03 December 2012
Nimefuraishwa na kasi ya ujenzi-RC
Na Moses Mabula, Tabora
SERIKALI imefuraishwa na kasi ya ujenzi wa barabara ya kurukia ndege yenye kiwango cha lami katika uwanja wa ndege wa Mkoa wa Tabora.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa huo, Bi Fatuma Mwassa wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo wa barabara ya kurukia ndege, uliopo mjini Tabora.
Alisema kwamba Serikali imerizishwa na kasi ya ujenzi huo, lakini huku akimtaka mkandarasi anayejenda barabara hiyo, kuongeza kasi zaidi ili ndege zianze kutua tena na hatimaye kupunguza tatizo la usafiri wa ndege kwa abiria Tabora.
Mkuu huyo mkoa alisema kuwa iwapo uwanja huo utakamilika ujenzi wake, mkoa wa Tabora utakuwa umeondokana na adha ya usafiri wa ndege kwa wananchi wake.
Alisema kwamba, huduma ya usafiri wa ndege mkoani humo, umesitishwa takribani mwaka mmoja kutokana na kupisha ujenzi wa barabara ya kurukia ndege
kwa kiwango cha lami.
Alisema kuwa kwa mujibu wa mkandarasi wa ujenzi huo, nikwamba utakamilika ujenzi wake ifikapo mwezi Januari mwakani, ambapo huku akiuagiza uongozi wa mamlaka ya uwanja ndege mkoani humo kuimarisha ulinzi katika uwanja huo.
Bi. Mwassa amesisitiza kuwa Serikali hatasita wala kumuonea haya mtu yoyote au kumchukulia hatua za kisheria atakayebainika kuharibu au kupitisha
mifugo yake katika miondo mbinu ya barabara hiyo ya kurukia ndege.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment