03 December 2012

Wananchi watakiwa kununua kinga'muzi

Na Heri Shaaban

WANANCHI wametakiwa kununua king'amuzi kwa ajili ya kutumia katika televisheni zao, pamoja na garantii  isiyopungua ya mwaka mmoja.


Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Masuala ya Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Habbi Gunze wakati wa kutoa taarifa kwa umma  kuhusiana na uzinduzi wa tangazo (JINGLE)na wimbo wa kuhamasisha uhamaji wa Teknolojia ya utangazaji kutoka analojia kwenda dijitali.

Gunze alisema kuwa kila mtanzania ambaye atanunua kingamuzi hicho lazima apewe lisiti pamoja na garantii kwa ajili ya ubora wa chombo hicho alichonunua.

"Nawaomba watanzania wote wanunue kingamuzi ili tuweze kuingia katika mfumo wa digitali tuweze kuangalia vituo vingi vya  televisheni tuachane na kutumia teknorojia ya utangazaji ya analojia."alisema Gunze.




Alisema kuwa kuanzia leo Desemba Mosi tumetoa wimbo  wa kuhamasisha umma kujiandaa na mabadiliko ya  digitali wimbo unaitwa Wakati wa Digitali Tanzania ambao ndio utatumika katika vituo vya televisheni na radio.

Gunze alisema kuwa tangazo hilo la wimbo vyote vinalenga katika kuelimisha kukumbusha na kuhamasisha umma umuhimu na faida za teknorojiampya ya digitali.


Pia aliwataka wananchi wote wasitupe televisheni zao za zamani kwa kuwa zitaendelea kutumika kwa kuunganishwa na king'amuzi  mara baada kuzimwa kwa mitambo ya analojia desemba 31 mwaka huu kwa mujibu wa kanuni za mamlaka ya mawasiliano kuhusu mifumo ya digitali za mwaka 2011.

Aliwataka watanzania wote kununua vingamuzi kwa mawakala wote waliosajiliwa na TCRA na wapate garantii ya vingamuzi hivyo.

No comments:

Post a Comment