05 February 2013

Auawa akidaiwa kuvunja, kuiba gunia la mpunga



Na Lilian Justice, Morogoro

MKAZI wa Mvomero, mkoani Morogoro, Muksin Zege (55), ameuawa na wananchi wenye hasira akituhumiwa kuvunja
nyumba na kuiba gunia mola la mpunga katika Kijiji cha
Hembeti, Kitongoji cha Hembeti, wilayani humo.


Kamanda wa Polisi mkoani humo, Faustine Shilogile, alisema
tukio hilo limetokea Februari mosi mwaka huu, saa tatu asubuhi,
ambapo marehemu alipigwa na kuchomwa moto baada ya kuvunja
nyumba ya Bw. Msafiri Omari (24), mkazi wa Wilaya hiyo.

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi mkoani humo, linamshikilia Bw. Yohana Obed (18), mkazi wa Mafisa kwa kosa la kumbaka mtoto
wa miaka 14 na kumpa ujauzito.

Kamanda Shiloghile alisema, kuwa tukio hilo limetokea Februari
3 mwaka huu, saa 11 jioni katika eneo ya Mafisa, mkoani humo.

Alisema jeshi hilo linamshikilia mtuhumiwa na atafikishwa mahakamani baada ya taratibu za kisheria kukamilika.


No comments:

Post a Comment