21 December 2012
Hoteli ya Giraffe Ocean View nayo yafungiwa
Na Waandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa, jana ameendelea na ziara ya kikazi kukagua hali
ya mazingira katika hoteli zilizopo pembezoni mwa fukwe za
Bahari ya Hindi, jijini Dar es Salaam.
Dkt. Huvisa alifanya ziara hiyo katika Hoteli ya Giraffe Ocean View, lakini alishangaa kuona maagizo aliyotoa Naibu Waziri Bw. Charles Kitwanga kwa uongozi wa hoteli hiyo mapema mwezi huu ya kurekebisha mfumo wa majitaka na kuweka fukwe katika hali ya usafi hayajazingatiwa.
Kutokana na hali hiyo, Dkt. Huvisa aliamua kuifungia hoteli hiyo hadi itakapotimiza masharti yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria
ya mazingira ya mwaka 2004.
“Naifunga hoteli hii hadi itakapotimiza masharti ya hifadhi ya
mazingira,” alisema Dkt. Huvisa.
Katika hatua nyingine, aliupongeza uongozi wa Hoteli ya Beach Comber kwa kuwa na mkakati endelevu wa mfumo wa maji taka
na hifadhi ya fukwe kwa ujumla.
Alisema ziara anzofanya ni mkakati endelevu wa kukagua hoteli zote pamoja na viwanda kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004, hoteli na viwanda vyote vilivyoanzishwa kabla ya matumizi ya sheria hiyo, vinatakiwa kufanya ukaguzi wa mazingira na kufanya tathmini ya athari za mazingira (Environmental Impact Assessment).
Katika ziara ya siku mbili iliyofanywa na Dkt. Huvisa pamoja na Naibu wake Bw. Kitwanga, hatua kali zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kuifungia Hoteli ya Double Tree hadi itakapotimiza
masharti waliyopewa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment