29 November 2012

Hamad Rashid akwaa kisiki mahakamani,Pia apata msiba wa mkewe

Na Rehema Mohamed

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana ailishindwa kutoa uwamuzi wa kesi ya Mbunge wa Wawi Zanzibar, Bw.Hamadi Rashid na wenzake 10 dhidi ya Wadhamini wa CUF, kutokana na uwamuzi huo kutokamilika kuandaliwa.


Jaji Agustine Shangwa anayesikilisha shauri hilo aliieleza mahakama hiyo jana kuwa bado hajakamilisha kuandaa uwamuzi huo hivyo anaiahirisha hadi Desemba 5 mwaka huu.

Januari 4,mwaka huu Jaji Shangwa aliliagiza Baraza Kuu la CUF lisitishe mchakato wa kuwasimamisha au kuwafukuza uanachama Rashid na wenzake wala kuendelea kuwajadili wakati wa mkutano wake wa Januari 4 uliofanyika Zanzibar.

Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo baada ya Rashid na wenzake kuwasilisha maombi Januari 3, 2012 wakiiomba mahakama hiyo iamuru mkutano huo ambao ulikuwa na lengo la kuwafukuza uanachama usitishwe hadi kesi yao ya msingi itakapomalizika.

Katika kesi yao hiyo ya msingi namba 1 ya mwaka 2012, Bw.Rashidi na wenzake wanahoji uhalali wa Kamati ya Nidhamu na Maadili ya chama hicho na uteuzi wa wajumbe wake.

Kamati hiyo ndio iliyowahoji Rashid na wenzake na kisha kupendekeza kwa Baraza Kuu wafukuzwe uanachama.

Pamoja na amri hiyo ya Mahakama CUF,iliendelea na msimamo wake wakuwavua uwanachamana ndipo Januari 10, mwaka huu, Bw.Hamad Rashid na wenzake waliwasilisha maombi mahakamani hapo wakiiomba iwaamuru viongozi wa CUF waitwe ili wajieleze ni kwa nini wasitiwe hatiani na kufungwa kwa kupuuza amri a Mahakama.

Pia anaiomba Mahakama ibatilishe uamuzi wa Baraza Kuu la CUF kuwafukuza uanachama na itamke kuwa wao bado ni wanachama halali wa chama hicho.


No comments:

Post a Comment