19 February 2013

MAUAJI YA PADRI Z'BAR Pengo atoa tamko zito



Na Waandishi Wetu

SIKU moja baada ya Padri Evaristus Mushi wa Kanisa Katoliki la Minara miwili Zanzibar, kuuawa kwa kupigwa risasi tatu kichwani na watu wasiofahamika, Askofu Mkuu wa kanisa hilo Jimbo Kuu
la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo,
ametoa tamko zito kwa Serikali.


Padri Mushi aliuawa juzi asubuhi wakati akishuka katika gari lake
ili kwenda kuongoza ibaada katika Kanisa la Betras ambapo tayari Jeshi la Polisi nchini, limeanza uchunguzi wa kina ili kuhakikisha wahusika wa tukio hilo, wanakamatwa kwa gharama yoyote.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,
Kardinali Pengo alivitupia lawama vyombo vya ulinzi na usalama
kwa kushindwa kuzuia mifarakano kati ya dini moja na nyingene.

Alisema vyombo hivyo vimeshindwa kusoma alma za nyakati kwani baada ya tukio la kupigwa risasi Padri Ambrose Mkenda wa kanisa hilo Parokia ya Mpendaye, Desemba 24,2012, wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho Zanzibar walisambaza vipeperushi vilivyokuwa na ujumbe uliokusudia kufanya jambo kubwa la uhalifu.

“Vipeperushi hivi vilikuwa na ujumbe unaosema, mapambano yataendelea hivyo vyombo vya ulinzi na usalama vilipaswa
kufanya uchunguzi wa kina ili kuzuia ualifu uliopangwa
kufanywa na wafuasi hao.

Aliongeza kuwa, tukio la kuuawa Padri Mushi halikutokea kwa dharura bali vyombo hivyo vilikuwa vinafahamu mkakati wa
jumuiya hiyo lakini bado vilishindwa kuchukua hatua.

“Padri Mushi hakuuawa akiwa baa wala sehemu nyingine tofauti na eneo lake la kazi bali mauaji yamemkuta akiwa kanisani ambako alikwenda kutekeleza jukumu lake la kikzai,” alisema.

Alisema mauaji hayo ni pigo kubwa kwa Taifa ambapo usaalama
wa imani moja ukikosekana kutokana na imani ya dini nyingine
ni tatizo na haijulikani nini kitatokea siku za mbeleni.

Alivitaka vyombo hivyo kuwa makini, kusoma alama za nyakati
ili kuzuia machafuko yanayoendelea yasitokee tena na kuwakata
waumini wa kanisa hilo, kutolipiza kisasi badala yake watulie, kuomba amani na kumuombea Padri Mushi.

Aliwataka Mapadri wengine wa kanisa hilo kuchukua tahadhari
ili kujiepusha na vitendo vya uhalifu dhidi yao na kusisitiza kuwa, umefika wakati wa viongozi wa nchi kulinusuru Taifa lisigawanyike kwa misingi ya imani za dini.

Kardinali Pengo, alisema Februari 24 mwaka huu, kanisa hilo litafanya ibada kubwa Zanzibar na Dar es Salaam kwa ajili ya kumuombea Padri Mushi.

Aliongeza kuwa, vipeperushi vilivyomfikia ambavyo alidai vimesambazwa na wafuasi wa jumuiya hiyo vina ujumbe
unaosema; “Kwa nguvu hizo, tumeweza kuyachoma makanisa
yao na kumtuliza kibaraka wa Kiislamu Soroga, alhamdulillah
hata nje hatoki (laanatullah).

“Lakini nguvu za ushindi mkubwa tulioupata ni huu wa kuwatuliza Makatoriki katika mkesha wao wanaoujua wenyewe (laanatullah), kumkosa Ambrose wa Kanisa la Mpendae, haijawa mwisho wa mapambano, tutahakikisha kila kiongozi wa Makanisa hapa
Zanzibar, hapati nafasi tena ya kuendeleza ujumbe wao”

“Wapenzi Waislamu, viongozi wetu (waliopo mahabusu), wanaendelea vizuri, ipo siku watatoka ishallah kwa nguvu za
allah, jambo kubwa la faraja viongozi wetu waliomo ndani ya Serikali na nje ya nchi, wametuhakikishia huu ndio mwisho wa kusherehekea sherehe za Mapinduzi (laanatullah)”

“Vijana wetu waliokuwa masomoni Somari, wametuhakikishia
kabla ya kusherehekea siku ya kuzaliwa Mtume Mohamed (s.a.w), kutatokeza sherehe nyingine yoyote,” ulisema ujumbe huo.

