19 November 2012

PADRE APIGWA RISASI KANISANI

Na Eliasa Ally, Iringa
November 16, 2012

Watu sita wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za bunduki na mapanga,
wamemvamia ndani ya kanisa majira ya usiku katika Paroko wa parokia ya Isimani
katika jimbo la Isimani Halmashauri ya Iringa Vijijini Padre Angelo Burgio (60) na
kumpiga risasi ubavu wa kushoto ambapo padre msaidizi wake Padre Helman Myala (36)
wamemcharanga kwa mapanga kichwani ambapo majambazi hao katika hatua hiyo majambazi
hao wameiba fedha za kanisa hilo milioni 3.5 na dola za kimarekani 100 na kukimbia.


Akizungumzia kuvamiwa kwake leo, Padre Angelo ambaye kwa sasa amelazwa katika
Hospitali ya mkoa wa Iringa katika wodi namba Nane, alisema kuwa majambazi hao
walivunja mlango wa geti la kuingilia mapadre baada ya umeme wa jenereta kuzimwa na
ndipo walipoingia ndani na kuanza kuwapatia kipigo msaidizi wake kwa kumkata kwa
mapanga wakimtaka awaoneshe paroko aliko.

Padre Angelo alisema kuwa majambazi hao walivaa mavazi ya kufunika uso mzima na
kuziba nyuso zao ambazo hazikuonekana hali ambayo ilisababisha kutowatambua ambapo
kati ya majambazi hao mmoja alikuwa na bunduki na wengine walikuwa na mapanga
mikononi.

"Walianza kumkata kwa mapanga Padre Helman Myala huku wakimtaka awaoneshe chumba
ambacho nilikuwa nimelala mimi, baada ya padre Helman kuona anaendelea kuumizwa kwa
kukatwa na mapanga ndipo alipowaonesha chumba changu nilisikia makelele na nikataka
kukimbia ndipo walinipiga kwa risasi kwenye ubavuni na kuchukua fedha hizo",
alifafanua Padre Angelo Burgio.

Aliongeza kuwa baada ya kupigwa risasi aliangua chini hali ambayo majambazi hao
walijua amekufa na baada ya kutekeleza azma yao ya kuiba fedha majambazi hao
waliondoka katika eneo la parokia yake baada ya kuwaona wananchi wanakuja baada ya
kusikia mlio ya risasi na makelele ya kuomba msaada katika parokia hiyo.

Baadhi ya watawa wa kanisa katoliki wakizungumzia kuvamiwa kwa mapadre hao, Bro.
Augustine Kagine alisema kuwa sakata la majambazi kuzivamia misheni za kanisa
katoliki katika jimbo la Iringa ambapo jana usiku majambazi hao walivamia kanisa la
jimbo katoliki la Iringa na kupora laki tano na wngine kuvamia parokia ya Isimani
ambapo hali hizo zinatia mashaka na kuitaka serikali ichukue hatua za kuyafuatilia
matukio hayo kwa kuwa yanaleta wasiwasi kwa wananchi na waumini mbalimbali wa kanisa
hilo.

Bro. Augustine Kagine aliongeza kuwa kwa mfululizo parokia tatu katika jimbo
katoliki la Iringa zimevamiwa  ambapo alizitaja kuwa katika parokia ya Nyololo
wilayani Mufindi majambazi walivamia misheni hiyo hao majambazi hao hawkaufanikiwa
kuiba chochote na baada ya uvamizi huo majambazi hao waliondoka na kukimbia na
kuwaacha wananchi kuwa na hofu na mashaka makubwa zaidi.

Diwani wa Kata ya Kihologota tarafa Isimani Bw, Costantino Kihwele CCM katika
Halmashauri ya wilaya ya Iringa Vijijini alisema kuwa padre Angelo ni msaada mkubwa
kwa wananchi wa Isimani ambapo kwa sasa anafadhilia mradi wa maji wenye thamani ya
shilingi bilioni 4  ambapo pia anawasaidia watoto yatima kuwasomesha kwa kuwalipia
ada wanaotoka katika tarafa nzima ya Isimani.

 Diwani Costantino Kihwele ameitaka serikali kuhakikisha inawasaka majambazi hao na
kuwafikisha mbele ya mkono wa sherika kutokana na hali hiyo inaweza kusbabisha Padre
Angelo kusitisha misaada yake ambayo anaitoa kwa wananchi na kurudi kwao Italia
kutokana na kwa sasa kukosekana kwa amani ndani ya nchi kwa kuwavamia mapadre
makanisani mwao jambo ambalo mkoa wa Iringa halijawahi kutokea.

Kamanda wa Jeshi la Polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamhanda alithibitisha kutokea
kwa tukio la kuvamiwa kwa misheni mbili za kanisa Katoliki ambapo katika kanisa kuu
la jimbo Katoliki majambazi hao usiku wa kuamukia  jana walivamia na kupora laki
tano ambapo katika kanisa la parokia ya Isimani majambazi wengine sita walivamia na
kumpiga risasi padre Angelo Burgio na kumjeruhi msaidizi wake kwa kumkatakata kwa
mapanga.

"Majambazi wamemvamia November 15 majira ya saa 4:30 za usiku katika kijiji cha
Lwang'a Isimani na kupora fedha jumla ya shilingi milioni 3.5 na dola za Kimarekani
zaidi ya 100 na pia siku hiyo na katika masaa hayohayo majambazi wengine walivamia
kanisa katoliki la Kihesa jimboni na kupora shilingi laki tano baada ya kuvunja
mlango na kumjeruhi mlinzi na majambazi hao bado wanaendelea kutafutwa", alisema
Kamanda Michael Kamhanda.

No comments:

Post a Comment