16 November 2010

Slaa amkataa Kikwete.

*Asema urais wake ulitokana na matokeo yasio halali
*Mbowe asisitiza watadai haki kwa misingi ya amani
*Adai wanajipanga kutoa vielelezo vya wizi wa kura
*CHADEMA kutokubali uteuzi wowote wa Rais Kikwete


Na John Daniel, Dodoma.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeseama hakitambui matokeo ya urais wa uchaguzi mkuu uliopita pamoja na
Rais Jakaya Kikwete aliyetokana na matokeo hayo.

Sambamba na hatua hiyo, chama hicho kimesema kitaendelea kudai uume huru ya uchaguzi pamoja na katiba huru bila kukata tamaa.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari mjini hapa jana, aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho, Dkt. Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Freeman Mbowe walisema kamwe hawawezi kumtambua Rais Kikwete kwa sababu ushindi wake 'ulichakachuliwa', hivyo kumtambua ni kutowatendea haki Watanzania.

"Nilishatoa tamko siku chache baada ya uchaguzi na leo narudia tena, sitambui matokeo ya urais na wala simtambui rais aliye madarakani, lengo la demokrasia ni kuwapatia wananchi kiongozi wanayemtaka, hatukuwa na uchaguzi huru wala wa haki, tuliandika barua tume kueleza tulivyobaini matatizo ya uchaguzi na tume ilikiri, lakini hadi leo haijatoa ufafanuzi wa hatua zilizochukuliwa," alisema Dkt. Slaa.

Alisema kitendo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kukiri kuwepo kwa matatizo ni ishara kuwa chombo hicho kilishindwa kusimamia uchaguzi, ama kwa sababu ya uzembe wa watendaji au ilishiriki 'kuchakachua' kura za chama hicho kwa makusudi.

"Nawashukuru Watanzania wote walionipa kura, kama mnavyojua siku za kampeni zilikuwa 71 lakini tuna majimbo ya uchaguzi 239, hata kwa miujiza nisingeweza kufika kila mahali lakini Watanzania wengi walinipa kura nyingi, jukumu langu kama mgombea ni kusema hayo mengine na hatua inayofuta ni ya chama chenyewe, mambo yaliyobaki sasa nakiachia chama," alisema Dkt. Slaa.

Alisema kutokana na jinsi Watanzania walivyojitokeza kumpigia kura hawezi kukata tamaa kudai haki na kuongeza kuwa safari ya ukombozi wa nchi ni ndefu, hivyo ataendelea kudai haki na kuwaomba Watanzania waendelee kukiunga mkono CHADEMA kwa kuwa mapungufu
yaliyojitokeza katika mchakato huo yatabakia kama yalivyo na kamwe hatabadilika wala yeye kukubali matokeo ambayo si sahihi kwa utashi wake.

Akijibu maswali ya waandishi kuhusu sababu iliyomfanya ashindwe kuwataja maofisa usalama walioshiriki kuchakachua kura zake alisema yeye kama mtu makini hawezi kutoa kila kitu mapema na kuwataka watu wanaodai amewadhalilisha au kusema uongo waende
mahakamani ili akawaumbue kwa ushahidi alio nao.

"Namshangaa sana yule Naibu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, kutaka niwapelekee ushaidi, ushahidi unapelekwa Usalama wa Taifa ili waupeleke wapi wao?" alihoji na kuongeza.

"Nawapa changamoto kama nilivyokwishawaeleza waandishi wa habari awali, kama nimesema uongo waende mahakamani, nitatoa ushaidi wangu mahakamani," alisisitiza Dkt. Slaa.

Kwa upande wake Bw. Mbowe alisema awali walipobaini mwenendo usioridhisha wa uchaguzi Mkuu walitoa tamko la kuitaka NEC kusitisha kuendelea kutangaza matokeo hayo lakini hawakusikilizwa na kwamba njia pekee wanayoweza kufanya kwa sasa ni kudai
kuundwa kwa tume huru ili kuchunguza sababu ya idadi kubwa ya Watanzania kushindwa kujitokeza kupiga kura.