Katika ujumbe huo, Soroga ambaye ametajwa na wafuasi hao ni Katibu wa Mufti wa Zanzibar na jina lake kamili ni  Shekhe Fadhil Soroga ambaye alimwagiwa tindikali na kukimbizwa Dar es Salaam ili kupata matibabu zaidi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kardinali Pengo alisema, kutokana na vyombo hivyo kukosa umakini, ndiyo maana vipeperushi vyenye ujumbe mzito kama
huo, vilisambazwa hadi kumfikia yeye ambaye ni kiongozi wa
ngazi ya juu katika kanisa hilo jambo ambalo kama hatua za
haraka hazitachukuliwa, kutatokea madhara makubwa.

Dkt. Shein ashtushwa

Kutokana na mauaji hayo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein, amepokea msiba
huo kwa mshtuko mkubwa, kutoa pole kwa waumini, ndugu,
jamaa, marafiki na wananchi wote wa Zanzibar.

Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Dkt. Shein, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, Bw. Mohamed Aboud Mohamed, alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga upya kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama na vyengine kutoka nchi za nje ili kuongeza nguvu ya kuwasaka wauaji.

“Zipo kasoro katika Jeshi la Polisi lakini limekuwa likifanya kazi nzuri, nawaomba wananchi mtoe ushirikiano ambao utafanikisha kukamatwa wahalifu wanaofanya matukio mbalimbali.

Alisema kutokana na jiografia ya Zanzibar, kuna maeneo
ambayo watu wanaweza kupitisha silaha lakini Jeshi la Polisi
kwa kushirikiana na Vikosi vya SMZ, litaziba mianya yote.

Bw. Mohamed, alikanusha taarifa zilizopo mitaani kuwa silaha nyingi zipo mikononi mwa wasiostahili kuwa nazo na kuwataka kuondoa hofu waliyonayo kwani hizo ni njama za watu wachache wanaotaka kuiingiza nchi katika machafuko ya kidini.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete na Dkt. Shein hawapendi kusikia vitendo vya uhalifu  na uvunjifu wa amani vikitokea nchini, kutokana na sababu hizo wameomba
msaada kwa nchi nyengine kuja kufanya uchunguzi wa
kuwabaini wahusika wanaofanya vitendo hivi,” alisema.

Maalim Seif alaani

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amelaani mauaji ya Padri Mushi na kusema kitendo hicho kimevuruga sifa njema ya Zanzibar kuwa kisiwa cha amani.

Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), aliyasema hayo Kisiwani Pemba wakati akifungua semina
ya madiwani wa chama hicho.

Alisema mauaji hayo hayakubaliki kwani Wazanzibari wamekuwa wakiishi kwa kuvumiliana hivyo ni wajibu wao kuendeleza sifa hiyo kwa kuendeleza upendo dhidi yao na kuwapa matumaini wageni wanaokuja kuitembelea Zanzibar kwa shughuli mbalimbali.

Marekani walaani mauaji

Katika hatua nyingine, Serikali ya Marekani imelaani vikali tukio
la mauaji ya Padri Mushi na kutoa salamu za pole kwa ndugu,
jamaa na marafiki wa familia ya marehemu.

Balozi wa Marekani nchini, Bw. Alfonso Lenhardt, aliyasema hayo katika taarifa yake aliyoituma kwa vyombo vya habari na kusisitiza kuwa, nchi yake ipo tayari kushirikiana na Watanzania ili kukomesha matukio ya aina hiyo.

Alisema vurugu za kidini hazipaswi kupewa nafasi Tanzania nchi ambayo inasifika kwa amani na utulivu, umoja na mshikamano
wa Watanzania wote.

“Watanzania mnapaswa kupuuzia vurugu hizi ambazo zinachochewa na watu wachache wenye dhamira ya kusambaratisha amani, utulivu, usalama na taswira ya muonekano bora wa ardhi yenu,” alisema.

Jumuiya ya Maimamu

Nayo Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) imedai kupokea taarifa za mauaji hayo kwa masikitiko makubwa na kulaani kitendo hicho ambacho wamekihusisha na uharamia ili kuitia doa Zanzibar.

Taarifa waliyoitoa kwa vyombo vya habari jana na Katibu wa jumuiya hiyo, Shekhe Juma Muhiddin, imesema Zanzibar ni
kisiwa cha amani na ukarimu tokea enzi na enzi.

