16 August 2012

Usajili Yanga, Simba huu hapa *Redondo, Yondan wazua 'sokomoko'



Na Elizabeth Mayemba

TAYARI vigogo vya soka nchini Simba, Yanga na Azam FC vimeshaanika usajili wao kwa ajili ya msimu ujao wa ligi, katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Mashabiki wengi wa soka nchini walikuwa wakisubiri kwa hamu kubwa, usajili hasa kwa timu za Yanga na Simba kutokana na upinzani wao mkubwa uliopo.


Lakini usajili huu umejaa vituko ambapo kwa Simba na Yanga wote wamepeleka jina la beki Kelvin Yondan, huku Azam FC nao wakiwa wamepeleka jina la Ramadhan Chombo 'Redondo' ambaye yupo pia kwa Simba.

Hivyo Kamati ya ya Sheria, Maadili na Hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya Mwenyekiti wake, Alex Mgongolwa ndiyo itakayoamua hatima ya wachezaji hao.

Kwa upande wake Simba wachezaji waliosajiliwa makipa ni Juma Kaseja na Hamad Wazir, mabeki Said Nassoro 'Cholo'Amir Maftah, Juma Nyosso, Patrick Ochieng, Yondan, Paul Ngarema, Mussa Mude, Shomary Kapombe na Haruna Shamte.

Viungo: Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Haruna Moshi 'Boban' Salum Kinje, Redondo, Jonas Mkude, Haruni Chanongo, Omary Seseme na Hassan Kondo, washambuliaji ni Felix Sunzu, Uhuru Selemani, Abdallah Juma, Christopher Edward, Ramadhan Singano 'Messi', Kigi Makassy, Emmanuel Okwi na Daniel Okufo.

Pia Simba inamfanyia majaribio beki wa kati anayetokea nchini Mali Abdoul Karim.

Kwa upande wa Yanga makipa ni Yaw Berko, Ally Mustafa na Said Mohammed, mabeki Shadrack Nsajigwa, Juma Abdul, David Luhende, Yondani, Nadir Haroub 'Cannavaro', Godfrey Taita, Ladislaus Mbogo, Oscar Joshua, Stefano Mwasika na Mbuyu Twite.

Viungo: Athumani Iddi 'Chuji', Rashid Gumbo, Juma Seif 'Kijiko', Haruna Niyonzima, Omega Seme, Frank Dumayo, Nizar Khalfan na Idrisa Assenga. Wakati washambuliaji ni Said Bahanuzi, Hamis Kiiza, Simon Msuva na Didier Kavumbagu.

Hata hivyo klabu hiyo inawatafutia wachezaji wake Jerry Tegete na Shamte Ally timu za kucheza kwa mkopo, ambapo inadaiwa Toto African ya Mwanza inamuhitaji Tegete.

Kwa upande wao Azam imewasajili Mwadin Ally, Deogratius Munish, Nuhu Samih, Ibrahim Mwaipopo
Luckson Kakolaki, Erasto Nyoni, George Odhiambo, Abubakar Salum, Zahoro Pazi, Kipre Tchetche, Gaudence Mwaikimba, Joseph Owini, Aggrey Morris na Abdallah Ghulam.


Wengine ni Said Morad,Omary Mtaki, Ramadhan Chombo 'Redondo', Cosmas Fred, John Bocco, Abdi Kassim, Ibrahim Shikanda, Mcha Khamis, Himid Mao, Humud Abdulhalim, Jabir Aziz, Salum Waziri, Kipre Bolou, Rajab Ibrahim, Sunday Frank na Jackson Wandwi.

No comments:

Post a Comment