"Tunadai iundwe Tume Huru ya Uchunguzi na kutambua sababu iliyosababisha wengi kushindwa kujitokeza kupiga kura, ua kama walipiga kura lakini kura zao hazikuonekana," alisema Bw. Mbowe.

Alisema sia sahihi kwamba CHADEMA pekee ndicho kinachosikitishwa na idiadi ndogo ya watu waliojitokeza kupiga kura, bali hata wananchi wenyewe wamekuwa wakihoji tatizo hilo kubwa la kidemokrasia nchini.

Kuhusu NEC na hatiba huru, Bw. Mbowe alisema CHADEMA itaendelea kudai kuwepo kwa Tume huru ya uchaguzi na katiba inayokidhi haja ya Watanzana kwa kuwa iliyopo sasa inalinda maslahi ya chama tawala na watu wachache wanaofaidika na chama hicho.

"Tutaendelea kudai Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba inayokidhi haja ya Watanzania ndani ya Bunge kupitia wabunge wetu, nje ya bunge na hata nje ya nchi, tutaendelea kukataa matokeo ya urais na kutokumtambua aliyeshinda kwa matokeo hayo ingawa tunaelewa wazi kuwa sheria za nchi na katiba inaeleza kuwa rais akishatangazwa hakuna chombo wala mamlaka ya kuhoji ushindi wake.

Hatuwezi kukaa kimya, kufanya hivyo ni unafiki na udhaifu ambao hatuwezi kuukiri, kwa kusema hivi hatuwatumi Watanzania kuingia barabarani, tutaendelea kudai haki kwa amani," alisema Bw. Mbowe.

Alipoulizwa uhalali wa wabunge wa chama hicho kuendelea kukaa bungeni kusikiliza hotuba ya rais ambaye hawamtumbia na kupitisha jina la waziri mkuu ambaye atateuliwa leo na kiongozi wasiyemtambua, alisema msimamo huo wa kutomtambua rais haiwafanyi wawakilishi kupitia CHADEMA kutotimiza wajibu wao kwa kuwa huo ni udhaifu wa katiba iliyopo sasa ambayo wanalazimika kuifuata japo ni mbovu na haikidhi matakwa ya Watanzania.

"Mabadiliko katika taifa ni process (mchakato) lakini kila jambo tunalofanya inajenga tofauti moja, tunaendelea kudai Tume Huru na Katiba mpya, kwa njia mbalimbali, msije mkashangaa mtakaposikia CHADEMA inapanga na kufanya maandamano sehemu mbalimbali
nchini," alisema Bw. Mbowe.

Akijibu swali kuhusu ushirikiano wa vyama vya upinzani bungeni, Bw. Mbowe alisema CHADEMA imeacha milango wazi kwa chama chochote makini kuungana nao lakini hawako tayari kuungana na chama ambacho hakipo makini.

"Jambo muhimu siyo kuunganisha vyama vya siasa, muhimu ni kuunganisha fikra na mawazo yanayokubaliana, tuko tayari kushirikiana na chama chochote makini, inashangaza kuona chama cha upinzani kikitupeleka mahakamani kudai fidia ya mabilioni," alisema Bw. Mbowe bila kutoa ufafanuzi wa kina.

Alipoulizwa kuhusu vielelezo vinavyothibitisha kura zao kuibwa na chama tawala, alisema watatoa taarifa ya kina na vielelezo vyote baada vikao vya juu vya Kamati Kuu na Baraza Kuu vya CHADEMA
kukutana na kuridhia hatua hiyo.

Alisema vikao hivyo vitafanyika hivi karibuni na kuongeza kuwa tamko walilotoa jana lililenga kufuta dhana kwamba wameridhika na kila kilichotokea katika uchaguzi mkuu na kwamba walishirikisha wabunge wa chama hicho na baadhi ya viongozi katika tamko
hilo kabla ya kulitoa kwa wana habari.

