03 December 2012
Vodacom yakabidhi vifaa kupambana na ukimwi
Na Darlin Said
KAMPUNI ya Simu za mkononi Vodacom imekabidhi vifaa vya kisasa vyenye thamani ya shilingi milioni.98 kwa Taasisi ya Elizabeth (EGPAF)vitakavyosaidia kutoa huduma kwenye mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa watoto wachanga.
Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa ni mashine 43 zijulikanazo kwa jina la SMS Pinter zinazotumia teknolojia ya hali ya juu kwa kutuma ujumbe mfupi katika utendaji wake.
Akikabidhi mashine hizo kwa EGPAF Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule alisema mashine hizo zitawawezesha akina mama na wataalamu wa afya nchini kupata majibu ya watoto kwa haraka kupitia ujumbe mfupi.
Hivyo vifaa hivyo vinatarajia kuongeza ufanisi katika sekta ya afya pamoja na kuboresha huduma hususani katika eneo la vita dhidi ya maambukizi mapya ya UKIMWI na njia za kukabiliana nayo.
Naye Mganga Mkuu EGPAF Dkt.Chrispine Kimario alisema kuwepo kwa mashine hizo zitasaidia kupatikana kwa muda mfupi ikilinganishwa na njia nyingine ambazo zinachukua muda mrefu.
Alisema EGPAF itatoa mafunzo kwa wataalamu wa afya vijijini juu ya matumizi ya vifaa hivyo pamoja na kuvisambaza kwenye vituo vya afya na hospitali za mkoa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment