20 February 2013
Matokeo mabaya, tulipigania majengo tukaacha elimu
TANZANIA imefanya jitihada kubwa za kuboresha mifumo ya elimu kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM), na Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES).
Hata hivyo, pamoja na madarasa mengi kujengwa na idadi ya wanafunzi walioandikishwa kuongezeka, lazima tujiulize elimu wanayopewa watoto wetu ni ina ubora kiasi gani?
Ukweli ni kwamba, elimu wanayopewa haiwafanyi watoto wetu wajifunze stadi muhimu ambazo zitawasaidia kupata kazi, kuishi katika jamii na kutoa mchango katika maendeleo ya Taifa.
Wakati MMEM na MMES zinatia msukumo wa kuongezsa ubora wa elimu, jitihada nyingi hadi sasa zimekuwa zikielekezwa katika wingi wa vitendea kazi.
Baadhi ya wanasiasa wamepewa tuzo kwa kutekeleza ajenda ya madarasa hata kama hakuna wanafunzi, walimu ambapo jamii
inafutahi kuona shule yao ina majengo.
Sisi tunasema kuwa, suala la ubora wa elimu linapaswa kuibuliwa
na kila mwananchi ili watoto wetu wanufaike na elimu yenye tija.
Matokeo yaliyotangazwa juzi na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa, yamethibitisha kuwa ubora wa
elimu katika shule nyingi ni hafifu.
Matokeo yaliyotangazwa juzi yameibua mjadala mkubwa wa maswali ambayo hayawezi kuwa na majibu kama Watanzania
wenye watoto waliopata sifuri hawata kasirika na kutaka
kujua ukweli wa matokeo yaliyosababisha anguko hilo.
Kwa hali ilivyo sasa, tunahitaji mjadala wa kitaifa juu ya ubora
wa elimu unayohitajika ili kujenga dira ya pamoja kuhusu ubora
wa elimu. Bila kufanya hivyo , tutaendelea kutatiza uwezo wetu
wa kuwajenga watoto waweze kukabiliana na mabadiliko.
Uhamasishaji mfumo wa kufikiri unaolenga mbele zaidi, umuhimu wake unazidi kuonekana. Elimu bora inapaswa kutafsiriwa upya
kwa kuzingatia matokeo na uwezo tunaokusudia kuujenga kwa
watoto wetu.
Lengo kuu la msingi wa elimu bora kwa watoto wetu ni kujengewa uwezo ambao utawafaa kwa siku za baadaye bila kujali watafanya kazi gani ambapo uwezo wa kusoma na kuhesabu ni wa muhimu ili kumwezesjha mtoto kuyaelewa masomo mengine kwa urahisi.
Imani tetu ni kwamba, uwekezaji mpana na endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kwa walimu kabla na wawapo kazini yanahitajika. Walimu wanahitaji mafunzo kwa ajili ya
kuongeza ufahamu wao katika masomo wanayoyafundisha.
Elimu bora haipatikani kwa urahisi, inahitajika michango ya kila mtu, wanafunzi, wazazi, wajumbe wa kamati za shule, walimu, jamii, wataalamu wa elimu, uongozi wa kielimu kimkoa na
kitaifa, Serikali na asasi za kiraia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SEKTA YA ELIMU SAWA NA AFYA SIO YA KUAJIRI KILA MTU IKO KAULI KUWA NI TAALUMA ZINAZOHITAJI WITO KWANI HAKUNA MSHAHARA UNAOTOSHELEZA KUWALIPA WAALIMU NA WAUGUZI WANAJITOLEA ZAIDI NI TAALUMA ZILIZOINGILIWA NA MAMLUKI KWAO MASILAHI KWANZA WITO BAADAYE MAMLUKI HAWA WANAANDAA KIZAZI CHA MAJAMBAZI ,WAHUNI ,WAZURURAJI NA MAZUZU SI VEMA KUTUMIA KIGEZO CHA "COGNITIVE" KUCHAGUA WAALIMU NI VEMA VIGEZO VYA "AFFECTIVE" NA "PSYCHOMOTOR" NAVYO VITUMIKE
ReplyDeleteWIZARA YA ELIMU INAONGOZA KWA UDINI
ReplyDeleteFIKIRIA WAKURUGENZI WA IDARA ZA WIZARA HIYO WANAPOTUMIA UDINI KAMA VIGEZO VYA UTEUZI KATIKA NAFASI MBALIMBALI ZA KIELIMU TUTEGEMEE NINI?
MKURUGENZI WA ELIMU YA SEKONDARI ATUMIE UKABILA, WA ELIMU YA MSINGI ATUMIE UDINI KUWATEUA MA REO, DEO,WA ELIMU YA WATU WAZIMA AENDE VIVYO HIYO TUTAFIKA KWELI?
KWA MTAJI HUO KWA NINI ELIMU ISIPOROMOKE. ITAFIKIA MAHALI MAAFISA ELIMU WA MIKOA NA WILAYA WOTE WAKAWA WAISILAMU AU WA KABILA MOJA KAMA SIYO MATUSI KWA TAIFA NA FANI YA ELIMU MAANA YAKE NI NINI?
KATIBU MKUU WA WIZARA YA ELIMU ANGALIA MAJINA YANAYOPENDEKEZWA KWAKO NA WAKURUGENZI HAWA UTAGUNDUA JAMBO.
Elimu bora haipatikani kwa urahisi, inahitajika michango ya kila mtu, wanafunzi, wazazi, wajumbe wa kamati za shule, walimu, jamii, wataalamu wa elimu, uongozi wa kielimu kimkoa na
kitaifa, Serikali na asasi za kiraia.
Kweli ndugu yangu kama ulikuwepo
ReplyDeleteMabosi wa wizara ya elimu wamegeuza ofisi zao kuwa vijiwe vya kunyanyuana hata kama mtu hana sifa,maadamu awe mtu wa kabila lake, dini yake na zaidi rushwa ndio haisemeki. kuteuliwa nafasi ya ofisa elimu wilaya mpaka utoe rushwa hata kama huna uzoefu wanaotaka. Zuberi anaangalia majina ya Waislamu ni kweli kabisa mbona ndiyo zake tangu apewe ukurugenzi.