10 September 2012

VODACOM yazindua maonyesho barabarani kitaifa M-pesa


Na Jane Hamalosi

Kampuni ya Simu za mkononi V0DACOM imezindua maonyesho ya barabarani kitaifa ya M-pesa Dar es Salaam  


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza alisema kuwa Maonyesho hayo yatajulikana kwa jina la Tumewafikia Roadshow yanatazamia kuwaelimisha wateja kuhusu kujiunga na huduma ya M-pesa na umuhimu wa kutunza namba za siri.

"Huduma ya M-pesa imetoa njia nafuu na ya haraka katika kutuma na kupokea pesa,kuwaelimisha wateja katika maeneo mbalimbali ya nchi na yanalenga kuelimisha zaidi kuhusu kujisajili na huduma hiyo pamoja na viwango vya kutuma na kupokea pesa kupitia huduma ya M -Pesa,"alisema.

Alisema kuwa huduma hiyo ya kutuma fedha kupitia njia ya simu iliyozinduliwa tangu mwaka 2008 na imetoa njia rahisi na ya haraka katika huduma za kifedha kokote nchi nzima.

Pia ilifafanua kuwa huduma hiyo yenye mawakala zaidi ya 25000 nchi nzima inatoa huduma kwa wateja wapatao milioni 10 kupitia huduma ya M – pesa na wateja wa Vodacom wanaweza kubadili fedha kupitia mawakala wa M – Pesa na kuweza kutuma fedha hizo katika mitandao yote Tanzania kupitia njia rahisi ya simu.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa huduma ya M – Pesa ni ya gharama nafuu na inawapatia wateja njia rahisi yenye gharama nafuu pale wanapohitaji kutuma na kupokea pesa na kwamba wanajivunia mafanikio waliyopata kupitia huduma hiyo.


1 comment:

  1. CHADEMA MKO JUU NA TUKO NYUMA YENU HATUOGOPI UNYAMA WA POLISI NA MAAGIZO WANAYOPEWA NA CCM YA KUTUTISHA KWA KUUA WATU HOVYO. HAKI INACHELEWESHWA TU NA KAMWE HAIPOTEI

    ReplyDelete