20 February 2013

Lowassa awashukia mahasimu wake kisiasaNa Moses Mabula, Nzega

WAZIRI Mkuu mstaafu Bw. Edward Lowassa, amewapiga vijembe mahasimu wake kisiasa wanaodai anatumia makanisa kuusaka uras katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.


Alisema watu wanoeneza uvumi huo ambao hauna ukweli wowote, wanamjenga katika jamii kiimani na kisiasa pamoja na kulaani vikali mauaji ya Padri Evaristus Mushi, yaliyotokea juzi Zanzibar baada ya kupigwa risasi tatu kichwani na watu wasiofahamika.

Bw. Lowasa aliyasema hayo jana mjini Nzega, mkoani Tabora, katika harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo la hosteli ya Idara
ya Wanawake na Watoto kwenye Kanisa la Moravian, Jimbo
Kuu la Tabora, Kanda ya Magharibi.

Katika harambee hiyo, zaidi ya sh. milioni 100 zilichangwa ambapo Bw. Lowassa pekee, alichangia sh. milioni 10 taslimu.

Akizungumza baada ya harambee hiyo, Bw. Lowassa alisema Watanzania wote wamekuwa na umoja kwa muda mrefu bila kubaguana kwa misingi ya dini wala kabila hivyo aliwaomba
Waislamu na Wakristo nchini, kuwa kitu kimoja, kuitetea
na kuilinda amani iliyopo.

Aliwataka viongozi wa dini nchini, kuisaidia Serikali ili kurejesha upendo unaotaka kupotea kati ya Waislamu na Wakristo.

Bw. Lowassa alisema yeye si tajiri wa pesa kama inavyosemwa mitaani bali utajiri wake ni wa watu wanaotambua juhudi zake
za kuchuchea maendeleo ya jamii.

Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa kanisa hilo Kanda ya Magharibi, Issack Nicodemo, alisema Waislamu na Wakristo
ni ndugu kutokana na mahusiano waliyonayo muda mrefu.

Alisema vitendo vya mauaji vinavyoendelea nchini kwa viongozi
wa dini vinapaswa kulaaniwa na kuongeza kuwa, upendo, amani ndio njia pekee ambayo itaendeleza umoja uliopo.

4 comments:

 1. Nazani Baba Askofu hauzunguki mitaani na kusiliza yanayo endelea. Kwa taarifa yako wanasema watahakikisha wametekeleza azma yao. Na hapa tusifumbe macho bali waumini wapewe tahadhari juu ya usalama wao na mali zao. Hapa tukumbuke wimbo unaotuweka pamoja *Twendeni Askari watu wa Mungu* katika tenzi za rohoni. Waumini wapewe ukweli kuwa hili ni janga na linakuja na wajiandae kwa lolote. Kama nikumuomba Mungu watu tunaomba ila pia tujipange kwa lolote. Pia kumbuka tatizo halipo kwa wakristo bali lipo kwa hao wneye kuujua ukweli wa Allah kuliko wanaoujua ukweli wa Mungu. Tusifichane mwenye tatizo akamwate aazibiwe tu.

  ReplyDelete
 2. lowasa akasomee u[padri halafu kituo chake cha kazi kiwe zanzibar!

  ReplyDelete
 3. NASHANGAA JINSI WATU WANAVYOOGOPA KUSEMA UKWELI
  TUSIPOSEMA UKWELI KUHUSU JAMBO HILI NI HATARI.WAISLAMU NDIO WANAORATIBU VURUGU HIZI MAANA NI NIA YAO KUONA UKRISTO UNAONDOLEWA TZ JAMBO AMBALO NI NDOTO ZA MCHANA.WAMEKUWA NA MKAKATI HUO MUDA MREFU.MUNGU AWASAIDIE ILI WAPATE UFAHAMU WA KUJUA KWAMBA NAO WANAMWILI PIA HAWAWEZI KUUMALIZA UKRISTO MAANA MUNGU NDIYE ALIYEUWEKA NA YEYOTE ANAYEJARIBU KUSHINDA NA KUSUDI LA MUNGU ATAONDOKA YEYE,HATA PAULO ALIKUWA KINYUME NA KANISA ILA ALISHINDWA

  ReplyDelete
 4. KUFANYA HARAMBEE HUKO TABORA SI KUMDHALILISHA SAMWELI SITTA ANAYEJISIFIA KUWA YEYE NDIYE ANAYEFAA URAS

  ReplyDelete