18 February 2013
Afa baada ya kugongwa na nyoka
Na Omary Mngindo, Kisarawe
MKAZI wa Kijiji cha Vikumburu Kata ya Vikumburu wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Bw. Shomari Kibange amefariki dunia baada ya kugongwa na nyoka.
Hayo yametanabaishwa na Diwani wa Kata ya hiyo Bw. Juma Dihomba wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini hapa mabapo amesema siku ya tukio marehemu alikuwa anaelekea katika shuhuli zake za kila siku.
Bw. Dihomba alisema marehemu ambaye shughuli zake kuu ni za ukataji mkaa alikumbana na tukio hilo la kugongwa na nyoka ambapo alipoteza maisha kabla ya kuanza kupatiwa matibabu.
“Marehemu ambaye ameacha mke na watoto alikumbana na janga hilo akiwa anaelekea kwenye shughuli zake ambapo hata hivyo juhudi za kutaka kuokoa maisha yake hazikuweza kuzaa matunda kwani alifariki kabla ya kupatiwa uduma yeyote,” alisema.
Aidha Diwani huyo ameongeza kuwa matukio aina hiyo yamekuwa yakitokea hali inayosababishwa na Kata hiyo kuwa jirani na mbuga ya Seluu iliyopo wilaya ya Rufiji ambapo nyoka wamekuwa wengi.
“Mwaka 2001 kuna mkazi mwingine Bw. Salum Ludewa amefariki kwa kugongwa na nyoka hali inayowafanya wakazi kuishi kwa mashaka makubwa kufuatia matukio hayo,” alisema.
Aidha amewaomba wakazi ndani ya Kata hiyo kutumia viatu virefu vya plastiki maarufu ganibuti ikiwa ni mikakati ya kudhibiti matukio aina
hiyo.
"Nawashauri wakazi wenzangu wa Kata ya Vikumburu tununue viatu virefu vya plasitiki maarufu ganibuti ili kudhibiti matukio haya ambayo yamekuwa yanatunyika raha," alimalizia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment