18 February 2013
Pinda kukutana na viongozi wa dini leo
Na Faida Muyomba, Geita
WAZIRI Mkuu Bw. Mizengo Pinda,leo(Jumamosi) anatarajiwa kufanya ziara ya siku mbili Mkoani Geita ,yenye lengo la kufanya mazungumzo na viongozi wa madhehebu ya dini yaliyomo mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Bw. Magalula Said Magalula,aliyasema hayo ofisini kwake,katika mazungumzo na waandishi wa habari mjini hapa jana.
''Mheshimiwa Waziri Mkuu atakuwa hapa kuanzia kesho(leo) kwa ziara ya siku mbili anatarajiwa kuondoka kesho kutwa Jumapili,lengo la ziara hii ni kufanya mazungumzo na viongozi wa dini zote walioko mkoani Geita.''alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Alisema,katika mkutano huo maalumu Waziri Mkuu amewataka viongozi wote wa dini hizo watakaopewa mwaliko,wahudhurie bila kukosa kwa lengo la kutatua mgogoro ulioibuka mkoani humo kati ya waislamu na wakristu.
Katika mgogoro huo uliohusisha nani mwenye haki ya kuchinja kati ya wakristu na Waislamu,mchungaji wa kanisa la Pentekoste Assemblies of God,Mathayo Kachila(48) aliuawa huku watu wengine saba wakiwa wamejeruhiwa vibaya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment