14 January 2013

Mkandarasi soko la Mwanjelwa adaiwa kushindwa kazi


Na Esther Macha, Mbeya

UJENZI wa Mradi wa soko la wafanyabiashara wadogo unaoendelea eneo la Mwanjelwa Jijini Mbeya ,unadaiwa kukwama,baada ya mkandarasi aliyepewa zabuni ya ujenzi wa soko hilo –TANZANIA BUILDINGS WORKS-TBW kwa gharama ya  zaidi ya Bilioni 12 anadaiwa kushindwa kazi.


Kazi ya ujenzi huo wa soko imeanza kujengwa mwaka 2010 miaka miwili baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya  Kikwete kukabidhi hundi kwa halmashauri ya Jiji la Mbeya Oktoba mwaka 2008 kama mkopo kutoka Benki ya CRDB.

Hata hivyo  Mkandarasi  huyo TANZANIA BUILDINGS WORKS  alipewa  zabuni na Halmashauri ya Jiji la Mbeya,ambaye ameanza ujenzi wa soko hilo Agost 25 mwaka 2010,kwa mujibu wa mkataba wa ujenzi wa soko hilo miezi 18 .

Akizungumza  jana  mara baada ya Waziri wa  nchi  ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa serikali za mitaa  Hawa Ghasia ,Meneja  mradi wa kampuni ya ushauri ya mradi wa ujenzi wa soko la Mwanjelwa Bw.Liberate  Materu alisema pamoja na kuwa mkandarasi huyo kulipwa fedha za walipa kodi zaidi ya Bilioni 8 lakini soko hilo halijakamilika mpaka sasa .

Hata hivyo kitendo cha kutokamilika kwa ujenzi huo  kimemtia hofu Waziri Ghasia  na kusikitishwa na kusua sua kwa ujenzi wa soko hilo,linalosubiriwa na wananchi.

Aidha Soko hilo lilitakiwa likamilike ujenzi.agost 24 mwaka 2011 na mkandarasi huyo kukakabidhi jengo kwa mwajili wake Halmashauri ya Jiji la Mbeya,.

Hata hivyo ujenzi huo umekamilika kwa asimilia asilimia 68 ya  gharama zote,inadaiwa amefikia asilimia 70 na ameshindwa kumalizia asilimia 30 ya ujenzi iliyobakia.

Hata hivyo Mkuu wa MKoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro alisema serikali imetoa fedha lakini baadhi ya watu wachache wameendelea kuiangusha.

Mkurugenzi wa Halmashaurii ya Jiji la Mbeya Bw. Juma Idd  amekiri kuwa pamoja na kushindwa kazi kwa mkandarasi huyu ,lakini pia hayupo eneo la ujenzi wa soko  kwa muda mrefu sasa.


No comments:

Post a Comment