18 February 2013

Ikulu, Polisi wakanusha taarifa za Wassira, IGP kutimuliwa


Na Mwandishi Wetu

KURUGENZI ya Mawasiliano ya Rais (DPC), Ikulu pamoja na Jeshi la Polisi nchini, wamekanusha habari iliyoandikwa katika Gazeti la TanzaniaDaima, ukurasa wa kwanza toleo la jana inayosema “Wassira, Mwema, watimuliwa Gaita”.


Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na DPC, imesema habari hiyo si ya kweli iliyolenga kuwadhalilisha Maofisa wa Serikali na kufafanua kuwa, Bw. Stephen Wassira, si Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu bali ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu.

“Tangu Februari 14, 2013, kama inavyodaiwa na gazeti hili, Bw. Wassira alikuwa akiandamana na Rais Jakaya Kikwete katika ziara za mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

“Alhamisi siku ambayo inadaiwa kuwa “alitimuliwa Geita”, Bw. Wassira alikuwa na Rais Kikwete katika mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi, Mhashamu Amedeus
Msarikie ambayo yalifanyika katika Kanisa Kuu la Kristo
Mfalme mjini humo,” ilisema taarifa hiyo.

Iliongeza kuwa, Februari 15, 2013, Bw. Wassira alikuwa mjini Arusha katika mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati, Dkt. Thomas Lazier yaliyofanyika Kanisa Kuu ya KKKT.

Kurugenzi hiyo ilisema Februari 16, 2013, Bw. Wassira na Rais Kikwete walirejea Dar es Salaam na kwenda moja kwa moja nyumbani kwake Masaki kushiriki msiba wa kaka yake.

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi nchini, limesema habari iliyoandikwa na gazeti hilo, si ya kweli kwamba IGP Mwema, alikwenda 888888nalo limekanusha


JESHI la Polisi nchini, limekanusha taarifa hiyo na kudai si ya kweli badala yake ni tabia ya makusudi ya mwandishi husika kutaka kuipotosha jamii.

Ukweli IGP hakuwa Geita alikuwa mjini Dodoma kikazi kutokana na opotoshaji huio jarada la uchunguzi limefunguliwa na upelelezi ukikamilika mwandishi huyo atafikishwa mahakamani.

Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa wote wenye tabia ya kuandika habari za uongo zenye mrengo wa kuchochea vurugu na fujo nchini kuacha tabia hiyo mara moja.

Jeshi la Polisi litaendelea kuwachukulia hatua watu wote wenye tabia kama hiyo. Advera Senso msemaji wa Jeshi la Polisi nchini.

1 comment:

  1. Polisi imekuwa ndio plaintful, prosecution na mahakama, kuna haki hapo au mis-reporting.Truly, we still have long way to go if the law says so. Watu wanataka tuwe kama prior 1992 na given hali yetu ya elimu kazi ipo.

    ReplyDelete