03 December 2012
Azam Marine kutoa usafiri B'moyo-Dar miundombinu ikikamilika
Na Kassim Mahege
KAMPUNI ya Azam Marine inayojishughulisha na usafirishaji wa abiria na mizigo kwa njia ya Boti,kutoka Dar es salaam,Unguja na Pemba imesema kuwa ipo tayari kupeleka boti kutoka Bagamoyo kuja Dar es salaam,iwapo Serikali itajipanga na kutengeneza miundo mbinu.
Akizungumza na gazeti hili jana Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, Bw.Hossein Mohamed Said alisema Serikali inatakiwa ijipange kwa kutengeneza miundombinu halafu baada ya hapo sio Azam tu isipokuwa hata kampuni nyingine zitakuja kuwekeza huko.
“Kwanza kabisa serikali wajipange,watengeneze miundombinu kwanza halafu baada ya hapo sio sisi tu bali hata makampuni mengine yatakuja kuwekeza .”alisema Bw.Said.
Alisema,serikali inatakiwa isome hali halisi ya mtanzania wa hali ya chini na kuongeza kuwa wasikurupuke,kwa kufanya hivyo wawekezaji nao watakuwa pamoja katika suala hilo.
Akibainisha kuhusiana na hali ngumu ya maisha,alisema,katika nchi yetu kuna matabaka matatu,tabaka la juu ambao ni matajiri ambapo wanaweza kuamuwa hata kusafiri kwa helkopta kutoka Bagamoyo hadi Dar es salaam,tabaka la kati ni wale ambao wanaweza kusafiri kwa kutumia magari yao na tabaka la tatu ni watanzania masikini na kuongeza kuwa tabaka hili ndio tabaka lenye wananchi wengi kuliko matabaka yote.alisema Bw.Said
Alitolea mfano kuwa nauli kutoka Bagamoyo hadi Dar es salaam ni shilingi 1800,kama tutapeleka Boti tunaweza kuchaji shilingi 5000, je mwananchi gani ataacha kupanda Gari ambayo nauli yake rahisi na kupanda Boti?alihoji Bw.Said.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment