10 September 2012
PSPF kukabidhi nyumba 493 kwa wanachama wake
Na Heri Shaaban
MFUKO wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF)unatarajia kukabidhi nyumba 493 kwa wanachama wa Mfuko huo mwezi Oktoba mwaka huu,zilizojengwa eneo la Buyuni Manispaa ya Ilala.
Nyumba hizo zitakazokabidhiwa wanachama mwezi Oktoba zimejengwa kwa thamani ya shilingi bilioni 30 ambazo watapangishwa watumishi wa Serikali.
Akizungumza wakati wa kufanya ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Bodi ya mfuko huo,kukagua miradi hiyo Dar es Salaam jana,Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji PSPF Bi.Neema Muro alisema kuwa mradi huo wa PSPF kujenga nyumba ni endelevu ambapo utafikia nchi nzima.
Bi.Muro alisema kuwa mpaka sasa mradi huo umefikia mikoa sita Tanzania Bara, na kila mkoa wamejenga nyumba aina tofauti kwa wanachama wake ili mwanachama aweze kuchagua nyumba anayopenda.
"Tumejenga nyumba 668 kwa mikoa sita ambapo Dar es Salaam tumefanikiwa kujenga nyumba 493,Mtwara nyumba 50,Morogoro nyumba 25,shinyanga 50 lengo kuu ni kila mwanachama aweze kukopeshwa nyumba hzo"alisema.Bi Muro.
Alisema kuwa kila mwanachama atakayekopeshwa nyumba hizo atauziwa shilingi milioni 68 atalipa kwa muda wa miaka 25 atakuwa akikatwa kidogo kidogo.
Aidha alisema kuwa mradi huo umelenga kuwakopesha watumishi wa serikali ambao ni wanachama baadae mradi huo utawakopesha watu wa kawaida,Aidha alisema kuwa mpaka sasa wanachama 300 wameshatuma maombi ya kuomba nyumba hizo.
"Tumeshaongea na halmashauri zote nchini ili waweze kutupa maeneo ya kutosha kwa ajili ya ujenzi wa endelevu wa nyumba hizo.
Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw.Adamu Majingu aliwagiza watumishi wa Umma wawe na nidhamu wasipoteze ajira yao waweze kurejesha mkopo huo kwa muda muhafaka.
"Nawagiza watumishi wote wa serikali na wanachama waliokuwepo katika mfuko huu muwe na busara sehemu zenu za kazi mlinde ajira yenu PSPF ifikie malengo yake,"alisema.
Wakati huohuo Bodi hiyo imekagua jengo la kibiashara ambalo limejengwa na mfuko huo,litakuwa na ukubwa wa ghorofa 32 na litakamilika mwaka 2018 mradi ulioghalimu shilingi bilioni 182.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment