16 January 2013

Dkt. Slaa awapa 'rungu' madiwani




Na Martha Fataely, Moshi

KATIKA hali isiyo ya kawaida, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa, amewahamasisha madiwani wa chama hicho Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, kumfungia nje ya ofisi Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Bi. Bernadette Kinabo.

Alisema sababu ya kufanya hivyo ni baada ya kuzuia juhudi za Baraza la Madiwani kuataka kuwalipia ada wanafunzi wa manispaa hiyo kama sehemu ya ahadi zake alizotoa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.

Dkt. Slaa aliyasema hayo juzi katika mkutano wa hadhara ambao ulifanyika katika Viwanja vya Railway, Manispaa ya Moshi na kudai kuwa, taarifa wa Meya wa Manispaa hiyo, Bw. Japhary Michael, ilidai mwaka 2011/12, baraza hilo lilitenga sh.
milioni 196 na mwaka 2012/13, sh. milioni 216 kwa ajili ya
kulipa ada wanafunzi lakini Bi. Kinabo amekaa kiziidhinisha.

Alisema hawezi kuvumilia kuona baadhi ya viongozi wamejibebesha dhamana za vyama vya siasa wakati ni watendaji wa Serikali na kusisitiza kuwa, Bi. Kinabo hana mamlaka ya kukataa jambo ambalo limeazimiwa na madiwani hivyo kama atakuwa na kikwazo, wamfungie nje ya ofisi yake.

Dkt. Slaa pia aliwaoneshea kidole baadhi ya viongozi akiwemo Mkuu wa Wilaya na Mkoa akidai wanaingilia shughuli za Baraza
la Madiwani pale linapoonekana kutekeleza ilani ya CHADEMA.

Alisema viongozi hao ni washauri katika baraza hilo lakini hawana mamlaka kikatiba kwani baraza ni sawa na Bunge hivyo wasimamie maamuzi yao wasikubali kuyumbishwa.

2 comments:

  1. MKURUGENZI NI MTAALAMU MADIWANI WENGINE DARASA LA SABA HAISHANGAZI RASILIMALIWATU TANZANIA KUSHUTUMIWA KUWA ASILIMIA 93 YA WAKAZI WAKE HUTEGEMEA USHIRIKINA,WAKATI KENYA NI 27 ASLIMIA NA UGANDA ASILIMIA 29 WATU WA AINA HIYO HATA WAKIAMBIWA WAJILIPUE NA PETROLI WANATEKELEZA HAIINGII AKILINI WATANZANIA WAKIONGOZA KWA USHIRIKINA DUNIANI KENYA WANAONGOZA KWA ICT AFRIKA

    ReplyDelete
    Replies
    1. ni kweli mkurugenzi ni mtaalamu lakini akikataa atoe sababu,

      Delete