24 comments:

  1. Slaa aangalie viongozi wa vyama vingine wanavyo behave. Yeye ana behave kama vile warrior soldier, anataka watu wafukuzwe kazi, wauawe, wapigwe, wachinjwe, wafilisiwe, wakomolewe. Sasa amekomolewa yeye. CCM na CUF wataongoza hii nchi na yeye na Chadema watabaki kuropoka. CCM na CUF wameungana, wanapendana, wanaheshimiana kimatakwa na ki-mtazamo, ki-uongozi. Yeye badala ya kuungana na wenzie anataka visasi, nani anamtaka madarakani huyu Slaa. Anachemsha kila siku kwa maneno yake mabaya akifikiri anawafurahisha watu. Hafai popote, akatubu kwanza madhambi yake ndipo ayaone ya wenzie. Anataka kuikwepa mahakama kwa kuiba mke wa mtu na watoto kwa kutumia cheo cha Urais, Waapi.... tunakuombea sheria ikuguse bega tu mzee. Una sera lakini huna dira. Uongiz wa kuropoka si uongozi. Anawa haribia kazi wenzie katika chadema. Chadema, mtoeni huyu Slaa, wekeni mtu mwingine. Ametuchosha huyu. mtu mzima hovyoo.. kila siku kelele za majungu, wivu na fitina. Basi JK kapita sasa chukua chupa umeze.

    ReplyDelete
  2. Petro Eusebius MselewaNovember 16, 2010 at 10:20 AM

    Kila mtu ana mawazo yake,msimamo wako,akili zake,fikra zake,mwili wake na chochote chake.Hapa namaanisha kwamba Dr.Slaa na Mbowe wamesema waliyoyaona na kuyaamini wao.Wasiingiliwe wala kupingwa bila hoja mujarabu.Wana haki yao Kikatiba.Hata ningekuwa mimi,kama sikuridhishwa mwanzoni siwezi kuridhishwa katikati.Hivi Dr.Slaa akikubali sasa matokeo na kumtambua Rais wananchi watamuonaje? Kwanini aanze sasa na si pale Karimjee au Uwanja wa Taifa? Amehongwa? Hana jinsi? Dr.(Ph.D)Slaa anakwepa maswali ya namna hiyo.Songa hivyo Dr.!

    ReplyDelete
  3. Nilitegemea watu wenye fikra mgando kama wewe (anonymous, first comment) watakuwepo tu hapa nchini na ni wachache sana-Either ni kwa sababu ya akili finyu(Ujinga), Au na wewe unafaidi matunda ya ufisadi. Kwa mtu kama wewe, Slaa hatakufurahisha kamwe lakini ujue kuna maelfu ya watanzania anawafurahisaha sana na tunamuona kama mkombozi wetu.. Ukipendana na kuheshimiana na fisadi basi na wewe ni fisadi hivyo usitegemee hata siku moja chadema eti ipendane na nyi nyi em. Unataka asiulize.., asiseme kama hakufanyiwa haki.. ndio maana, ndio maana nchi hii haiendelei kwa sababu no one is able to question.. they'v killed ur minds.. kila kitu, YES! Tutafika..? Badilika tuikomboe nchi yetu, Kuna watu wana maisha magumu hata kumnunulia mtoto wao daftari la sh. 100 hawawezi! Acha ubinafsi, acha kujiangalia mwenyewe tu.. Imenibidi niseme

    ReplyDelete
  4. First comment ana mawazo mgando,kwani hakuona masanduku ya kura yalikamatwa tarime? Watanzania wa sasa wameamka, hivyo Dokta Slaa ni mkombozi wetu. Rasilimali za taifa zinaibwa kweupe, CUF wako kimya!!!
    Sasa ona MWai Kibaki amesema atashusha bei ya cementi, Museveni anatoa Elimu Bure. Zote hizo wameiga Chadema.

    Peoples Power, Chadema twende

    ReplyDelete
  5. Ama kweli vichaa ni wengi Tanzania.Kumbe anonymous wa pili na wa tatu wanaungana na kichaa mwenzao dr silaa siyo?naona walikuwa msiuni sasa wamerudi kama walivyosema mwanzo?nashangaa sana,wizi wa kura ni pale tuu mliposhidwa lakin majimbo mliopata kura nyingi hamkuibiwa.sasa tuwaeleweje nyinyi wa dr silaa?siasa siyo mchezo wa kuigiza wajameni,kushinda na kushindwa ndiyo fomila yake,na si vinginevyo.wachu wa dr silaa mnakuwa kama mtu anayekwenya kupima ukimwi,badala ya kutegemea majibu ya positive na negative yeye anakuwa na jibu la negaive pekee ndiyo maana akipaa majibu ya positive anakufa baada ya siku chache.wakati angekuwa amejenga kuwa majibu yoyote yanaweza kuwepo angeishi kwa muda mrefu saana.
    Kweli kama chadema wanamkataa raisi na bungeni wasiende kabisa ili kweli tuone wanajali watanzania kama wanavyojinadi kwa watanzania?wanakimbilia dodoma kuchukua mashangingi huku wanamdanganya huyo dr wa masilahaa ili awaone wako naye.hiyo ni danganya toto bwana.najua chama cha upinzani tanzania ni cuf pekee,walikataa matokeo na wabunge wao walikataa kwa kipindi cha miaka mitatu bila kuchukua mali ya walipa kodi,hao ndiyo wapinzani wa kweli bwana.

    ReplyDelete
  6. Dkt. Slaa asonge mbele wala asitishwe na walioshiba na ufisadi wa CCM,ukisikia mtu anayemkandia Slaa au CHADEMA anayo hisa aidha katika makampuni yanayomilikiwa na mafisadi wa CCM au ni mtoto anayetafuna vinono vya babake ambaye ana ushirika vigogo vya CCm, anayempinga Slaa hivi yuko nchi gani,haoni askari wetu polisi, magereza wanavyishi maisha ya taabu miaka 50 baada ua uhuru? ametembelea mitaa ya miji yetu na vijijini kuona maisha wanayoishi Watanzania? Eti anatuambia muafaka kati CCM na CUF, CUF ambayo tunaifananisha na Mbwa anayepiga kelele kwa sababu ya njaa akishatupiwa hata mifupa kimya!!!.tunaiomba CUF kama ni chama pinzani kweli irudi kwenye mistari ya kuwatetea walalahoi watanzania.Eti wanasema kuwa Slaa anataka kuleta vita apigane na nani, hatutaki fikra za mgando tunahitaji Tanzania ya haki,Tanzania ambayo raia zake wanafaidi matunda ya nchi kwa usawa.Wewe unayepinga CHADEMA hujui kwamba CHADEMA ndicho chama kinachofanya CCM irekebishe mambo angalau kidogo.kama utakuwa na chama cha upinzani kinaweka muafaka na chama tawala ujue kimekwisha.jifunze kwa Republican na Democratic kule Marekani hakuna ambacho kinaweza kuingia muafaka na kingine kwa sababu viko pale kukoseleana.Tanzania tunahitaji vyama kama hivyo na CHADEMA imeonesha njia.tumuunge mkono Dkt. Slaa asonge mbele.

    ReplyDelete
  7. first comment (Said) wewe hufai kwa ukombozi wa Tanzania unaifurahia CUF na CCM kushirikiana kwa sababu ya udini uliokithiri ndani mwao (islamic) ndo mana unaona vizuri sana. fikiri sana kuwa ni watanzania wangapi wanaombwa kura na Kikwete na wanaishi mazingira magumu? na wanahalimbaya ya maisha? lakini yy anaishi pazuri hata anadiriki kuwapa uongozi wakimbizi Mfano Babati vijijini? anamiliki Muhindi ni mtanania? nauliza asitetee maslahi ya Chama bali maslahi ya wananchi basi kama hivyo aongoze watu wanaompenda kama Bagamoyo huko kwao mana wanamaisha mazuri.
    Hivi aibu hana anakaa ikulu wakati ameshindwa kushusha bei ya vifaa vya ujenzi kwahiyo watanzania tuendelee kuishi vyumba vya kupanga tuzaliane vyumba vya kupanga, tusomeshe vyumba vya kupanga, hivi watanzania kwa hali hii tutafika kweli vijana tuna hali mbaya kwa chama tawala.

    ReplyDelete
  8. huu usisiem umewalemaza watu, wakipewa tisheti moja basi ndo wanadaganyika wanasahau msoto wa miaka 5, hebu watanzania tokeni chini ya gunia jeusi mlilofunikwa usoni mnataka malaika ashuke aseme ndipo muamini? basi akishuka na ujira wake mkononi kumlipa kila fisadi sawasawa na matendo yake ndipo siku mtajua kuwa mkombozi wa kweli wa wanyonge ni nani, na nani anatetea maslahi binafsi ya washikaji wachache?.hata huko zbr tunakosifia amani kiongozi wa upinzani alikuwa na msimamo uliopelekea kuleta/kusababisha kura ya maoni ya serikali ya umoja, na wananchi wengi wakapigia kura ya kukubali serikali ya umoja , ni mchakato mrefu, leo tunawapongeza zbr kwa utulivu unadhani wamefika hapo walipo kirahisirahisi tu? wapo wanaoona kama dr Slaa anakosea , sawa na waone hivyo, nataka nikuambie hata nabiiMusa alipotumwa kuwatoa wana wa Israeli Misri wapo waliombeza, nabii Yeremia alipowaendea wafalme kuwatabiria mambo ayatakayowapata endapo hawatamtii Mungu walimbeza na kumburuza rumande na kumtesa, baadae yalipokuja kutokea kiuhalisi ndo wanazinduka na kukubali wakati wamekwisha chelewa.MWENYE MASIKIO YA KUSIKIA NA ASIKIE.

    ReplyDelete
  9. Huyo 1st Anonymous hawezi akawa mtanzania mwenye uchungu na nchi yake, Otherwise ni mpambe wa hao wanaochukizwa na mapambano ya Dr dhidi ya mafisadi. Hivi nani asiyejua kuwa ccm ni master kwenye wizi wa kura, kule nyamagana na Ilemela wameshindwa wakatumia kila mbinu ili wabadili matokeo nguvu ya wananchi ikasaudia kunusuru hilo tatzo, tatzo la huyo 1st anonymous ni kuwa mwenye shibe hamjui mwenye njaa!

    ReplyDelete
  10. watake wasitake,mabadiliko ni lazima,mnamkumbuka yule waziri wa saddam hussein aliyekuwa anakanusha kila kitu lakini mambo yapo tofauti?huyo jamaa wa kwanza na baadhi wanaofuata achanane nao maana kny msafara wa mamba na kenge nao pia wamo,hao ni kenge.Wanamapinduzi wenzangu safari ya mabadiliko imeanza na wabishi wameshaona dealili zote,tutafute haki kwa njia ya amani pasipo kumwaga damu na tuwaondoe manyang`au wote wanaofilisi mali za umma ambao wamo nky chama cha sisiemu.Wamemtosa 6 hawajui kuwa wanajipalia makaa 2015?mama makinda anafahamika kwa jazba zake na ufahamu mdogo wa kupambanua mambo.sina hakika km atamaliza hata mwaka maana kuna kina tundu lissu,mdee,mnyika,zitto,sugu,msigwa,jamaa wa mwanza,naona safari ya chama cha mafisadi imewadia,people`s power!

    ReplyDelete
  11. Acheni unafiki, Chadema ni wanafiki sana maana haiyumkiniki mtu haitambui serikali iliyopo madarakani lakini mnakwenda Bungeni na kuunda serikali ya upinzani, mnampinga nani?

    KAMA KWELI DR SLAA HATAMBUI MATOKEO YA URAIS YANAYOMPA JK HAKI YA KUUNDA SERIKALI, BASI YEYE NA WABUNGE WAKE WAONYESHE KWA VITENDO. WATOKE HUKO BUNGENI, NA WASISHIRIKI KIKAO HATA KIMOJA, wakishiriki tu tayari wamekubali kuwepo kwa serikali ya CCM na Rais wake.

    PILI WASIPOKEE PESA YOYOTE YA RUZUKU INAYOTOKA KWENYE HIYO SERIKALI AMBAYO HAWAITAMBUI. mtu unakataa mbele ya vyombo vya habari huku nyuma mnapokea ruzuku kutoka serikali hiyo hiyo mnayoikataa?

