03 December 2012

DC Mbulu asifiwa na Wahadzabe

Na Mary Margwe,Mbulu
 
WANANCHI wa jamii ya wahadzabe wanaoishi katika bonde la Yaeda Wilayani Mbulu Mkoani Manyara wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Mbulu,Bw.Anatory Choya kwa kukaa nao chini kwenye vumbi na kusikiliza kero zao.


kwa kuwa mzalendo na kuamua kujishusha kukaa nao chini kwenye vumbi na kusikiliza kero zao, licha ya kuwa yeye ni kiongozi mkubwa,kitendo ambacho kimeombwa kuigwa na viongozi wengine hapa nchini.

Jamii hiyo ya wahadzabe ambao huishi kwa kutegemea kula mizizi,matunda,asali, nyama na ubuyu, waliyasema hayo jana wakati mkuu huyo aliipowatembelea jamii hiyo mara baada ya Serikali kutoa tani zipatazo 201.8 za chakula cha msaada kwa Wilaya hiyoambapo jamii hiyo alifanikiwa kupata tani 20.2 za mahindi na kugawiwa bure kwa kulingana na hali ya uchumi waliyonayo.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Mbulu,Bw.Choya amepewa pongezi hizo mara baada kuonekana kuwa tofauti kabisa na viongozi mbali mbali wa ngazi za juu hapa nchini, anayeweza kujishusha na kukaa chini na jamii na kuweza kusilikiza kero za wananchi ukilinganisha na baadhi ya viongozi wengine wanaopenda kujikweza machoni pa jamii.

“Huyu ni kiongozi wa kwanza kabisa kwetu na hata kwa sehemu nyingine hapa nchini tuliyemuona anakaa chini kabisa kwenye vumbi na sisi,tulipomuona anaelekea kuja kwetu tulipokaa sisi chini tulitaka kukimbia kabisa akatuambia hapana msikimbie  najua nyie ni wazee ambao hamna uwezo wa kuuliza maswali machoni mwa watu,na hivyo nimekuja kuwasikiliza tukae chini tu wote wala msiniogope mimi ni sawa na nyie kabisa ,kasoyo yangu kwenu ni nyadhifa tu na si vinginevyo”alisemammoja wa jamii hiyo anayetambulika kwa jina la  MzeeTherathini Nkwemo.

Wananchi hao walisema iwapo viongozi wangeweza kujishusha  kama Mkuu huyo wa Wilaya ya Mbulu basi Tanzania ingekua na almasi  ya viongozi, ambapo walidai kuwa viongozi wengi wamekua na tabia ya kujikweza hali inayowapelekea jamii  mbalimbali kushindwa hata kuwaingia na kuelezea kero zao.

Aidha kufuatia kitendo cha mkuu huyo wananchi hao wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kuhakikisha kuwa iwapo kuwa viongozi anaowaangalia kwa jicho moja moja  basi wamemtaka kumuangalia Mkuu huyo Choya kwa macho mawili  mawili kwani ameonyesha kitendo ambacho ni cha pekee kinachotakiwa kuigwa na viongozi wengine hapa nchini.

Aidha walifafanua kuwa ni jambo la furaha kwao hususani kwa jamii hiyo inayoonekana kuwa na hali ya chini kiuchumi ukilinganisha na jamii zingine hapa nchini kumpata kiongozi anayekwenda na mazingira ya eneo husika  ukilinganisha na viongozi wengine waliowahi kutembelea bonde hilo la yaedachini.

“Mkuu huyu hajawahi kabisa kuja huku kwetu na kutuvamilia hii inayokaa shingoni na kuja hadi tumboni( tai) yeye huwa anakuja kwetu hadi kukagua chakula tunachopika na kula na familia zetu hali ambayo sisi inatupa faraja sana,jamami sisi hatuna cha kumpa isipokua mungu mwenyeweatajua nini ampe kazi yetu sisi ni kumuombeakwa mungu azidi kumpa afya njema  ikiwezekana aongoze  hadi atakaposema yeye mwenyewe basi” alisema mmoja wa mama wa jamii hiyo.
Hata hivyo walifafanua kuwa Mkuu huyo amekua mkombozi kwao kwa kile walichodai kuwa ameweza kuwasaidia kata kwa msaada wake binafsi nje ya serikali kwa jamii hiyo hususani wakati wa kipindi cha sensa ya mwaka huu,ambapo wamedai alifanya zira mara kadhaa kwenda kuwatembelea na hata kutoa machazi pale ambapo ameona hali imekua mbaya zaidi kwa jamii hiyo.

Akiongea nje ya eneo hilo mkuu huyo alisema kuwa  yeye ni kiongozi wa jamii hiyo ya Wilaya hiyo, hivyo  ni jukumu lake kuhakikisha kuwa jamii yote anaisikiliza ikiwa ni pamoja na kusikiliza lika mbalimbali kama watoto, vijana, na wazee ili kujua namna ya kuwasaidia 

“Iwapo Rais wetu mwenyewe ni mtu mzalendo asiyependa kujikweza,mimi ni nani ,Mimi binafsi sioni sababu ya kujikweza kwanza wala sio tabia yangu kabisa tokea nilipokua mbunge ,mimi nina utamaduni wangu huu huu wala sijabadilika kabisa,nafasi ya kunipandisha si yangu mimi bali ni ya mungu pekee ndiye mwenye maamuzi ya kukushusha ama kukupandisha” alisema Choya ambaye ni Mkuu huyo wa Wilaya ya Mbulu.

Aidha alisema licha ya kuwa wakati wa mikutano kuna nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali lakini bado baadhi ya wananchi hususani wazee wamekua wakionekana kuto kupewa nafasi ama kuogopa kuuliza maswali mbalimbali, na ndio maana mimi nikipata nafasi huwa nakaa nao ili kuwasikiliza na watakwambia mengi na mazito kuliko michango mbalimbali inayotolewa na vijana.

"Hata nyie waandishi wa habari nadhani pia mna taratinu na kanuni zenu mlizojifunza mkiwa vyuoni zinazowapelekea kufuata ili kuenenda sambamba na mazingira ya sehemu unayotaka kupata habari yako, babi nami ndivyo nilivyo kabisa  au unanionaje? alihoji mkuu huyo.


No comments:

Post a Comment