Alisema kutokana na mauaji hayo, jumuiya hiyo inawataka Wanzanzibari wote pamoja na dini zote, kuwa watulivu katika
kipindi hiki kigumu, kutunza amani iliyopo na mshikamano
chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Imeandikwa na Rachel Balama, Rehema Maigala, Godfrey Ismaely na Mwajuma Juma.

9 comments:

  1. There must be a political leader who empowers them, wakati fulani rais mstaafu karume alikuwa akihutubia umma, kukatokea mgkuzuno "uamsho huyo"
    Swali langu ni: 1. Je endapo ikitokea mtu kama huyo ndiye mhusika wa vurugu, je baba chkwete utamruhusu yeye kutinga mahakamani?
    2. Uchunguzi mwingine ufanywe kwa salim ahmed salim na sharifu hamad. Msibweteke na hotuba jamaa hao si wa kuaminika sana. kikulaho ki nguoni mwako.

    ReplyDelete
  2. Poleni, haya matatizo yalianza 1985 baada ya kuingia madarakani awamu ya pili. Chanzo ni wote wakiristo na waislamu mnataka kuteka nchi lakini serikali zetu zimeshindwa kuwachukulia hatua kwa sababu wanazozijua wao wenyewe.
    Nashauri serikali pamoja na hatua zingine itakazozichukua, wapige marufuku MIADHARa. Mafundisho yote yafanyike ndani ya misikiti na makanisa au maeneo yao kama wanavyofanya Ismailia, Hindu, Freemason, RC, Angalikan nk. Pili ipigwe marufuku mafundisho au nyimbo au sala za dini kwa kutumia vipaza sauti, inashangaza sala ni mausiano ya mtu na mungu wake lakini ifikia wakati sala hiyo anataka na mwingine ajue kama huyo mtu anasali.
    Sheria zipo lakini serikali ya CCM inashindwa kuzitekeleza kwa kuwaogopa CHADEMA na CUF. Kwa hiyo tatizo kubwa uenda ikawa ni CCM.

    ReplyDelete
  3. mimi nasema serkali ndiyo yenye makosa iliruhusu mihadhara ya waislam kuendeshwa nchi nzima wakiishtumu utawala wa awamu ya kwanza nakutoa matusi na lugha ya uchochezi ktk kanda mbalimbali kama vile Mfumo kristo, Waislam amkeni n.k. serkali haikuona haya? serkali ya kujihami itaanguka siku moja

    ReplyDelete
  4. HIVI KAMA MAMBO HAYA YANGEKUWA WAMAFFANYIWA WAISLAM KWELI WANGEWEZA KUVUMILIA KAMA WANAVYODAI KWAMBA TUVUMILIANE?

    TATIZO WATU HAWATAKI KUELEZA UKWELI,WANAOCHOCHEA JAMBO HILI NI WAISLAM MAANA NDIO WAMEKUWA NA MIHADHARA YA KUTKANA WAKRISTO,NA REDIO YA IMANI YA MOROGORO INAYOTUKANA WAKRISTO KILA SIKU.ZAIDI WANAJIGAMBA HAWATISHWI KWAKUWA TU UONGOZI NI WA JUU NI WAO,NA HIVI NDIVYO WANAVYOJIGAMBA.HATA WANAOSEMA WANASHUGHULIKIA WANAWAOGOPA WAISLAM

    ReplyDelete
  5. ahadi walizoahidiwa kipindi cha nyuma zimekwama kutekelezeka haya mambo ni mazito sana chanzo ni government iliyoko madarakani matukio haya yangefanywa na wakristo tungekuwa tunazungumza mengine wasitupofue wanajua nini asili ya yote hawa government

    ReplyDelete
    Replies
    1. HILI NI LETU SOTE TUSHIRIKIANE KUKOMESHA HAYA AMANI IKITOWEKA MADHARA YAKE NI MAKUBWA NA WALALAHOI TUTAATHIRIKA ZAIDI AMANI NI YETU SOTE TUILINDE

      Delete
  6. Nyero,

    Tatizo kubwa ni ukosefu wa elimu. Ukweli uko wazi tu. Elimu ipewe nafasi kubwa ili watu wengine wajua ku-analyse mambo ya dunia. Angalia kule Middleeast; tatizo nini?

    Elimu dunia ina nafasi kubwa sana.

    ReplyDelete