    TATU VUNJENI HIYO SERIKALI YENU YA UPINZANI, MNAMPINGA NANI NA SERIKALI IPI? nashangaa, utapingaje serikali ambayo huitambui kama serikali, kuunda serikali ya upinzani au kushika uongozi wa upinzani bungeni maana yake ni kukubali kuwa hiyo serikali iliyopo na wabunge wake wameshinda kihalali na kwa kuwa ni majority wanaongoza nchi.

    KATAENI KIKWELI KIKWELI KAMA CUF KIPINDI KILE NDIO TUTAWAONA KWELI NYIE NI WANAUME WA SHOKA. KUKATAA GANI HUKO WAKATI MMEKWISHAKWENDA BUNGENI NA POSHO KARIBU MTACHIKICHIA? TENA MUMEMCHAGUA KUGOMBEA USPIKA NA UNAIBU SPIKA? KUSUSA GANI AU KUKATAA GANI HUKO NUSU NUSU?

    Tena wanyamaze kimya wale vyao kimya kimya na ubinafsi wao hawana msimamo wako sitaki nataka, na leo kama wao vijogoo Mheshimiwa Rais akiingia ndani ya ukumbi wa Bunge watoke nje na wamwambie mbele ya uso wake kuwa tunatoka kwa sababu hatukutambui kama rais wa nchi hii! Nyambaff! Danganyeni hao hao watoto wadogo sio sie watu wazima na mvi zetu!

    ReplyDelete
  12. HUYU SILAHA KWELI HANA SIFA YA UONGOZI WALA SI MUUNGWANA UDOKTA WAKE NI UBABAISHAJI NA UHAMASISHAJI NA NDIO MAANA ALISHINDWA KULITII KANISA, NA HAWA WENZAKE NI WAFANYA BIASHARA HAWANA UKWELI UNAMKATAA KUMTAMBUA KIONGOZI WAKATI UNAMTII? NA HUNA JEURI YA KUPINGA MAAMUZI YAKE, HIVI ALIYEMDANGANYA SILAHA KUWA LAZIMA ATAKUWA RAISI NANI? MAANA KAANZA KUJIIBIA KURA,KUJIDHULUMU, KUWEKA KARATASI ZA BANDIA, KUSHUTUMU USALAMA WA TAIFA HAYA YOTE NI MBINU ILI AJE ADAI ALIYOSEMA NDIO YAMEKUWA, MAANA YEYE HATA HUO UDAKTARI WA KANISA ALIUPATA ZAIDI NI FANI YA PROPAGANDA ILI AWARUBUNI WATU WAMWAMINI,WOTE HAWA NI WANAFIKI HAWAFAI KUOGOZA NA NI HATARI KWANI SASA NDIO TUNAONA UKWELI WAO NI WENYE TAMAA YA MADARAKA, MALI, NA NIA YA KULIPIZA VISASI-KIGMB

    ReplyDelete
  13. HIV CHADEMA INAONGOZWA NA MALAIKA NINI? NAOMBENI JIBU NDUGU ZANGU. MAANA KILA WANALOSEMA WAO NI KAMA AYA YA MSAHAFU WA KIISLAM AU BIBLIA, NI MARUFUKU KUPINGA. JAMANI HII NDIO SIASA KWELI? MNAWAWEKA WANACHAMA WENU ROHO JUU BURE KUONA KWAMBA MMEIBIWA NA WALA SI KWELI. HEBU SEMA UMESHINDIA WAPI? TOENI USHAHIDI BASI. KILA SIKU WEWE TU MAGAZATENI KWANI WEWE NDIO NANI? AU UMENUNUA MAGAZETI HAYA YAKUNADI?? UNAKUA KAMA MTOTO IDD WA J NATURE BWANA!!!!! SH'HOMMMO NAROBONG'OTONI.

    ReplyDelete
  14. Wewe uliyechangia hoja wa kwanza na wa mwisho mna mawazo mgando kabisa. hata ndugu zenu huko kijini humuwatakii mema, wataendelea kuishi kama wanyama wa porini. Nadhani ninyi wote mnaotoa maoni mgado huku mkiunga mkonao wizi hamjaenda shule na hata jamii zenu zote hazijaenda shule, hamjui maana ya HAKI ya kila mtanzania.

    ReplyDelete
  15. Na wewe unayewaambia wenzako hawajaenda shule, bora wao hawajaenda shule wana akili na hawadanganyiki kuliko wewe uliyekwenda shule lakini unadanganyika kirahisi. Tumewakataa Chadema kwa kuwa tunajua ni mabepari na Mwalimu Nyerere alitwambia kuwa Ubepari ni unyama na kweli leo tunauona kwa macho. Hebu aangalie tu huyo Mgombea wenu viti vingapi vya ubunge mmepata mlinganishe na viti vya ubunge vya CCM. Kiakili tu ya kawaida kweli mngeweza kushinda urais wakati hata maeneo mengine hamkuweka wagombea wala hamkufanya kampeni?

    Sasa temeni pesa za watu mlizokula, rudishieni wenyewe pesa zao msituletee fujo bure. Tunajua mlichukua pesa nyingi za wafanyabiashara wakitegemea washike Ikulu na njia kuu za kiuchumi wazidi kupurura nchi hii. Sasa tunawaambia hivi kibano kinachofuata sasa hivi mtajuta kukwepa kulipa kodi na kuiba umeme na kuiba kwa kalamu kwenye mabenki na mashirika mengine.

    Hivi nauliza hamuoni AIBU SALAMU ZA PONGEZI KUTOKA NJE YA NCHI ZINAVYOMIMIKA KWA JK? Maana watu wanawaona ni wehu tu na wenye tamaa ya madaraka, hakuna hata mmoja anayestuka na hizo propaganda zenu. Kwanini hamjiulizi mara mbili mbili, mbona Zimbabwe na Kenya Kibaki na Mugabe hawakupewa salamu za pongezi, maana naona mnataka kutumia mtaji kama wa Zimbabwe lakini hebu jiangalieni jumuia ya kimataifa imewadharau kama tambara la deki!

    ReplyDelete
  16. NYie watu mnazozana nini? Mwacheni Dr. Slaa anadai haki yake, ni kweli baadhi ya majimbo yalichakachuliwa walishinda chadema lakini ushindi walipewa CCM wewe anonymous wa 4,11,12 hmna akili kbs mnamawzo finyu hao mafisadi wanawapa nini? sana sana ni kofia na tshirt, ANONYMOUS WA 4, yeye ndio kichaa aliye kosa mwelekeo kabisa ni bendera fuata upepo. Watanznia tunahitaji uongozi bora na mabadliko katk nchi hatutaki kuendeshwa kidkiteta. Slaa upo juu.

    ReplyDelete
  17. Chadema ndiyo mkombozi wa Tanzania. CCM watang'oka tu. Adolf Hittler na utawala wake wa "Third Reich" alidai utadumu miaka 1000 lakini kwa nguvu ya washirika na juhudi za pamoja utawala wa dictator huyu ulidumu kwa miaka 12 tu. Ushindi aliopokonywa Dr. Slaa tumepokonywa sote kama watanzania. Kwa nguvu ya Umma na msaada wa Mungu tutashinda tu.

    ReplyDelete
  18. Mimi ni miongoni mwa watu wanaotaka kuona demokrasia inaimarishwa nchini Tanzania. Vyama vya upinzani Tanzania kwa sasa vinaonyesha mwelekeo hasa CHADEMA. Dr. Slaa lazima aonyeshe kukomaa kisiasi, hawezi kusema hatambui serikali ya nchi anayoishi na kutaka siku moja kuwa raisi wa Tanzania. Unapogombea uongozi wa kuongoza watu, uchaguzi hauwi halali tu pale unapochaguliwa, mwingine akichaguliwa haukuwa halali! Huo ni uchanga wa kisiasa na kimawazo. Madai ya matatizo ya kura yaliyojitokeza hatakama yangerekebishwa kama Dr. Slaa anavyodai bado Rais Kikwete angeshinda. Dr. Slaa na CHADEMA wako kwenye njia sahihi kuelekea Ikulu, ila wanatakiwa kujua kuwa wananchi wanatakuona ukomavu wao katika matamshi yao.
    Mungu abariki Tanzania.

