07 January 2013
JK kuzindua miradi ya ujenzi wa barabara Tabora
Na Stella Aron
RAIS Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa miradi minne ya barabara na daraja katika mkoa wa Tabora.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya habari jana Dar es Salaam na Katibu Mkuu Balozi Herbert Mrango,imesema kuwa uzinduzi wa miradi hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuhakikisha kuwa makao makuu ya mikoa yote yanaunganishwa kwa barabara za lami.
Katibu Mrango alisema kuwa miradi hiyo ni mafanikio makubwa katika sekta ya usafirishaji na itatoa chachu kubwa kwa uchumi wa mkoa wa Tabora na Taifa kwa ujumla.
"Miradi hii itasaidia sana katika kuimarisha usafiri wa barabara kati ya Tabora na mikoa ya Kigoma,Shinyanga,Singida na Dodoma," ilisema.
Alisema pamoja na shughuli nyingine, kesho rais Kikwete akiwa mkoani humo ataweka jiwe la msingi kwa ajili ya uzinduzi wa ujenzi wa daraja la Mbutu lililoko Wilayani Igunga.
Alisema keshokutwa Rais Kikwete ataweka jiwe la msingi la uzinduzi wa ujenzi wa lami wa barabara za
Nzega-Puge, Puge -Tabora, Tabora- Ndono na Tabora- Nyahua.
Katibu huyo alisema kuwa Januari 9,mwaka huu Rais ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Ndono hadi Urambo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment