07 September 2012
Miili ya askari watatu JWTZ yawasili nchini
Na Stella Aron
MIILI ya askari watatu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), waliofariki dunia Darful, nchini Sudai walikokuwa wakilinda amani, imewasili nchini jana.
Marehemu hao ni Sajini Julius Chacha, Private Anthony Daniel na Koplo Yusuph Said ambao walikutwa na mauti baada ya gari walilokuwa wamepanda kusombwa na maji wakati wakivuka mto uliopo Kijiji cha Hamada, eneo la Manawasha ambapo miili hiyo ilipokelewa na Maofisa wa JWTZ, familia zao, ndugu, jamaa na marafiki.
Miili hiyo iliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Da es Salaam, saa 4:20 asubuhi, kwa Ndege ya Shirika la Kenya (KQ).
Baada ya miili hiyo kutelemshwa katika ndege, ilipelekwa eneo maalumu ambalo zilitolewa heshima za kijeshi ambapo familia zao, ndugu, jamaa na marafiki nao walipata fursa ya kutoa heshima zao.
“Wakati taratibu hizo zikiendelea, vilio vilitawala eneo hilo na baadae majeneza yao yaliyokuwa yamefunikwa Bendera za Taifa, yaliingizwa kwenye magari na kupelekwa Hospitali ya Jeshi Lugalo.
Marehemu Koplo Said anatoka Kikosi cha Mafunzo jijini Arusha, na Sajini Chacha na Private Daniel, wanatoka Kokosi cha 34 KJ Lugalo, Dar es Salaam.
Askari hao walikuwa katika batariani ya sita ya kulinda amani nchini humo ambapo batariani zote zilizowahi kwenda zimerudi salama.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment