17 September 2012
Mbunge: Mwenge wa uhuru marufuku *Adai ukifika jimboni kwake ataongoza kuuzima
Na Richard Konga, Arumeru
MBUNGE wa Arumeru Mashariki, mkoani Arusha, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Joshua Nassari, ameshikilia msimamo wa kupiga marufuku Mwenge wa Uhuru kufika jimboni kwake na kuwataka wananchi kuupuuza akidai hauna tija kwa maendeleo yao.
Aliwataka wananchi jimboni humo wakae mkao wa kula kwani jitihada za kuyatwaa mashamba makubwa yanayomilikiwa na wageni, zinaendelea hivyo wawe wavumilivu.
Bw. Nassari aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika mkutano wa hadhara wa Operesheni Sangara uliofanyika kwenye Kata ya Usa River, wilayani humo.
Aliwaataka wananchi kuupuuza mwenge huo, kutoshiriki kuchangia mchango wowote na kusisitiza kama mtu yeyote atabughudhiwa kutokana na ujio wa mwenge amualifu.
“Sioni sababu ya Mwenge wa Uhuru kukimbizwa maeneo mbalimbali nchini kwani badala ya kuhamasisha maendeleo, umegeuka sehemu ya ufujaji wa fedha za wananchi.
“Hali hii inachangia umaskini wa Taifa na kuhamasiha maovu katika maeneo yote ambayo mwengu huu unalala, nasema hivi, Mwenge wa Uhuru marufuku kufika jimboni kwangu.
“Mtu yeyote ambaye ataombwa mchango kwa ajili ya mwenge muiteni mwizi na mimi nitakuwa wa kwanza kuuzima baada ya kufika jimboni kwangu,” alisema Bw. Nassari.
Aliwataka wananchi hao kuendelea kushiriki shughuli za maendeleo bila kujali itikadi zao kisiasa na kuihadharisha Halmashauri ya Meru kuzingatia maadili ya utendaji kazi na kuacha kuwabughudhi wananchi kwa kuwachukulia bidhaa zao hasa wanapokusanya ushuru sokoni kupitia wakala wao.
Akizungumzia suala la uvamizi wa mashamba, Bw. Nassari
aliwataka wananchi kuwa wapole kwani anaandaa mkakati wa kuhakikisha ndani ya miaka mitatu, wamiliki wa mashamba hayo wanakimbia wenyewe ili wananchi waweze kujitwalia ardhi yao.
Katika hatua nyingine, Bw. Nassari alisema fedha zilizotengwa na halmashauri kwa maendeleo Kata ya Usa River, kuanzia Julai mosi mwaka huu hadi June mwaka 2013, ni sh. milioni 54.3 ambazo zitatumika kuboresha miundombinu na huduma ya maji safi.
Alisema ukarabati wa barabara kutoka Usa River hadi Magadilishu umetengewa sh. milioni nane na barabara za mji mdogo katika kata hiyo zenye urefu wa kilometa tano, zitagharimu sh. milioni 75.
Katika mkutano huo, wafuasi 15 kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), na Tanzania Labour Party (TLP) walitangaza kuvihama vyao vyao na kujiunga CHADEMA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Dogo sasa unaitafuta jela.
ReplyDeleteUsiende mikutanoni huku umevuta bangi. Utanyea debe muda si mrefu
mwehu huyu mbunge hawa ndio wataoleta balaa nchii wakiingia madarakani.
ReplyDeletembunge! ni ibara gani ya katiba ya jamhuri ya muungano imekupa uwezo wa kutangaza marufuku juu ya shughuli yoyote? hata olyimpiki ina mwenge!naona huna jipya,ni ujuaji tu.Acha hizo.heshimu mamlaka zilizopo na sheria za nchi,ujuaji huu Tanzania hautatupeleka kokote! maana sasa kila mtu anajua nani ataongozwa sasa.mbona hujapinga alama ya mwenge kuwa ktk coat of arms? msidanganye watu,siku mkigundulika patakuwa hapatoshi hapa.
ReplyDeletewanasiasa wengi wa Tanzania wananikera kani ni mamruki wa mawazo sio wao! hakika! hasa hawa wa upinzani,wanadhani madaraka ni kutokuwa na sheria kila mtu kuwa huru bila mipaka,nchi ipi hiyo,binafsi mimini mhafidhina wa UTAWALA WASHERIA.....PERIOD!
ReplyDeleteHakika Mh. Nassari hajuai anacho zungumza kwani akumbuke chama chake kinachangisha fedha kuto kwa hao walala hoi anao kataa mwenge utakapo kuja katika jimbo lake wasiuchangie.
ReplyDeleteChama kinapo changisha fedha hutumiwa kwa ajili ya mikutano ambyo anaghalama kubwa pia huwenda ikasababisha baadhi ya shughuli kusimama,
na kupo teza mapato kwa taifa na walala hoi wa tanzania jamani tumefika mahara sasa kufikilia na sisi kukubali kila jambo lisemwalo na hawa wabunbe wetu wengi na mamluki kama huyu.
Ni kweli mwenge wa Uhuru auna faida katika Nchi yetu kwani tunaitaji kubadilika ukiangalia Tanzania bado tuko nyuma kimaendeleo ivyo basi fedha ambazo zinatumika kukimbiza mwenge wa uhuru kila mwaka ziwekwe kwenye shughuli za kutengenezea miundombinu kwani sioni faida ya mwenge kila mwaka basi mkishindwa kuotoa basi fanyeni mwenge wa uhuru kila baada ya miaka mitano Jamani watanzania tubadilike namuunga mkona bwana jishua Nassari
ReplyDeletecha msingi hapa si kulaumiana, kitu cha msingi ni kuangalia na kutathimini, tangu mwenge wa uhuru uanze kukimbizwa hadi leo umeleta faida gani? tuweke pembeni itikadi zetu za vyama vya siasa na tusimame katika ukweli
ReplyDeleteama kweli huyu jamaa hapo juu mumiani,miradi mingapi ya maendeleo infunguliwa mwenge unapopita sehemu. hawa jamaa siwashangai maana usemaji huu unawasaidia kupata mlo, kumbukeni kusimamishwa kwa mkurugenzi wa tanesco Zitto alivyokurupuka, hadi leo najiuliza sijapata jibu. hapa tz ukisema sana unaunganishwa kwenye ulaji,ndio hawa jamaa. huyu jamaa mkutano mmoja huko kwao alisema anatangaza taifa jipya,kuna jamaa mmoja amenitonya huyu jamaa alikuwa anapuliza ganja (bangi) vibaya sana hana hakika kama kaacha
DeleteUKISIKIA MKAKATI WA KUFANYA NCHI ISITAWALIKE NDIO HUU. KWANI CHADEMA WAMEZOEA KUVUNJA SHERIA NA KUJA JUU YANAPOTOKEA MADHARA YANAYOSABABISHWA NA UVUNJIFU WAO WA SHERIA. WANANCHI TUSIPOKUWA MAKINI TUTAFANYWA WAKIMBIZI SASA HIVI.
ReplyDeleteHawa wanasiasa wa Bongo matapeli,hebu jiulizeni ati akifa mtu utawaona mbio kwenda kupandisha bendera zao. hii ni laana. wanachuria nchi iingie machafuko. leo hii wanagombea kichnga cha miezi saba huko Morogoro
ReplyDelete