    ReplyDelete
  19. hivi Dr.slaa kukataa kuitambua serikali ya kikwete kuna kosa gani?mbona CUF walikataa serikali ya Salmin Amour, hata karume kulikuwa na kosa gani,au kwa kuwa CUF wamekubaliana na CCM katika muafaka na maridhiano yao fake iwe kigezo cha CHADEMA kukubaliana na ufudu wa ccm?jamani CHADEMA wana uhuru na mtizamo wao kama chama kukubaliana na hata kukataa na jambo lolote lile ambalo wao wanaona linafaa au halifai katika maendeleo ya nchi yetu, nawashangaa wenye mgando wa mawazo kuwa CHADEMA kukataa kumtambua fisadi Kikwete kuwa ni usaliti eti kwa kuwa CUF wao wanashirikiana na CCM fisadi, ukitembea na mwizi nawe u mwizi tu, CUF mmeiba na nyie mpo njia moja na CCM - ni wafisadi wote

    ReplyDelete
  20. Nimejaribu kusoma kwa makini maoni mbalimbali, nimeelewa kuwa wengi wanatoa maoni yao kiitikadi na sio kimantiki. Hivi mtu akiwa na kosa na yeye akafanyiwa kosa na mwingine, anarruhusiwa kulalamika au la? nadhani wote tuna macho na masikio, tulitenda, tulisikia na mahali pengine tuliona. Hivi NEC inapokiri kuwa kulikuwa na matatizo kadhaa katika suala zima la Uchaguzi uliopita, inakuwaje wengine wasema hapana? Ina maana wao ni zaidi ya NEC?

    Anacholalamika Dr. Slaa ni hicho. Tunaomba wale wanaotoa maoni yao waheshimu wengine hata kama huwapendi. Udakitari wa Slaa si wa kutungua kama walivyo wengine, amkwenda shule, hivyo ni vizuri tulitambue hilo hata kama hatumpendi.

    ReplyDelete
  21. Shule gani hiyo alokwenda Dr Slaa? Tupe data kuanzia degree ya kwanza alisoma nini na wapi, na pili pia alisoma nini na wapi na hiyo ya tatu alifanya utafiti wa nini na wapi mpaka akawa Daktari wa falsafa. Kama hamna majibu basi hata Mashehe wetu wa kiislam ni madokta na wao!

    ReplyDelete
  22. wewe unayewambia wenzako wanamawazo mgando wewe ya kwako ndo ukoko kabisaa!sasa hao ndugu wa vijijini uliambiwa Silaa akiwa Rais atawapeleka ikulu ? Fursa zipo badala mzitumie mbadilike na muongeze kipato chenu kalagabaho ufikiri Silaa akiwa rais atakuja kurazimisha bibi yako ahame village! unajifanya msomi kumbe akili imeganda kama ukoko wa pilau la nyanya!

    ReplyDelete
  23. Mbenga said..

    Akili ni nywele...., Lazima tutofautiane kufikiri na kama si Dr. Slaa na chadema kutoamua kupinga matokeo ya urais pia kutomtambua, tusinge kuwa tunahemkwa kimawazo kama tufanyavyo sasa, angalia hakuna mjadala kwa nini vyama vingine vimekubali yaishe. Big up Chadema, mnawafanya watanzania waendelee kuitaja nchi yao kwa mitazamo mbalimbali

    ReplyDelete
  24. Jamani mtasema na mkimaliza mtanyamaza na CCM ndio inaongoza nchi ! tuliwaona wajinga wazanzibari pale walipotaka kuandama na hatimae kuuliwa na serikali...sasa hapa bila ya kujidhatiti basi hili la kutomtambua JK ni kama ya CUF miaka ya mwanzo pale Zanzibar ambayo haikuzalisha manufaa yoyote.sasa kiasi fulani wamebanwa Zanzibar ndio ikaja hiyo serikali ya mseto.Kazi ipo na njia sio fupi ila tusikate tamaa .....ipo siku

    ReplyDelete