07 September 2012
CHADEMA wasitisha M4C Iringa
Na Goodluck Hongo, Iringa
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesitisha mikutano yake ya Oparesheni Sangara na Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), iliyokuwa ikiendelea mkoani Iringa.
Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Bw. Hamad Yusuph, aliyasema hayo mjini hapa jana wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya vurugu zilizosababaisha kifo cha mwandishi wa Kituo cha Chanel Ten, marehemu Daudi Mwangosi.
Alisema uamuzi huo umefikiwa na viongozi waliokuwa wakiratibu operesheni hiyo ili waweze kurudi Dar es Salaam ambapo Jumapili wiki hii watakutana na Kamati ya Halmashauri Kuu kujadili vurugu hizo ambazo zilitokea wilayani Mufindi.
“Tumeamua kusitisha operesheni zetu kwa muda ili tukakakutane na Kamati ya Halmashauri Kuu tuweze kujadili matukio yaliyojiri likiwamo la kuuawa kwa mwandishi,” alisema Bw. Yusuph.
Katika hatua nyingine, Bw. Yusuph amemtupia lawama Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Mkoa hapa, Charles Kamuhanda na kudai ndiye chanzo cha vurugu zilizotokea Kijiji cha Nyololo.
Alisema baada ya viongozi wa CHADEMA kuwasili na Kamanda wa operesheni hiyo, Bw. Single Kigairo, katika eneo la Nyololo, polisi waliwazuia kufanya mikutano ya hadhara.
“Sisi tulikubaliana na agizo lao lakini tulimuomba Kamanda wa Polisi Wilaya ya Mufindi ili tufungue matawi ya chama na alikubali pamoja na kuwapa maelekezo askari wake wasifanye lolote, baada ya makubaliano hayo tulifanikiwa kufungua tawi la kwanza.
“Wakati tukiwa katika harakati za ufunguzi wa tawi la pili, ghafla aliwasili Kamanda Kamuhanda na kuamuru wafuasi watu wakae chini na kunyoosha mkono juu mikono juu agizo ambalo tulilizingatia bila matatizo,” alisema.
Aliongeza kuwa, jambo la kushangaza Kamanda Kamuhanda aliagiza wafuasi wa chama hicho wakamatwe ndipo vurugu hizo zilipoanza kutokea na kusababisha mauaji.
Akizungumzia mazingira yaliyosababisha kifo cha Mwangosi, alisema polisi ndio waliomuua wakati akimtetea mwandishi wa Gazeti la Nipashe, Bw. Godfrey Mushi, ambaye alikamatwa na polisi na kushambuliwa wakati akikimbia moshi wa mabomu.
Alisema kabla ya kukumbwa na umauti, marehemu Mwangosi alikuwa akirekodi matukio ya siku hiyo lakini baada ya vurugu hizo kuanza, kila mmoja alianza kutafuta njia ya kuokoa maisha yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

MASKINI CCM NA SERIKALI YAKE! WAMESHINDWA KUJITAKASA MBELE YA WANANCHI, KWA SABABU UFISADII AMBAO UMEANGAMIZA NCHI YETU KILA MTU ANAUONA NA HAKUNA JUHUDI ZINAZOONEKANA ZA KUREJESHA HAKI NA UTAWALA WA SHERIA NA HAKI KWA WOTE. KATIKA HALI HIYO, WANAAJARIBU KUIFUNGA MINYORORO NA KUKIZIBA MDOMO CHADEMA ILI KIACHE KUWAFUNGUA MACHO WATANZANIA AMBAO KWA MIAKA 50 WALIPUMBAZWA WASIJUE HAKI ZAO ZA KIRAIA NA ZA KIBINADAMU.LAKINI CCM NA SERIKALI YAKE WAMECHELEWA.HIKI NI KIPINDI CHA KILA MWANANCHI KUITUPA MINYORORO YA UKONDOO NA WOGA KWA SERIKALI AMBAYO KAIWEKA MADARAKANI YEYE. WANAUNGA MKONO CHAMA KINACHOONEKANA KIMEDHAMIRIA KULETU UHURU MPYA.HAPO NDIPO CCM NA SERIKALI VINAPOLAZIMIKA KUTUMIA VITISHO, IKIWA NI PAMOJA NA KUUA RAIA, ILI KUTUREJESHA KATIKA ZAMA ZA 'CHAMA KUSHIKA HATAMU'. WANAUA WATU KUSUDI WAOGOPE KUONESHA SUPPORT NA MATUMAINI YAO KWA CHADEMA. WAMECHELEWA. KAMA HAWAKUSOMA HISTORIA, BASI WAWAULIZE MAKABURU.
ReplyDelete