18 February 2013

Abiria 60 wanusurika kufa MuhezaNa Steven William, Muheza

ABIRIA 60 waliokuwa wakisafiri na basi la Simba Mtoto kutoka Dar es Salaam kwenda mkoani Tanga, wamenusurika kufa baada
ya basi hilo kuacha njia na kupinduka katika eneo la Mamboleo, Wilaya ya Muheza, mkoani humo.


Akizungumza na gazeti hili, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Costantine Massawe, alisema ajali hiyo ilitokea juzi usiku.

“Basi hili aina ya Isuzu, dereva wake alitaka kulipita gari jingine gafla ilitokea gari mbele yake akaliingiza basi katika mtaro akiwa mwendo kasi,” alisema.

Aliwataja baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Yohana Kapufi, Hashimu Ibrahimu, Alfani Hassani, Rafaeli Mathew, Ester Kiyondo, Mariam Zuberi, Maua Bakari na Janeti Rafaeli ambao wamelazwa katika Hospitali Teule ya Mkoa huo.

No comments:

Post a Comment