume huru, waiweka serikali mtegoni



Na Goodluck Hongo

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kuunda tume huru ya kimahakama ili iweze kuchunguza mauaji ya raia yaliyofanywa katika mikutano ya chama hicho mkoani Singida, Morogoro, Iringa, Igunga na Arumeru.

Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Freeman Mbowe, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema tume hiyo itasaidia kubaini ukweli wa mauaji yaliyofanywa na Jeshi la Polisi ili wahusika wachukuliwe hatua na jinsi baadhi ya viongozi wanavyotumika kisiasa kukisingizia chama hicho kuwa ndio kinara cha mauaji ya raia katika mikutano yao.

“Katika kikao chetu cha Kamati Kuu, tuliazimia kumtaaka Rais Kikwete aunde tume huru kuchunguza mauaji ya raia, pia tunamtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema na Mkuu wa Oparesheni Makao Makuu ya jeshi hili, Bw. Paul Chagonja wajiuzulu.

“Pia tunamtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro na Iringa wakiwemo na Makamanda wa Vikosi vya FFU katika mikoa hii, wakamatwe na kufunguliwa mashtaka ya mauaji,” alisema.

Alisema kama Serikali itashindwa kufanya hivyo, chama hicho kitaitisha maandamano nchi nzima ambayo hayajawahi kutokea katika historia ya Tanzania.

Akizungumzia kauli ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bw. John Tendwa, kuwa anaweza kuifua CHADEMA kwa madai ya kusababisha vurugu, Bw. Mbowe alisema kuanzia sasa watafuata maagizo ya sekretari wa ofisi hiyo badala ya msajiri kwani kauli yake inahatarisha usalama wa nchi.

“CHADEMA si chama cha mfukoni bali kinaongozwa kwa misingi ya sheria na katiba, msajiri asifikiri chama hiki ni cha Mbowe, bali wanachama wake ni mamilioni hivyo akikifuta atawapeleka wapi.

“Kama anataka kukifuta ajaribu aone, kuanzia sasa hatutafanya kazi na Tendwa, ila tutafuata sheria na taratibu za ofisi yake hata kama maamuzi yatatolewa na sekretari,” alisema Bw. Mbowe.

Aliongeza kuwa, Bw. Tendwa kuanzia sasa ni adui wa demokrasia na hafai kuwa katika nafasi aliyonayo ambapo CHADEMA haitashiriki shughuli zozote ambazo ataziandaa lakini kama ataomba radhi kwa matamshi yake, wapo tayari kushirikiana naye.

Bw. Mbowe akizungumzia mgogoro uliokuwa jijini Mwanza na kusabnabisha Meya wa CHADEMA kuondolewa, alisema Kamati Kuu ya chama hicho baada ya kupitia maelezo ya kamati iliyoundwa kuchunguza sakata hilo, imeamua wawavua uanachama madiwani wao wawili ambao ni Bw Adam Chigulani (Kata ya Igoma) na Bw. Henry Matata (Kata ya Kitangiri).

“Hawa madiwani wamehusika na tukio hili hivyo kukikuka maazimio na misingi ya chama chetu, tupo tayari kwa lolote na wengine wataendelea kuchukuliwa hatua,” alisema.

Akizungumzia Operesheni Sangara, Bw. Mbowe alisema itaanza  muda mfupi ujao kwani waliisimamisha baada ya mauaji ya watu wawili akiwemo marehemu Daudi Mwangosi (mwandishi wa Kituo cha Channel Ten), ili kutoa fursa ya chama hicho kuyajadili

7 comments:

  1. HONGERA CHADEMA. MSIMAMO HUO WA KUTONYWEA MBELE YA MAADUI WA UHURU WA WATANZANIA NA VIKARAGOSI WAO, KINA TENDWA NA POLISI, NDIO PEKEE WA KUREJESHA UHURU WETU AMBAO ULIPORWA NA TANU/AFRO /CCM TANGU ENZI ZA UTAWALA WA CHAMA KIMOJA. HAKI HUSHINDA! WATALIPA DAMU WANAZOZIMWAGA ZA RAIA WASIO NA HATIA!WATATAPIKA MALI ZA NCHI WANAZOPORA NA KULIMBIKIZA NDANI NA NJE YA NCHI NA KUACHA WANANCHI WAKIOGELEA KATIKA LINDI LA UFUKARA NA TABU ZISIZOMITHIRIKA. DAIMA MBELE KUDAI UHURU WA KUJIAMULIA UONGOZI(SIUTAWALA) TUNAOUTAKA, ULIOTUKUKA.!

















    ReplyDelete
  2. Tendwa hana jipya kwani ni mtanzania gani asiyejua kuwa yeye ni kibaraka wa chama tawala?

    Tendwa kateuliwa na Rais wa chama cha ccm ambachjo ndicho chama tawala kwa nini asijipendekeze kwake?

    Hakuna mtanzania mjinga wa kudanganywa eti CHADEMA ndo kinasababisha mauaji ya raia na kama ni hivyo mbona wahusika hawakamatwi na kushitakiwa?

    Polisi Tanzania inatumiwa na watawala kuhakikisha wananchi hawapewi elimu na uelewa juu ya mambo yanayoendelea.Polisi wanaua rai halafu wanasema CHADEMA ndo wanaua.

    Msajili anajiaminije mpaka kusema atafuta CHADEMA? NI upuuzi mtupu!mtupi!mtupu

    CHADEMA NI CHAMA KIPENZI CHA WANANCHI TANZANIA NA 2015 NDO KITATAWALA TAIFA HILI AMBALO LIMEBEBWA NA MAFISADI SASA HIVI.

    ReplyDelete
  3. Tendwa huna jipya afadhali ya kujiuzulu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. HIZO NDIO SIASA, SIJUI TWAENDA WAPI, TUOMBE TU NGUVU YA MOLA TUSIFIKIE VYA SYRIA, MISRI, LIBYA.... MAANA NCHI ITAKUWA HAIKALIKI.......

      PANDE ZOTE TWAZIOMBA ZIWE MAKINI NA WELEDI KATIKA KUTEKELEZA SIASA... MAANA NDIO NYANJA ZAO. SHUKRANI MUNGU IBARIKI TANZANIA,

      Delete
  4. Tendwa kufuta chadema sio mwisho wa harakati. Mbona huwafuti ccm kwa kuongoza kuiba mali, ufisadi, dhuluma na ujambazi wa wazi dhidi ya wananchi na mali zao?

    Tendwa kafie mbali. Kibaraka mkubwa sana wewe!

    ReplyDelete
  5. CCM na vibaraka wake wanafikiri watanzania hawajui ni nani wauaji na ni nani si wauaji. Hivi karibuni Afrika Kusini kumetokea mauaji ya wachimba migodi 34 ktk kudai maslahi bora ya kazi. Lakini pamoja na kuwaua waandamanaji hao haikusaidia kitu bali kumeongezeka umoja wa kudai haki.

    Huu ni mfano tu kuwa CHADEMA na watanzania wengi uelewa na ambao vitisho kwao wamevijua na kuvielewa ni mbinu ya chama tawala kudhoofisha upinzani, ni wazi kuwa hautasaidia kupunguza kasi ya mabadiliko bali ni petroli ya kuongeza nguvu ya wananchi kuidhoofisha seriakali na chama cha mapinduzi. Kitawanyike chama cha mapinduzi! Kitawanyike Chama Tawala.

    ReplyDelete
  6. Nenda kalime mchicha kwenye mabonde kazi haikufai ya kuongoza utakuja kuleta uhasama

    ReplyDelete