20 February 2013

MATOKEO IV Shule zenye majina ya vigogo aibu *Ndio zilizofanya vibaya zaidi, wananchi wahoji



Rehema Maigala na Rose Itono

SHULE za sekondari zinazotumia majina ya watu maarufu nchini yakiwemo ya viongozi, zimefanya vibaya kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotangazwa juzi na Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa.

Uchanguzi uliofanywa na Majira, umebaini miongoni mwa shule hizo ni pamoja na zinazotumia majina ya Marais wastaafu na
Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete.

Shule nyingine ni zile zinazotumia  majina ya Mawaziri na watu wengine maarufu waliowai kushika nyadhifa mbalimbali za
uongozi nchini katika Serikali za awamu tofati.

Miongoni mwa shule hizo ni Sekondari ya Lowassa ambapo wanafunzi waliopata daraja la pili (4), III (9), IV (51), ambapo waliopata 0-131.

Sekondari ya Benjamin William Mkapa, wanafunzi waliopata I (2), II (32), III - 41, IV 188, waliopata 0-199, ambapo Sekondari ya Ali Hassan Mwinyi, I (1), II (hakuna), III (3), IV (53), waliopata 0-182.

Katika Sekondari ya Jakaya Mrisho Kikwete, hakukuwa na mwanfunzi aliyepata daraja la I-III, IV (17) na waliopata 0-110. Sekondari nyingine ya  Jakaya Kikwete, hakuna mwanafunzi
aliyepata daraja III, IV (17), waliopata 0-59.

Sekondari ya Dkt. Wilbroad Slaa, nayo haikuwa na wanafunzi waliofaulu I-III, IV- (17), waliopata 0-22 ambapo Sekondari ya
Samwel Malecela nayo haikuwa na wanafunzi waliofaulu
kuanzia I-III, IV- (7), waliopata 0-32.

Katika shule ya Sekondari J.K. Nyerere, daraja la I- (1), II (13), IV (94), waliopata 0-115. Shule ya Sekondari Sumaye daraja 1 (1), II (3), III (11), IV (59), waliopata 0-185, ambapo Sekondari ya Cleopa Msuya, hakuna mwanafunzi aliyepata daraja I-II, III (2), IV (27), waliopata 0-90.

Sekondari ya Kawawa, wanafunzi waliopata daraja I (2), II (4), III (15), IV (85), waliopata 0-73, Sekondari ya Yusuf Makamba, hakuna mwanafunzi aliyepata daraja la kwanza, II (1), III (11), IV (52), waliopata 0-334.

Katika Sekondari Karume, hakuna mwanafunzi aliyepata daraja I-III, IV (14), waliopata 0-18, Sekondari ya Maria Nyerere, hakuna aliyepata daraja la I, II (2), III (7), IV (52), waliopata 0-63.

Sekondari Mwapachu, hakuna mwanafunzi aliyepata daraja la I-III, IV (11), waliopata 0-103. Katika Sekondari ya Isdore Shirima, hakuna mwanafunzi aliyepata daraja la I-III, IV (4), 0-57, ambapo
Sekondari ya Chenge hakuna aliyepata daraja la I-III, IV (18), 0-26.

Katika Sekondari ya Regina Mumba Lowassa, hakuna mwanafunzi aliyepata daraja la I-III, IV (7), 0-37, Sekondari ya Willium Lukuvi hakuna aliyepata daraja I, II (1), III (3), IV (22), 0-10.

Sekondari ya wasichana ya Mandera, hakuna mwanafunzi aliyepata daraja la I-II, III (5), IV (60), 0-106. Katika Sekondari ya Mkuchika hakuna mwanafunzi aliyepata daraja I, II (2), 0-22.

Shule ya Sekondari Celina Kombani, hakuna mwanafunzi aliyepata daraja la I-III, IV (2), 0-77, Sekondari ya Ngwilizi, hakuna aliyepata daraja la I-III, IV (10), 0-32. Katika Sekondari ya Karamagi, hakuna waliopata daraja la I-III, IV (9), 0-31.

Sekondari ya Balozi Mshangama, hakuna mwanafunzi aliyepata daraja la I-III, IV (6), 0-39, katika Sekondari ya Mizengo Pinda, hakuna waliopata daraja la I-III, IV (11), 0-47, wakati Sekondari
ya John Samwel Malecela, hakuna aliyepata daraja la I-III, IV (7),
waliopata 0-32.

Katika Sekondari ya Seth Benjamin, hakuna waliopata daraja la I-II, III (2), IV (14), 0-69. Sekondari ya Salma Kikwete, hakuna waliopata daraja la I, II (6), III (14), IV (128), 0-123.

Sekondari ya Monika Mbega, hakuna waliopata daraja la I-III, IV (1), 0-25. Katika Sekondari ya Sakila Bujiku, hakuna aliyepata daraja I, II (2), III (3), IV (37), 0-96, wakati Sekondari Philip
Marmo, hakuna waliopata daraja la I-III, IV (23), 0-59.

Katika Sekondari Mwanamwema Shein, hakuna aliyepata daraja la I, II (1), III (1), IV (12), 0-56, Sekondari Ali Shein, hakuna aliyepata daraja la I-II, III (1), IV (7), 0-26.

Sekondari ya Pius Msekwa, hakuna waliopaata daraja la I-II, III (2),  IV (21), 0-128, katika Sekondari ya Rashid Kawawa, hakuna aliyepata daraja la I-II, III (2), IV (17), 0-101.

Shule ya Sekondari ya Murad Saddiq, hakuna aliyepata daraja la I-II, III (2) IV (16), 0-109. Sekondari ya Gerge Washngton, hakuna aliyepata daraja la I-III, IV (2), 0-22.

Kutokana na hali hiyo, wananchi mbalimbali waliozungumza na gazeti hili, walisema viongozi ambao majina yao yanatumika
katika shule hizo, wanapaswa kuzisaidia ili majina yao
yaendelee kuheshimika kwenye jamii.

2 comments:

  1. Kati ya majina yote hayo aliyestahili kupewa heshima ni SETH BENJAMIN PEKE YAKE. Wengine wote ni UCHURO TU

    ReplyDelete
  2. MBONA ZA WATAKATIFU ZIMEFANYA VIZURI

    ReplyDelete