03 December 2012

'Tanzania miongozi mwa nchi zisizofikia milenia 2015'



Na Rehema Mohamed

TANZANIA ni miongoni mwa nchi ambazo zinaelekea kutofikia melengo ya milenia yanayoishia mwaka 2015 hasa katika suala la kupunguza umaskini wa mahitaji muhimu kwa wananchi wake.

Hayo yameelezwa jana na Mtafiti Mshiriki wa Taasisi za Uchumi na Jamii (ESRF)Dkt. Osward Mashindano wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu majadiliano ya mchakato wa maendeleo unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Dkt.Mashindao alitaja eneo lingine ambalo linaonekana kutofikiwa ni kupunguza vifo vya watoto wachanga, ambapo ifikapo mwaka 2015 inatakiwa vipungue hadi asilimia 38.

Dkt.Mashindao alisema kutokana na hali hiyo nchi zote zilizoridhia kutimiza malengo ya milenia ikiwemo Tanzania zimetakiwa kufanya majadiliano na wadau mbalimbali ili kuona namna ya kufikia malengo hayo.

Alisema kwa hapa nchini,ESRF imeteuliwa kusimamia majadiliano hayo ambayo yatahusisha watu kutoka serikali za mitaa,asasi za kiraia ,wanawake wadogo na wazee.

Alisema kuwa majadiliano hayo yatafanyika katika kanda saba nchi nzima ambazo ni kanda ya Kaskazini katika Mkoa wa Arusha,Mashariki Mkoa wa Morogoro,Kanda ya Ziwa Mkoa wa Mwanza,Kanda ya Kati Dodoma,Magharibi Shinyanga,Kusini Mtwara na Nyanda za Juu Kusini Mkoa wa Mbeya, ambapo katika kanda itajumuisha wajumbe 30.

"Tayari tumeshafanya maandalizi na majadiliano hayo yatafanyika Desemba 4 mwaka huu,wadau tuliowateua kuja kujadili ni wale wasiopata fursa za kutoa madukuduku yao jukwaani mfano wale walio na kipato cha chini,"alisema.

No comments:

Post a Comment