03 December 2012
Mbunge Mtemvu aombwa kusimamia mradi
Na Mariam Mziwanda
WANANCHI wa Wilaya ya Temeke wamemuomba Mbunge wa jimbo la Temeke Bw. Abbas Mtemvu kuhakikisha anakuwa mlezi na kusimamia ipasavyo mradi wa Tambua haki yako ili uweze kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Akizungumza katika mkutano wa kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo jana Mratibu wa mradi Bw. Rashid Seif alisema kuwa endapo mradi huo utasimamiwa ipasavyo na Mbunge wa jimbo la Temeke utafanikiwa katika malengo yaliyokusudiwa ikiwemo kuwajengea uwezo wananchi hao.
"Leo tunapitia taarifa ya utekelezaji wa mradi wa mwananchi tambua haki yako unaotekelezwa katika mitaa 13 ya kata nne za Wilaya ya Temeke matarajio yetu mbunge wa jimbo hili atazipokea jitihada za wananchi wake na kuwa mlezi wa mradi huu hasa katika kusimamia mafanikio yake,"alisema
Alisema kuwa mradi huo umetokana na utafiti wa changamoto za utekelezaji wa utawala bora na uwajibikaji katika ngazi za mitaa kwa mitaa ipatayo kumi na tatu na kata nne za manispaa hiyo.
Bw. Seif alisema kuwa mradi huo ambao ulianzishwa Septemba 2012 umewawezesha wajumbe wake katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wakiwemo wenyeviti wa mitaa 13,wajumbe wa Serikali za mitaa zipatazo 76 na wawakilishi wa wananchi 52 katika awamu tatu na kisha kualika wawakilishi 66 kutoka sekta mbalimbali wilayani humo.
Kufuatia tathimini hiyo ya utekelezaji washiriki hao wamefanikiwa kuandaa mpango wa utekelezaji utakaokabili changamoto mbalimbali za manispaa hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment